CCM, Serikali Mbili Zilizoboreshwa, na Hatima Ya Muungano

CCM, Serikali Mbili Zilizoboreshwa, na Hatima Ya Muungano

Hadi sasa chama hajajibu hoja, sijui kama anajua hilo. Serikali mbili zilizoboreshwa zitaboresha vipi muungano? Nimejadili kwanini maboresho hayo yatakuwa ni "kero zilizoboreshwa", na sio kingine. Sio yeye wala Mwanadiwani ambao wamejibu hoja hii.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mchambuzi hapa naomba kutofuatiana na wewe. Unajua kero zinazotajwa kuwa ni kerso za muungano zimewahi kujadiliwa mara nyingi. Sikumbuki vizuri, lakini JK na Amani Karume waliwahi kukaa na kujadili kero za Muungano, na baadhi ya matokeo ya vikao vile ni Zanzibar kujitangaza kuwa nchi kikatiba.

Ukianza kuangalia unaweza kuona kuwa CCM ndio imekuwa mstari wa mbele kuyumbisha na kuvuruga muungano. Kwanza ukiangalia kwa undani unaweza kuona kuna mambo yaliyoingizwa kwenye Muungano kinyemela (tofauti kabisa na yale ya msingi yaliyomo kwenye articles of union) ambayo ndio yamekuwa msingi wa kero za Muungano.

Tatizo ni kuwa baadhi ya members wanakwepa kusema CCM ndio chanzo cha matatizo yaliyopo kwenye muungano.
 
Mag3
Unakunywa ile kitu nyeupee; hebu nisome kwa kituo; mimi si muumini wa serikali 2 au 3 mimi ni muumini wa serikali 1 haya magumashi ya 2 tunayakubali ili kuweka mazingira ya 1; serikali 3 haziwezi kuondoa kero huo ndio ukweli zinalenga zaidi kuuvunja muungano; sasa kama hoja ni kuuvunja hatuna haja ya kujitwisha gharama za ziada na uvunjike tu; tunapoteza muda kujadili kitu ambacho hakina tija kwa mamilioni ya watanzania; hapa tujadili; ardhi; haki za binadamu; wanawake ; watoto; wakulima; wafanyakazi; maliasili na rasilimali za taifa kuondoa umaskini; tatizo lenu akili ni za kushikiwa Chadema kimepoteza mwelekeo kwa wananchi hakina hoja kuururdisha umaarufu wake kimeamua kudandia hoja ya Zanzibar wao hawana shida sana na muungano ila hawana jinsi ndio maana wamejitia kwenye UKAWA na CUF; kule Zanzibar CUF hapewi uraisi ashinde au assishinde hiyo ni juu yao serikali za Zanzibar inaitwa ya Mapinduzi akipewa CUF itwaitwaje?? hapo hakuna jibu ndio maana hapewi; hapo wafu 2 wamekutana hakuna hata kimoja kitachofanikiwa; Maalim anajua wazi Zanzibar bila Tanzania Bara kiuchumi haijiwezi ndio maana anataka mkataba yeye sio muumini wa 3 hapo huoni kama hitilafu za kiufundi? Hapo kwenye vyama tofauti 3 vishinde chaguzi ; Zanzibar CUF; Bara Chadema; Muungano CCM hapo patatawalika vipi mbona mnakuwa na mjibu mepesi ambayo hayaingii akilini?? Mag3 pata mirinda baridi tuongee vitu vyenye kumgusa mtanzania wa kawaida na vizazi vijavyo; ile kitu nyeupee achana nayo utaunguza maini kwanza haijapimwa halafu bima ya afya huna.
 
naam tuendelee na mjadala, bila kusahau kulinganisha na hoja za watetezi wa s2 walizoanza nazo huko Zanzibar.

Jee s3 ni matashi ya wananchi au UKAWA ?
 
Mchambuzi hapa naomba kutofuatiana na wewe. Unajua kero zinazotajwa kuwa ni kerso za muungano zimewahi kujadiliwa mara nyingi. Sikumbuki vizuri, lakini JK na Amani Karume waliwahi kukaa na kujadili kero za Muungano, na baadhi ya matokeo ya vikao vile ni Zanzibar kujitangaza kuwa nchi kikatiba.

Ukianza kuangalia unaweza kuona kuwa CCM ndio imekuwa mstari wa mbele kuyumbisha na kuvuruga muungano. Kwanza ukiangalia kwa undani unaweza kuona kuna mambo yaliyoingizwa kwenye Muungano kinyemela (tofauti kabisa na yale ya msingi yaliyomo kwenye articles of union) ambayo ndio yamekuwa msingi wa kero za Muungano.

Tatizo ni kuwa baadhi ya members wanakwepa kusema CCM ndio chanzo cha matatizo yaliyopo kwenye muungano.
Mkuu Bongolander, niliposema "kero zilizoboreshwa", maana yangu ni kwamba - kero hazipatiwi ufumbuzi bali zinawekewa rutuba zizidi kushamiri. Naunga mkono hoja yako ya msingi hapo juu.
 
Last edited by a moderator:
Mag3
Unakunywa ile kitu nyeupee; hebu nisome kwa kituo; mimi si muumini wa serikali 2 au 3 mimi ni muumini wa serikali 1 haya magumashi ya 2 tunayakubali ili kuweka mazingira ya 1; serikali 3 haziwezi kuondoa kero huo ndio ukweli zinalenga zaidi kuuvunja muungano; sasa kama hoja ni kuuvunja hatuna haja ya kujitwisha gharama za ziada na uvunjike tu; tunapoteza muda kujadili kitu ambacho hakina tija kwa mamilioni ya watanzania; hapa tujadili; ardhi; haki za binadamu; wanawake ; watoto; wakulima; wafanyakazi; maliasili na rasilimali za taifa kuondoa umaskini; tatizo lenu akili ni za kushikiwa Chadema kimepoteza mwelekeo kwa wananchi hakina hoja kuururdisha umaarufu wake kimeamua kudandia hoja ya Zanzibar wao hawana shida sana na muungano ila hawana jinsi ndio maana wamejitia kwenye UKAWA na CUF; kule Zanzibar CUF hapewi uraisi ashinde au assishinde hiyo ni juu yao serikali za Zanzibar inaitwa ya Mapinduzi akipewa CUF itwaitwaje?? hapo hakuna jibu ndio maana hapewi; hapo wafu 2 wamekutana hakuna hata kimoja kitachofanikiwa; Maalim anajua wazi Zanzibar bila Tanzania Bara kiuchumi haijiwezi ndio maana anataka mkataba yeye sio muumini wa 3 hapo huoni kama hitilafu za kiufundi? Hapo kwenye vyama tofauti 3 vishinde chaguzi ; Zanzibar CUF; Bara Chadema; Muungano CCM hapo patatawalika vipi mbona mnakuwa na mjibu mepesi ambayo hayaingii akilini?? Mag3 pata mirinda baridi tuongee vitu vyenye kumgusa mtanzania wa kawaida na vizazi vijavyo; ile kitu nyeupee achana nayo utaunguza maini kwanza haijapimwa halafu bima ya afya huna.

Kwa kauli yako hapo juu, mchakato wa katiba mpya uliogharimu wananchi zaidi ya shillingi billioni 250 billion hadi sasa ulilenga kuadaa tu wananchi. Hii ni dhambi kubwa sana mmefanya. Wananchi wametoa maoni yao, mmeyakataa, kumbe mna katiba yenu ya mafichoni. Mnajaribu lazimisha watu 400 kutuandikia katiba watu 45 million, hii ni sawa na 0.000009%, na bado mna question takwimu za tume kwamba sio representative of the population.

Hiyo serikali moja misingi yake ndio maboresho mnayofanya sasa kama nilivyojadili huko juu? Zile changamoto nilizojadili kwamba zitavunja muungano kwanini unakwepa kuzijadili kwa hoja, kwa mfano, bunge la Tanzania Bara, umakamu wa Urais wa Muungano kwenda kwa rais wa Zanzibar, kikwete kutangaza bungeni kwamba Znz watajinga na OIC, zanzibar watapewa gesi na mafuta yao wayaendeshe pamoja a karafuu zao kama bara wanavyoendesha dhahabu na kahawa zao etc etc, zote hizi ni hoja hamjajibu. Ndio kuelekea serikali moja kwa mwendo huu? Na iwapo znz katika kura ya maoni wanakataa serikali mbili zilizoboreshwa, mtafanya nini, mtawapiga mabomu ambayo Mwalimu mwaka 1968 alisema mbele ya intl media kwamba hatofanya hilo? Na iwapo Mwalimu alikataa serikali moja, tena wakati ule muungano una afya nafuu kuliko leo, hiyo serikali moja mnailetaje leo? Kwa kulazimisha znz? Wengi preference ni serikali moja lakini hatutaki Poteza muda kujadili "wishful thoughts" bali pragmatic issues kwa kuangalia the contemporary. Znz hawatakubali serikali moja, wala mbili, na sio CCM, serikali ya muungano, wala mabomu yatafanisha agenda yenu hii very arbitrary and undemocratic.

Hoja yako kuhusu uwezekano wa serikali tatu kuipa CUF urais znz, Chadema Tanganyika, na Ccm bara, aliyedhania alikuwa na majibu rahisi ni TANU baada ya kulazimisha suala la vyama vya siasa liwe la muungano 1964. Katika mkataba ule, hapakutajwa TANU, ASP wala neno chama cha siasa, na CCM ndio kabisa, ilikuja dandia treni kwa mbele na kupokonya usukani. Matokeo yake ndio taifa kupotea, muungano kuwa hatarini kuvunjika, na ccm kuanza kujichimbia kaburi. Unadhani kwanini mkataba wa muungano (1964) haukutaja masuala ya vyama vya siasa? TANU ilijipenyeza kwa hila kuanzia katiba ya muda (1965), unajua madhara yake yamekuwa nini? Hali unayojadili hapo juu kwamba upo uwezekano wa vyama tofauti kushinda sehemu tofauti, ni matokeo ya sera mbovu ya ccm ya muungano. Mwaka 1995, baada ya ujio wa vyama vingi, chama kilikuwa njia panda, kwa hofu uliyojadili hapo juu. Mwalimu akamuomba jaji bomani aokoea jahazi, mwalimu Akashauriwa nchi ifuate mfumo wa "shirikisho" kama marekani wa "mgombea mwenza", na hivyo ndivyo chama kikaepuka aibu ya kujitengenezea yenyewe. Tangia wakati ule, ndivyo Marehemu Dr. Omar, Dr. Shein na Dr. Bilal ndio wamekuwa makamo wa urais. Leo katika maboresho yenu ya serikali mbili, mnataka kumtoa bilal pale na kumpa shein awe makamu wa rais kwa kofia yake ya urais znz. Mnajua madhara yake? Nimejadili kwa kina huko juu. Kwa kifupi, kwa vile rais wa znz atakuwa ni makamu wa muungano automatically bila ya kujalisha rais wa muungano anatokea wapi, ccm inajenga mazingira ya nchi kuja kuwa na Rais na Makamo wake kutoka nchi jirani ya znz. Na siku inatokea ccm inamsimamisha mzanzibari urais wa muungano, ni nyie nyie mtajaa humu kupinga hilo na makundi yenu ya urais wakati chanzo cha tatizo ni nyie mnaomtukana warioba.

Bara hawataipigia ccm kura kwa rais na makamo wa muungano kutoka nchi jirani, na znz wataSema wanaonewa kwani hawatatoa tena rais wa muungano kwa serikali zenu zilizoboreshwa. Huo utakuwa ndio mwisho wa muungano, na ccm vile vile.

Nadhani hapa unaona bayana ni wewe na makada wenzako wasio na upeo juu ya janga hili ndio wavivu wa kufikiri.
 
Ahsante Mchambuzi MaCCM wanangangania uwanja mpana wa kifisadi, hawataki kuwajibika;
Kama hivi,
Mdude Chadema Nyagali > Sauti ya Tanganyika DENI LA TAIFA KUTOKA TRION 27 MWAKA JANA MPAKA TRION 40.6
KWA NINI DENI LA TAIFA LINAONGEZEKA WAKATI MATUMIZI NI YALE YALE?
1.MISHAHARA KWA WATUMISHI NI ILE ILE
2.BARABARA NI ZILEZILE.
3.HOSPITAL NI ZILEZILE NA BADO HAZINA MADAWA
4 KAMA NI KATIBA TOKA MCHAKATO UANZE KWA JAJI WARIOBA MPAKA BUNGE LA KATIBA NI BILON 82 TU NDO ZILIZOTUMIKA.

HUENDA MATUMIZI MABAYA YA SERIKALI NDIYO YANAYOSABABISHA DENI HILI KUWA KUBWA EBU TUANGALIE MATUMIZI KWENYE OFISI LA RAIS USUSANI SAFARI ZA NJE .

1.Rais kama anasafiri nje ya nchi huongozana na maafisa wasiopungua 22 wakiwamo afisa usalama madoctor n.k.

2.mjumbe ama afisa yoyote anayekuwa kwenye msafara wa rais analipwa 600000/= laki sita kwa siku sasa unapaswa kuzidisha pesa hiyo kwa wajumbe wote 22 ambapo utapata milion 13200000/=milion kumi na tatu laki mbili kwa siku.

3.mjumbe ama afisa anayekuwa kwenye msafara wa rais analala HOTEL yenye thamani ya DOLA 1200 ambayo sawa na 1900000/= milion moja na laki 9 pesa hiyo uizidishe mara wajumbe 22 unapata 41800000/= milion arobaini na moja na laki nane kwa siku moja

4.hivyo basi ukijumlisha posho na malazi ya maafisa ama wajumbe kwenye msafara wa rais unapata shilingi 55000000/=milioni hamsini na tano kwa siku moja.

jumla ya safari za rais nje ya nchi ni 395 ukizidisha 395 mara shilingi milion 55 utapata hesabu kamili ya matumizi ya safari zote za rais nje ya nchi kwa maana calculator yangu imenock kwa kulingana na ukubwa wa hesabu.

5.bado usafiri ndege ya rais iliruka angani kwa muda wa saa moja hutumia milion 16.2
bado matumizi mengine kwenye ofisi ya rais kama vile safari za ndani n.k

6.baraza la mawaziri ;waziri mmoja hutengewa mafuta lita 200 ambazo sawa na laki nne 400000/= kwa siku ata kama anakoenda hakujulikani na hakuna faida kwa serikali na kuna mawaziri 60 ukizidisha idadi ya mawaziri hao mara laki 4 unapata 24000000/=milion ishilini na nne kwa siku moja

SASA NDUGU ZANGU KWA MATUMIZI HAYA KWA NINI TAIFA LISIPATE DENI KUBWA?
KWA NINI WATANZANIA MNAENDELEA KUKUMBATIA CCM KWA MATUMIZI MABAYA KAMA HAYA WAKATI HUO KUNA SHULE HAZINA MADARASA?

TAFAKARI CHUKUA HATUA
That's a tip of the iceberg!!
 
Mtumishi Wetu, asante sana kwa takwimu na uchambuzi huu muhimu juu ya gharama. Haya ni masuala ambayo kina chama, Kobello, MwanaDiwani, Mdondoaji, hawataki kuyajadili. Ninaendelea kuandaa uzi mahususi kabisa wa gharama za serikali mbili, na nitahitaji sana mchango wako; serikali mbili zinafuja sana hela za walipa kodi, zinaficha so much leakages. Accountability na transparency on tax payers money haipo kabisa. Hata DFID ya Uingereza ilitoa ripoti kwamba about 35% ya fedha zinazotengwa kwa ajili ya bajeti kila mwaka wa fedha zinapotea tu bila ufanisi wowote katika uchumi lakini pia maisha ya walio wengi. Hizi ni nje ya fedha zinazopotea kupitia misamaha ya kodi kwa wageni lakini pia wakubwa ambao wana makampuni makubwa yanayokwepa kodi kwa ulaghai wa tax exemptions. Wanaolipia muungano huu wenye gharama kubwa wengi wao ni walahoi, wakulima, wafanyakazi kupitia kodi mbalimbali, sio wakubwa ambao ingawa mishahara yao inakatwa kodi, wanarudisha makato hayo mara mia zaidi kupitia ufisadi, na posho za ajabu ajabu kama ulizojadili hapo juu.

Serikali tatu itafumua yote haya, leakages in public finance zitabanwa sana, serikali itakuwa na fedha nyingi zaidi, umma utapata more incentives kulipa kodi kwani under fiscal decentralization ya serikali tatu, matumizi ya kodi yatakuwa wazi zaidi, faida zake zitakuwa wazi zaidi, tutaweza hatimaye kuanza t link public finance and politics on the ground. Nitayajadili haya kwa kina kwenye uzi ninaoandaa. Until then, tafadhali endelea kutusaidia na takwimu muhimu kama hizi.
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi
hivi una matatizo ufahamu? Muungano ni sehemu ndogo sana ya mapendekezo ya katiba yapo mambo ya msingi ambayo yanamgusa kila mtanzania na yana umuhimu kwenye maisha yao ya kila siku; tatizo nyie Chadema mmepoteza mwelekeo hamna jipya la kuwaeleza watanzania ndio maana mmeng'ang'ania kwenye muungano na serikali 3; yapo mambo ya msingi nimeyagusia hapo juu kwa hiyo hizo bilioni 250 hazijapotea bure hivi Zanzibar leo waamke waseme hawataki muungano tutaacha kujadili mustakabali wetu kwasababu muungano halitakuwemo kwenye katiba?? halafu ukiandika jaribu sana ku hit kwenye point maelezo yanakuwa mengi kiasi unapoteza mtiririko.
 
Hii tabia ya kutajana majina inanikera sana.......ina maana sisi akina Mjini chai tukae Pembeni tusichangie hoja..........?
 
Hoja ni kuijadili Rasimu......Kwa nini wanadandia hoja ambazo hazipo kwenye Rasimu naona Wabunge wa BMK hawapo makini........EL bhana anaivuruga sana hii nchi...........
 
Hii tabia ya kutajana majina inanikera sana.......ina maana sisi akina Mjini chai tukae Pembeni tusichangie hoja..........?

Mkuu mjini Chai, hii sio kero tu bali pia ni dharau. NI kweli watanzania wote nmi wadau wa mambo ya Tanzania, hata kama maoni yetu ni ya kijinga yanapaswa kusikilizwa. Ni afahdahri tuambiwe yepi ni ya maana ya yepi ni yasio na maana na sababu zake za msingi ili tujue ni ya kijinga, na sisi wenyewe tuache.

Mimi nakasirika sana kuona kuwa sehemu ndogo sana ya watu ndani ya CCM wanataka kuhodhi mwelekeo wa namna ambavyo watanzania tunakata kuongozwa. Sisi ndio tuliowapa dhamana ya kutuongoza, na ni sisi ndio tunatakiwa kutoa dhamana ya namna tunavyotaka kuongozwa. Kuwapa dhama ya kuiongoza hakuna maana kuwa wanaweza kuamua mambo kwa maslahi yao na sio kwa maslahi ya taifa. Kwa mantiki hiyo hata mawazo na maoni yetu kuhusu namna tunavyotaka kuongozwa yanatakiwa kutoka kwetu. Na yawe huru.
 
Tawire..............
 
Mchambuzi
katika bandiko #265 unalazimisha kupewa majibu ya mapendekezo; hilo ni kupoteza muda ni sawa na kujadili ndoto; mapendekezo hayakidhi haja zote lakini kwasababu hayajawa maamuzi rasmi ya wananchi hatuna sababu ya kuumiza vichwa subiri yapite yawe maamuzi; kila siku kuna mapendekezo mapya CCM milango yetu ipo wazi; mapendekezo yetu hayatokani na vikao vya sebuleni kwa baba mkwe ni mawazo ya wananchi kwa maana majibu yapo kwasababu yalijadiliwa kwa mapna na marefu.
 
Serikali tatu itafumua yote haya, leakages in public finance zitabanwa sana, serikali itakuwa na fedha nyingi zaidi, umma utapata more incentives kulipa kodi kwani under fiscal decentralization ya serikali tatu, matumizi ya kodi yatakuwa wazi zaidi, faida zake zitakuwa wazi zaidi, tutaweza hatimaye kuanza t link public finance and politics on the ground. Nitayajadili haya kwa kina kwenye uzi ninaoandaa. Until then, tafadhali endelea kutusaidia na takwimu muhimu kama hizi.
Itabidi utuambie how, siyo ku-assume tu kuwa serikali tatu zitakuwa na malaika automatically.
Fiscal responsibility inaweza kuwepo hata kwa mfumo huu, mradi tu wananchi na viongozi waamue. Hata bunge la sasa hivi linaweza kuweka debt ceiling, linaweza kuondoa misamaha ya kodi nk. tatizo siyo kwa sababu hakuna uwezo, sababu ni kutotaka na kutowajibishwa na wananchi.
That can happen even with 1000 governments. Mimi nasubiri tu huo uzi.
 
BLK lilianza kwa mjadala wa sura ya kwanza na sita. Katika hatua hiyo, ccm ililenga kuhakikisha inabomoa chochote kinachojenga mazingira ya serikali tatu au uzinduzi wa Tanganyika. Baada ya kufanikisha hilo, CCM ingepenyeza maboresho niliyojadili humu. Wazungumzaji wakuu na rasmi kwa haya wannasubiri muda muafaka. Lakini pia Kama ulikuwa unafuatilia bunge, wapo baadhi wa wachangiaji waliojitambulisha kutokea makundi ya "walio wengi" walisikika wakisema kwa juu juu kwamba Zanzibar itaruhusiwa kukopa, na mengine mengi niliyojadili, huku wakijenga hoja kwamba serikali mbili zitaboreshwa na kutatua kero za muungano. Inawezekana ukawa sahihi kwamba hoja yangu ni "bad timing", inahitaji kusubiri, lakini pia wapo wenye kuona kwamba, since huo ndio ukweli, hakuna ubaya kufanya a pre-emptive strike. All that said and done, you have a choice kusubiri kuchangia hadi August kama una amini ndio "good or best timing".
Ndiyo maana nimechangia kwa kusema kuwa bado hujaonyesha source ya mjadala, hivyo nafikiri kwamba ungeweza kuwa na hoja iwapo vitu vingewekwa wazi, lakini hiyo rasimu bado haijaletwa barazani.
 
La muhimu kabla ya kukubali S2, CCM watusaidie kwanza tupitishe hayo mapendekezo ya kuboresha hali ya sasa, kama ni rahisi hivyo kufanyika, (yenye katiba kinzani katika Tanzania). Wasi wasi ni dhahiri haitakuwa rahisi kupitisha yale maboresha muhimu (e.g. yaliyoingizwa katika katiba yao ya sasa) wazanzibari wakaridhia, tukijua kutoka huko nyuma kuwa ni kero nzito kwao na si vizuri wakaburuzwa.
 
Zaidi ya Miezi minne iliyopita, tulijadili juu ya rasimu ya mafichoni ya CCM iliyo sheheni Viroja vya serikali Mbili zilizoboreshwa. Lakini Kama kawaida, Yao, wale wote ambao wamekuwa wanakaririshwa misimamo ya chama hivyo kushindwa kuchambua issues objectively walikejeli hoja zetu, huku wakihoji hiyo rasimu ya mafichoni Ipo wapi. Sasa tunaona jinsi gani Kamati za BLK kupitia wajumbe wanaojitambulisha Kama ni "wengi", wakileta maoni Yale Yale tuliyojadili miezi minne Iliyopita. Hivi ni Viroja ambavyo Kama Aliyosema EMT, ni sinema inayokaribia ukingoni muda sio mrefu.

Cc MwanaDiwani, chama, Kobello, Dingswayo, Mag3 Nguruvi3 JokaKuu, Jasusi, Pasco, MJINI CHAI, Bongolander, Mtanganyika

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Hivi ni Viroja ambavyo Kama Aliyosema EMT, ni sinema inayokaribia ukingoni muda sio mrefu.

Well, inawezekana cinema ndo kwaanza inanoga maana kuna suspense za hapa na pale.

Habari zilizopo (kama ni za kweli) ni kuwa Mahakama Kuu imesitisha Bunge la Katiba kuendelea na vikao vyake.
 
Zaidi ya Miezi minne iliyopita, tulijadili juu ya rasimu ya mafichoni ya CCM iliyo sheheni Viroja vya serikali Mbili zilizoboreshwa. Lakini Kama kawaida, Yao, wale wote ambao wamekuwa wanakaririshwa misimamo ya chama hivyo kushindwa kuchambua issues objectively walikejeli hoja zetu, huku wakihoji hiyo rasimu ya mafichoni Ipo wapi. Sasa tunaona jinsi gani Kamati za BLK kupitia wajumbe wanaojitambulisha Kama ni "wengi", wakileta maoni Yale Yale tuliyojadili miezi minne Iliyopita. Hivi ni Viroja ambavyo Kama Aliyosema EMT, ni sinema inayokaribia ukingoni muda sio mrefu.

Cc MwanaDiwani, chama, Kobello, Dingswayo, Mag3 Nguruvi3 JokaKuu, Jasusi, Pasco, MJINI CHAI, Bongolander, Mtanganyika
Mchambuzi, hayo mambo sisi wengine tuliyaona toka mapema kabisa na kwa kweli nawapongeza sana UKAWA kutokubali kushiriki huu upuuzi unaofanyika ndani ya eti Bunge Maalum La Katiba. Nakumbuka jinsi Kobello alivyokuwa akitetea kwa kudai eti tukiacha vipengele viwili vilivyohusu muundo wa Muungano vilivyozua utata toka mwanzo vingine kwenye rasimu havingeleta taabu. CCM hawakuwa na nia wala hawajawahi kuwa na nia ya kuandika katiba mpya kwa sababu katiba mpya ingehatarisha mipango yao ya kuhakikisha hawatoki madarakani...tazama wanavyoichachana rasimu na hasa vile vipengele vinavyobana kutowajibika.

Kinachofanywa ndani ya BMLK ni marekebisho/maboresho ya katiba ya zamani na kusema kweli hayakuhitaji Bunge Maalum, yangeweza kufanywa na Bunge la kawaida na hivyo tungeokoa mabilioni yaliyotumika toka mchakato uanze. Hivi kuna mtu yeyote amewahi kuhoji pesa zilizokuwa walipwe wajumbe waliosusia hili Bunge zinakwenda wapi? UKAWA kususia Bunge imekuwa neema kubwa kwa utawala...hizo pesa ambazo wangelipwa si ajabu zinaingizwa kwenye mfuko ule ule zilikoenda za chengi ya rada na ESCROW. Usiku na mchana wanakesha wakiomba msimamo wa UKAWA usibadilike wazidi kufaidi kwa kutafuna shamba la bibi kama nzige.
 
Back
Top Bottom