Mungu ni mwema kila wakati na atatutendea Taifa letu yaliyo mema tu. Naamini Magufuli amechokwa na kila mtu mpaka na wale waliomsaidia kuiba kura akina Lubuva, Kipilimba, Nape na Kinana. Na lazima Mkutano Mkuu umtose kama mgombea wa CCM hapo August 2020. Kama washauri wake aliamua wawe ni akina Makonda, Bashiru Ally na Pole pole badala ya wazee wetu wastaafu wenye busara na upeo basi anawajibika kwa haya yanayotokea.
Naamini kama CCM wasipomtosa 2020 tutarajie machafuko makubwa nchini kwa kuwa Magufuli hawezi akapata hata 20% ya kura za kupigwa kwa sanduku la kura. Badala yake atafanya vituko zaidi kuliko uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2019. Na wananchi hawatavumilia.
Atambue tu kuwa toka Uhuru wa Tanzania mwaka 1961 Taifa letu halijawahi kuwa na mstakabali mbovu wa kisiasa na kidiplomasia ya Dunia kama kipindi hiki. Kitendo cha Paul Makonda kuzuiwa kwenda Marekani ni ujumbe tu kuwa kuna mengi yanafuata. Mojawapo ni hili hapa;
"The administration’s expanded travel ban now affects close to a quarter of the population of the African continent."
qz.com
Magufuli asijidanganye kuwa kwa vile huwa hasafiri nje ya Tanzania basi hayamhusu. Hapana, jina lake na la Kabudi, Mambosasa lipo tu kwa watu ambao hawatakiwi kwenda US, muda tu wa kutaja haujafika
Wamarekani wanazo details za udhaifu wa Serikali ya Magufuli ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu, ukosefu wa utawala wa sheria, utekaji wa wakosoaji, kubambikia watu kesi, mauaji na ukandamizaji wa demokrasia ya vyama vya upinzani.
Magufuli asijidanganye kuwa anaweza kufanya Tanzania anavyoyaka kama anavyofanya kwenye familia yake, hapana!! Utulivu wa Tanzania una masilahi makubwa kwa nchi za Magharibi hasa US, UK na Germany. Tanzania ikitulia maana yake eneo zima la maziwa makuu limetulia. Waganda walipochafuana miaka ya 1970s walikimbilia Tanzania, Warundi na Wanyarwanda walipochafuana miaka ya 1960s nao walikuja Tanzania. Kuanzia 1960 mpaka 1990s Tanzania ilikuwa Makao makuu ya vyama vya ukombozi vya Afrika kama SWAPO, MPLA, ANC, PAC na ZANU.
Hata Wakenya mwaka 2008 walipouana ni Tanzania iliyohusika kuwapatanisha.
Nchi za Magharibi haziwezi kukubali Magufuli na Makonda waharibu amani ya nchi hii. CCM hamujachelewa mtupeni huyu Magufuli kwenye bahrii kama Yona alivyotupwa alipokataa kwenda NINAWI ili chombo kiendelea na safari. Mkishindwa ataondolewa kwa nguvu na CCM itakuwa imekwisha kama iliyokwisha UNIP ya Kaunda au KANU ya Kenyatta. Uchaguzi ni wenu na muda munao, na uwezo munao.