Black Sniper
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 32,406
- 55,148
Naona watu wanajadili zuio la Makonda kuingia Marekani badala ya kujadili sababu zilizopelekea hilo zuio. Wenye akili ndogo wameanza kusema "Kwani Marekani ni mbinguni? Kwani asipoenda atapungukiwa nini?" Hii ni comment ya Mbunge mmoja wa CCM kule Twitter.
Lakini hoja si Makonda kuzuiwa kuingia Marekani au kuingia Chato. Hoja ya msingi ni madai yaliyotolewa na Marekani kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na Makonda.
Pamoja na mambo mengine, Pompeo amesema Marekani ina USHAHIDI kuwa Makonda ameshiriki KUDHULUMU HAKI YA KUISHI KWA WATU KADHAA. Hii ni kauli ngumu sana, inayotafakarisha sana.
Kudhulumu haki ya watu kuishi means kuamua kumuondolea mtu uhai kabla ya wakati wake. Je ni kweli Makonda amefanya hayo? Kwa akina nani? Kwa ruhusa ya nani? Kwa sababu gani? Lini? Wapi? Na kwanini?
Kumbuka taifa lenye teknolojia kubwa kama Marekani linaposema lina USHAHIDI juu ya jambo fulani bila shaka limejiridhisha vya kutosha.
Kwahiyo ili tuwe na mjadala wenye tija tuachane na kujadili zuio, tujadili sababu zilizopelekea hilo zuio. Hata kama asingezuiwa kwenda Marekani, lakini tuhuma alizotajwa nazo ni kubwa sana. Zinaogofya, zinatafakarisha, zinatisha. Kumbuka Marekani imesema ina USHAHIDI na kumbuka Pompeo alikua Mkurugenzi wa CIA kabla ya kuwa Waziri.!
Kwa hiyo Simu zote zinasikilizwa kila kukicha
Hawa watu hata ukiwaalika kule wanaacha vinasa sauti vigogo kama punje ya mchele [emoji23][emoji23]
Sent from my iPhone using Tapatalk