kichakaa man
JF-Expert Member
- Oct 20, 2011
- 5,500
- 5,164
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Safari hii bundi amepiga kambi Lumumba. Wapiga kura hawadanganyiki tena.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Safari hii bundi amepiga kambi Lumumba. Wapiga kura hawadanganyiki tena.
Kwa miaka mitano uwanja ulikuwa ni wetu. Tumewafunga minyororo ya miguuni, mikononi na hata shingoni huku midomo yao tumeyafunga kwa vitambaa. Uwanja ulikuwa ni wetu, tumewakejeli, tumewasimanga tumewaita kila haina ya majina huku wasiojulikana wakiwafanyia kweli bila kujulikana.
Tumewasweka lupango, tumewanunua kana kwamba ni mitumba. Tumetumia vyombo vya habari peke yetu. Tuliwazibia kila kona, ilikuwa ni CCM. Tumetembea vifua mbele huku tukijinasibu kama wana maendeleo. Polisi wamewatesa sana wana CHADEMA. Hawa jamaa wamekiona cha moto lakini bado wanapumua !
Tumeimba singeli za Stigllers Gorge, tumenunua midege, SGR, Flyovers, elimu bure, na kila haina ya maendeleo. Hatukuwa na kosa, tulikuwa weupe kama theluji bila kujua kwamba tulikuwa wachafu mithili ya nguruwe alijetumbukiza kwenye matope.
Ghafla bin vuu, maendeleo yote tuliyokuwa tunajivunia imegeuka kuwa kamba ya kutunyongea. Mwenyekiti wangu kakamatwa suruali chini Kibiti, "Anatoa Rushwa".
Maendeleo ya kujenga Uwanja wa ndege Kijijini Chato imegeuka kuwa kashfa ya karne.
Laiti tungalijua, tungewahacha hawa watu waongee, maana watu wangechoka mapema na hii mashambulizi yao isingekuwa kivutio kama ilivyo leo. Kwa hali iliyopo, ukigeuka kulia, watu wanataka kusikia nondo za Lisu. Kuhsoto wataka kumsikiliza Lissu. Kwenye daladala lissu, sehemu za starehe ni Lissu. Makanisani Lissu. Vijijini Lissu kila kona Lissu na Chadema.
Ingawa tumeziba vyombo vya habari kutangaza habari za Chadema, Instagram na mitandaoni ni hoja nzito za Lissu. Mbaya zaidi, muda wa kujitetea haitoshi nikiangalia miaka mitano na siku 60 za kampeni. hesabn haiku bali. Hatuwezi kutoboa
Mikutano yetu iliyokuwa Mubashara toka Ikulu, leo imegeuka kuwa Maigizo ya wana usalama kuchoma mahindi na bastola kiunoni. Maendeleo yetu ya Flyovers imekuwa Wapinzania kutaka kuuza Scrapper. Hoja mfu!
Bandugu kwa miaka mitano tumelikoroga. Sasa inabidi tulinywe. Mwaka huu kuiba kura ni kaa la moto na atakayethubutu anakwenda na maji.
Ama kweli majuto ni mjukuu!
Ukiwaaambia ww sio mzalendo.Katika Awamu nilizoshuhudia nikiwa najitambua aisee hii awamu iacheni tu imekithiri sana kwa vitu viwili pacha "UONGO NA UNAFKI"
Mwenyekiti wetu apatia huruma.Juzi namshangaa anavyolalamika eti wakipata Urais Wapinzani watavunja flyover na ndege zitakuwa scrapers. Nikacheka sana. Nikajisemea moyoni yaani mwenyekiti amekata tamaa hivi kiasi hana hoja tena??
Kweli wakati ni ukuta.
Sana na hapo Kampeni bado. Yaani yule jamaa alidhani kujenga fly over mbili Dar zitambeba hadi huko Katavi na Urambo.😅😅Mwenyekiti wetu apatia huruma.
Ndugu yangu, bao la mono gumu sana maka huu. Ubunge tunapoteza.
[/QUOTEafdhali
Hio quotation ya ukweli.Heri kijana mdogo mwenye hekima kuliko mfale mzee mpumbavu asiyetaka kusikia maonyo
Tukishindwa kujibu hoja tunakwambia kunaviashiria vya uvunjifu wa amani, ukitugonga kwenye msumari umetumwa na mabeberuSiamini kabisa. Tumewaburuza jamaa kwa miaka mitano leo tunaonekana kama mazwazwa hata kujitetetea hatuwezi tunabakia kuwatumia wakina TID. Shame on Polepole. Sijui walimuokota wapi!
[emoji16] You nailed itNimekumbuka kisa cha vazi la ajabu la mfalme aliyekua anatembea uchi huku umati ukimshangilia mpaka pale mtoto mdogo (Lissu) aliposema "lakini mfalme yupo uchi"
CCM haina hojaNimependa hii paragraph [emoji1787]
Mikutano yetu iliyokuwa Mubashara toka Ikulu, leo imegeuka kuwa Maigizo ya wana usalama kuchoma mahindi na bastola kiunoni. Maendeleo yetu ya Flyovers imekuwa Wapinzania kutaka kuuza Scrapper. Hoja mfu!
Alikuwa rasi.Hivi mfalme alikua amenyoa? Nje ya mada lakini
Hahaa kwa hiyo mwenye kiti wenu ni mfalme juha !!?Nimekumbuka kisa cha vazi la ajabu la mfalme aliyekua anatembea uchi huku umati ukimshangilia mpaka pale mtoto mdogo (Lissu) aliposema "lakini mfalme yupo uchi"