CCM: Tunafuatilia mienendo ya viongozi wetu wanaopotosha umma, kwenda kinyume na maelekezo ya Mwenyekiti wetu

CCM: Tunafuatilia mienendo ya viongozi wetu wanaopotosha umma, kwenda kinyume na maelekezo ya Mwenyekiti wetu

20210723_082645.jpg
 
Chama Cha Mapinduzi kinafuatilia kwa makini mienendo ya baadhi viongozi wake.

Chama Cha Mapinduzi kinafutilia kwa makini mienendo ya baadhi viongozi wake ambao wamekuwa wakipotosha Umma na kwenda kinyume na maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu na maadili ya Chama.

CCM inawahakikishia wanachama na watanzania kuwa hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wote ambao wanatumia nafasi hiyo kusukuma ajenda zao binafsi, kwa mujibu wa Katiba, kanuni za maadili na uongozi za CCM

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi.

View attachment 1869351
"Chama cha majambazi kinafuatilia kwa makini mienendo ya majambazi wake"

Kwa sababu hatuna viongozi kwenye hicho chama, ni wahuni kama kilivyo kikundi chenyewe
 
Kwa mujibu wa katibu mwenezi ndg Shaka wote waliopinga maagizo na maelekezo ya mwenyekiti juu ya suala la chanjo ya korona na tozo wajiandaye kukiona cha mtema kuni.

Source:ITV
Danganya toto tu hiyo walikuwa wanaandaa mazingira ya kumpeleka Mbowe gerezani
 
CCM hampendi changamoto kabisa.

Taarifa zilizopo ni kwamba bibi ameagiza Gwajima afukuzwe chama kwa msimamo wake wa kupinga chanjo ya korona.

Hatari Sana hii.

Maoni hayapigwi mawe.....Kikwete
Huu upendeleo mbona Diallo bado mwenyekiti au yeye matamshi yake hayawahusu?
 
Huyo dogo hana kingine cha kueneza zaidi ya kutishia watu wazima nyau?
 
NASIMAMA NA MH.SHAKA HAMDU SHAKA....

Haiwezekani chama chetu bora kiwe na makada wasioheshimu maelekezo kuntu ya mh.Mwenyekiti wetu...

#HatuaKaliZichukuliwe
#HongeraMh.ShakaHamduShaka
#NchiKwanza
#JMTMilele
#SiempreCCM
#HastaLaVictoriaCCM
 
Hii inatia moyo. Upotoshaji uchwara haukubaliki.

Cc: Jumbe Brown
.....haukubaliki kabisa kabisa....

Komredi pamoja na kuwa tumekuwa na mawazo kinzani kila uchao.....

Ila katika hili TUNASIMAMA PAMOJA kukataa nidhamu mbovu ya kutomheshimu mh.Rais wa JMT na mwenyekiti wa CCM.....

#NchiKwanza
#KwaMaslahiYaTanzaniaTukoPamoja
#JMTMilele
#KaziIendelee
 
Chama Cha Mapinduzi kinafuatilia kwa makini mienendo ya baadhi viongozi wake.

Chama Cha Mapinduzi kinafutilia kwa makini mienendo ya baadhi viongozi wake ambao wamekuwa wakipotosha Umma na kwenda kinyume na maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu na maadili ya Chama.

CCM inawahakikishia wanachama na watanzania kuwa hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wote ambao wanatumia nafasi hiyo kusukuma ajenda zao binafsi, kwa mujibu wa Katiba, kanuni za maadili na uongozi za CCM

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi.

View attachment 1869351
CCM inamuogopa sana Askofu Rashid Gwajima kwani ana watu,mkileta fyoko anaweza kuwafanya chochote,hamumuwezi huyo pornstar.
 
Siku hizi ni mwendo wa matamko tu bila matendo. Shaka we andaa wabunge wa chama chako na UVCCM wakinge mabega kuhamasisha wananchi wengine
 
Huyo dogo hana kingine cha kueneza zaidi ya kutishia watu wazima nyau?
Ikiwa Manara tu anapigania maslahi ya SSC kufa na kupona....iweje iwe tofauti kwa mh.Shaka Hamdu Shaka anayekisemea chama kinachoongoza dola la JMT?!!!

#NidhamuKwanza
#NchiKwanza
#JMTMilele
#KaziIendelee
 
Kwa mujibu wa katibu mwenezi ndg Shaka wote waliopinga maagizo na maelekezo ya mwenyekiti juu ya suala la chanjo ya korona na tozo wajiandaye kukiona cha mtema kuni.

Source:ITV
Ntashangaa president Samia na Mohamed mcherenga , na Shaka , na mkuu wa TISS, Kama wataacha kumshughulikia huyu taperi mmoja asiye na heshima kwa mamlaka,

Wakimuacha wajiandae atafanya upuuzi na dharau zaidi ya hizo..

Gwajima inatakiwa itumike namna Kama yakufuta maandishi kwenye kitabu, azimwe tu, Ni mtu hatari sana
 
Back
Top Bottom