CCM: Tunayataka mataifa yote duniani yaliyoiwekea vikwazo nchi ya Zimbabwe kuondoa vikwazo hivyo mara moja

CCM: Tunayataka mataifa yote duniani yaliyoiwekea vikwazo nchi ya Zimbabwe kuondoa vikwazo hivyo mara moja

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
39,468
Reaction score
31,952
Makamu Mwenyekiti wa CCM BARA ataongea na umma juu ya msimamo wa chama na diplomasia ya kimataifa kutokea Ofisi ndogo za CCM - Lumumba.


UPDATE
Itakumbukwa kwamba Mkutano wa 10 wa Vyama vya Ukombozi vya Kusini mwa Afrika uliofanyika Zimbabwe tarehe9-12 Septemba 2019 uliazimia Vyama kupaza sauti kwa pamoja kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kuondoa mara moja vikwazo dhidi ya Zimbabwe

Kwa kutambua Jukumu letu ktk kuimarisha Umoja, Mshikamano wa Waafrika na kuendeleza mapambano dhidi ya Ukoloni Mamboleo, kupiga vita Ubeberu na Ubaguzi wa aina yoyote pamoja na kuimarisha uhusiano mwema na Vyama vyote vya Siasa vya Nchi nyingine vyenye itikadi kama ya CCM

CCM kinaamini kuwa vikwazo dhidi ya watu wa Zimbabwe ni muendelezo wa fikra na matendo ya uonevu na unyonyaji kwa Waafrika. Watu wa Zimbabwe wameonewa kiasi cha kutosha, na sasa tunaazimia kuwa uonevu huo ufike mwisho

Vikwazo dhidi ya Zimbabwe vimewekwa takribani miaka 19 sasa tangu mwaka 2000. Wanaadhibiwa wananchi ambao wengine hata walikuwa hawajazaliwa wala kusababisha kwa namna yeyote kuwekwa kwa vikwazo hivyo

CCM kama sehemu ya Vyama vya Ukombozi ktk Bara la Afrika na hasa kwa nafasi yake ya kuwa Chama Kiongozi wakati wote wa mapambano ya kulikomboa Bara la Afrika Kisiasa na sasa mapambano yanayoendelea ya kuikomboa Afrika na Tanzania Kiuchumi

CCM inatumia nafasi hii kupaza sauti na kushinikiza mataifa yote ambayo yameiwekea vikwazo Zimbabwe, kuhakikisha yanaondoa vikwazo hivyo bila masharti yoyote ili nchi hiyo iweze kupiga hatua za haraka za Kimaendeleo, Kiuchumi na Kijamii kwa watu wake

Tunatambua na kupongeza Serikali za Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) chini ya Uenyekiti wa Rais Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania kwa kutoa kauli moja kulaani vikwazo dhidi ya Zimbabwe na kutaka vikwazo hivyo kuondolewa maramoja.

Kwa tamko hili tunaweka msisitizo, kupitia kwa Serikali ya Tanzania, Serikali za Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC
na Nchi wanachama wa Jumuiya ya EAC kwamba ufike wakati Umoja wa Afrika uchukue nafasi yake na kusimamia haki za Nchi wanachama.

CCM inatambua juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Zimbabwe ikiwemo kuimarisha demokrasia na uongozi bora pamoja na kujitegemea kiuchumi; lakini kutokana na vikwazo hivyo nchi hiyo inashindwa kupiga hatua za maendeleo kiuchumi na kijamii kwa kasi inayostahili

Ustawi wa watoto, akina mama na vijana ndio ulioathirika vibaya zaidi, hawa wote wanaumizwa na vikwazo ambavyo vinaathiri Taifa lao

Mapinduzi ya Afrika ambayo lengo lake ni Ukombozi kamili wa Mwafrika yanapingana na Siasa za Kimataifa za kinyonyaji, za ukoloni-mamboleo na ubeberu ambazo kwa muda mrefu zimekwapua utajiri wa Afrika na kuutumia utajiri huo kwa maslahi ya Nchi zao badala ya kuwanufaisha waafrika

Kwa kuzingatia ukweli huo, kushiriki katika Mapinduzi ya Afrika na kushiriki katika ukombozi uliobaki, ukombozi wa kiuchumi ni jambo la msingi kwa Chama chetu

CCM kinaamini na kutambua kwamba Watanzania tunathamini sana uhuru wa Taifa letu, maana hapo ndipo ulipoanzia ukombozi wa wananchi wengi wa Afrika. Kwasababu hii tuna wajibu wa kuchukua hatua zote muhimu zitakazotuwezesha kulinda uhuru wetu

Chama Cha Mapinduzi, Vyama vya Ukombozi vya Kusini mwa Afrika na watu wote wenye mapenzi mema na watu wa Zimbabwe tutaendelea kupaza sauti hadi hapo Jamhuri ya Zimbabwe itakapoondolewa vikwazo hivyo vya kiuchumi
 
Mzee siku hizi kushwinei... hata demekorasia ikibakwa hawezi kukemea... kutokana na misimamo yake huko nyuama... anamaliza uzee vibaya! Tangu alipobanwa na wanamatandao akaenda kulima viazi Njombe... then akarudishwa amekuwa mwepesi kama mabua ya mpunga!
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM BARA ataongea na umma juu ya msimamo wa chama na diplomasia ya kimataifa kutokea Ofisi ndogo za CCM -Lumumba.
Hiki kiswahili cha wapi? "Juu ya msimamo wa chama" huo msimamo UNAHUSU NINI?"
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM BARA ataongea na umma juu ya msimamo wa chama na diplomasia ya kimataifa kutokea Ofisi ndogo za CCM -Lumumba.
Basi sawa mkuu ikiwezekana weka link tu stream live online.
 
Huyu huwa haongeiongei mara kwa mara tutamsikiliza labda ataongea vitu vya maana
Hahaha hawa utapoteza muda wako tu, siku za karibuni Bashiru ndiye kawa msemaji wa chama Polepole kapotea, naye uta mmiss?!
Hawa kuwasikiliza uwaelewe ni mpaka ujitoe akili.
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM BARA ataongea na umma juu ya msimamo wa chama na diplomasia ya kimataifa kutokea Ofisi ndogo za CCM -Lumumba.
Huenda anatakakung'atuka maana hali sio nzuri saana huko
 
Usisahau pia ni chama kinachoongoza kwa WIZI WA KURA.
[emoji124][emoji124][emoji124]
Chama kikongwe barani africa kinacholea demokrasia na kilichopigania na kuzikomboa nchi nyingi barani africa na kuzikwamua kutoka kwenye makucha ya mabeberu!
 
Karibuni Lumumba kwa vichwa vyenye akili sawa
Lumumba FC buku saba hakuna kitu
tapatalk_1570970337110.jpeg
 
Usipende kumtukana mtu bila.sababu huko ni kulekewa vibaya hebu kuwa na heshima
Mzee siku hizi kushwinei... hata demekorasia ikibakwa hawezi kukemea... kutokana na misimamo yake huko nyuama... anamaliza uzee vibaya! Tangu alipobanwa na wanamatandao akaenda kulima viazi Njombe... then akarudishwa amekuwa mwepesi kama mabua ya mpunga!
 
Back
Top Bottom