CCM: Tunayataka mataifa yote duniani yaliyoiwekea vikwazo nchi ya Zimbabwe kuondoa vikwazo hivyo mara moja

CCM: Tunayataka mataifa yote duniani yaliyoiwekea vikwazo nchi ya Zimbabwe kuondoa vikwazo hivyo mara moja

Kwani nchi za africa zimeiwekea Zimbabwe vikwazo ? Ni vikwazo gani wanavyodai viondolewe na mabeberu ? Mpaka sasa vikwazo vilivyobaki ni kwa watu binafsi (individuals) akiwemo raisi Mnangagwa kwa ukiukwaji wao wa haki za binadamu. Kama ni vikwazo vya kibiashara kati ya Zimbabwe na EU wasahau .EU ilikuwa soko kubwa la bidhaa za Zimbabwe kwa vile biashara ile ilifanywa na Wazungu walowezi ila zama hizi ambazo mashamba yote walishawanyang'anya wazungu walowezi biashara na western countries wasahau.
Kama ni wawekezaji wawavutie wachina na warusi wasilazimishe western investors.Mnawaita mabeberu wakati mnanuka shida tupu.
Wazimbabwe wapambane na hali zao, kama biashara wafanye na nchi za Africa na China.
 
Makamu mwenyekiti wa CCM mzee Phillip Mangula amesema CCM inataka kuyaona mataifa yaliyoiwekea Zimbabwe vikwazo yanaviondoa mara moja.

Mzee Mangula amesema ni wakati muafaka sasa nchi za Afrika kuunganisha nguvu ili kupambana na nguvu za mabeberu.

Hivyo CCM inaweka msimamo wa Diplomasia ya kimataifa kuhusu Zimbabwe na inataraji itaungwa mkono na vyama vyote vya kizalendo Afrika.

Source Channel ten mubashara!
Hicho ndio kipaumbele cha ccm? 🤔 we have a long way to go !
 
CCM wekeni kwanza uwanja mzuri wa DEMOKRASIA ndipo mtasikilizwa otherwise mnaweza mkawekewa vikwazo na hao mabeberu na kuwa kama Zimbabwe.
 
CCM wekeni kwanza uwanja mzuri wa DEMOKRASIA ndipo mtasikilizwa otherwise mnaweza mkawekewa vikwazo na hao mabeberu na kuwa kama Zimbabwe.
Uwanja ni mzuri na demokrasia inaanzia kwenye vyama mfano ndani ya Chadema!
 
Mzee wetu Mangura angejitahidi kurekebisha hari yetu ya kisiasa ya Tanzania .Mwalimu Nyerere aliwashauri wazee wenzake wangatuke alijitahidi kuleta mfumo wa demokrasia wa vyama vingi na kuweka mfumo wa kiongozi kutawala vipindi 2 tu.Je mzee Mangura utatuachia nini ukingatuka kabula ujaenda kusaidia Zimbabwe iondolewe vikwazo?
 
EU wenyewe walishakanusha kwamba wamewawekea vikwazo zimbabwe.Tatizo Zimbabwe wanadhani mambo yatakuwa kama enzi zile anafanya biashara na western countries. Biashara na EU zimbabwe asahau atafute namna nyingine ya kujenga uchumi wake..

POSITION OF THE EUROPEAN UNION ON SANCTIONS AGAINST ZIMBABWE

With reference to recent statements made by Zimbabwean officials and underlined by the local press on the occasion of the recent SADC Summit in Dar Es Salaam, according to which the so-called sanctions imposed against Zimbabwe by the EU have accelerated the economic crisis and brought about suffering for the population, the following should be noted:

1) The EU is not imposing economic or trade sanctions against Zimbabwe. The EU shares the opinion expressed by a number of international organisations whereby the main cause of the serious social and economic crisis which Zimbabwe is experiencing should be sought in inappropriate economic policies, the manner in which the land reform has been carried out, the drought and the HIV/AIDS pandemic;

2) the measures adopted by the EU, as a result of the break down of the rule of law and human rights abuses, are the freezing of personal assets of senior members of government and other high-ranking officials, the prevention of the same to travel to EU Member States and the embargo on the sale of arms. None of these measures could affect or cause any hardship to the Zimbabwean population;

3) the suspension or re-orientation of certain financial and development cooperation programmes with the Government of Zimbabwe is mainly due to the fact that it has not complied with the provisions of the pertinent bilateral agreements and to the political and economic environment which is not conducive to development cooperation with government structures;

4) the EU and its Member States are deeply concerned with the economic and humanitarian crisis in Zimbabwe. Consequently, the humanitarian assistance given to the people of Zimbabwe by the EU and its Member States has continued and has, in the last two years, amounted to Euro 300 million (equivalent to approximately USD 330 million). In addition, the EU and member states fund progammes in direct support of the people of Zimbabwe in poverty alleviation, education, health, infrastructures, human rights and democratisation;

5) the EU remains committed to engaging the Government of Zimbabwe in a comprehensive dialogue on the present difficulties being experienced in the country with the aim of restoring political, social and economic stability.
 
Sawa mbabe aka taifa kubwa duniani
Umeskika

Ova
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM BARA ataongea na umma juu ya msimamo wa chama na diplomasia ya kimataifa kutokea Ofisi ndogo za CCM - Lumumba.

UPDATE
Itakumbukwa kwamba Mkutano wa 10 wa Vyama vya Ukombozi vya Kusini mwa Afrika uliofanyika Zimbabwe tarehe9-12 Septemba 2019 uliazimia Vyama kupaza sauti kwa pamoja kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kuondoa mara moja vikwazo dhidi ya Zimbabwe

Kwa kutambua Jukumu letu ktk kuimarisha Umoja, Mshikamano wa Waafrika na kuendeleza mapambano dhidi ya Ukoloni Mamboleo, kupiga vita Ubeberu na Ubaguzi wa aina yoyote pamoja na kuimarisha uhusiano mwema na Vyama vyote vya Siasa vya Nchi nyingine vyenye itikadi kama ya CCM

CCM kinaamini kuwa vikwazo dhidi ya watu wa Zimbabwe ni muendelezo wa fikra na matendo ya uonevu na unyonyaji kwa Waafrika. Watu wa Zimbabwe wameonewa kiasi cha kutosha, na sasa tunaazimia kuwa uonevu huo ufike mwisho

Vikwazo dhidi ya Zimbabwe vimewekwa takribani miaka 19 sasa tangu mwaka 2000. Wanaadhibiwa wananchi ambao wengine hata walikuwa hawajazaliwa wala kusababisha kwa namna yeyote kuwekwa kwa vikwazo hivyo

CCM kama sehemu ya Vyama vya Ukombozi ktk Bara la Afrika na hasa kwa nafasi yake ya kuwa Chama Kiongozi wakati wote wa mapambano ya kulikomboa Bara la Afrika Kisiasa na sasa mapambano yanayoendelea ya kuikomboa Afrika na Tanzania Kiuchumi

CCM inatumia nafasi hii kupaza sauti na kushinikiza mataifa yote ambayo yameiwekea vikwazo Zimbabwe, kuhakikisha yanaondoa vikwazo hivyo bila masharti yoyote ili nchi hiyo iweze kupiga hatua za haraka za Kimaendeleo, Kiuchumi na Kijamii kwa watu wake

Tunatambua na kupongeza Serikali za Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) chini ya Uenyekiti wa Rais Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania kwa kutoa kauli moja kulaani vikwazo dhidi ya Zimbabwe na kutaka vikwazo hivyo kuondolewa maramoja.

Kwa tamko hili tunaweka msisitizo, kupitia kwa Serikali ya Tanzania, Serikali za Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC
na Nchi wanachama wa Jumuiya ya EAC kwamba ufike wakati Umoja wa Afrika uchukue nafasi yake na kusimamia haki za Nchi wanachama.

CCM inatambua juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Zimbabwe ikiwemo kuimarisha demokrasia na uongozi bora pamoja na kujitegemea kiuchumi; lakini kutokana na vikwazo hivyo nchi hiyo inashindwa kupiga hatua za maendeleo kiuchumi na kijamii kwa kasi inayostahili

Ustawi wa watoto, akina mama na vijana ndio ulioathirika vibaya zaidi, hawa wote wanaumizwa na vikwazo ambavyo vinaathiri Taifa lao

Mapinduzi ya Afrika ambayo lengo lake ni Ukombozi kamili wa Mwafrika yanapingana na Siasa za Kimataifa za kinyonyaji, za ukoloni-mamboleo na ubeberu ambazo kwa muda mrefu zimekwapua utajiri wa Afrika na kuutumia utajiri huo kwa maslahi ya Nchi zao badala ya kuwanufaisha waafrika

Kwa kuzingatia ukweli huo, kushiriki katika Mapinduzi ya Afrika na kushiriki katika ukombozi uliobaki, ukombozi wa kiuchumi ni jambo la msingi kwa Chama chetu

CCM kinaamini na kutambua kwamba Watanzania tunathamini sana uhuru wa Taifa letu, maana hapo ndipo ulipoanzia ukombozi wa wananchi wengi wa Afrika. Kwasababu hii tuna wajibu wa kuchukua hatua zote muhimu zitakazotuwezesha kulinda uhuru wetu

Chama Cha Mapinduzi, Vyama vya Ukombozi vya Kusini mwa Afrika na watu wote wenye mapenzi mema na watu wa Zimbabwe tutaendelea kupaza sauti hadi hapo Jamhuri ya Zimbabwe itakapoondolewa vikwazo hivyo vya kiuchumi
Hamna ubavu huo.
 
aliykuwa katibu mkuu wa CCM, na pia aliyewahi kuneemeka na MAREKANI walipokuja kuingia mikataba ya kilaghai hapa Tanzania kwa kufua umeme SYMBION ni pamoja na PHILIP MANGULA lakini kwa sasa amejitoa ufahamu ama uzee umekuja ghafla na kuanza kuwatukana marekani.

huyu mzee watoto wake wamesoma marekani, aa akaunti ya fedha za kigeni huko kama ilivyo kwa viongozi wengine pamoja na baadhi ya makada kama chenge aliyeficha mabilioni yake huko visiwa vya JERSSEY.

MANGULA KAMA ILIVYO KWA JIWE, wamekuwa wakiitukana marekani na kuwaita "mabeberu" huku maekani wenyewe wakikaa kimya kwa kuwatazama kama watoto wadogo wasio jielewa.

URUSI, IRAQ, LIBYA, walianza hivi hivi, kilichowakuta sihitaji kusema .

CCM Yatoa Tamko Kulaani Vikavyo Vya Uchumi ilivyowekewa Zimbabwe*

*KOMBORA*

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM – Taifa), Philip Mangula ametoa tamko la azimio la chama hicho juu ya vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa Zimbabwe tangu mwaka 2000.

Mangula ametoa tamko hilo leo Jumatano Oktoba 24, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salam ambapo amesema kuwa vikwazo hivyo ni mwendelezo wa fikra na matendo ya unyojaji kwa Afrika na hivyo wameazimia kuwa uonevu huo ufike mwisho.

“Kwa kutambua jukumu letu katika kuimarisha umoja, ushikamano wa Waafrika na kuendeleza mapambano dhidi ya ukoloni mamboleo pamoja na kuimarisha uhusiano mwema wa vyama vya siasa vya nchi nyingine vyenye itikadi kama ya CCM, chama kinaamini kuwa vikwazo dhidi ya watu wa Zimbabwe ni muenedelezo wa fikra na matendo ya unyojaji kwa Afrika na sasa tuaazimia kuwa uonevu huo ufike mwisho,”.

“Ni miaka 19 ya kuwekewa vikwazo hata wale ambao walikuwa hawajazaliwa wanaadhibiwa na vikwazo hivi nadhani huu sio ubinadamu, sambamba na kutekeleza maamuzi hayo CCM kwa nafasi yake ya kuwa chama kiongozi wakati wote wa kulikomboa Bara la Afrika kisiasa inatumia nafasi hii kupaza sauti na kushinikiza mataifa yote yaliyoiwekea vikwazo Zimbabwe kuviondoa bila masharti yoyote ili nchi hiyo iweze kupiga hatua za haraka za maendeleo kiuchumi na kijamii kwa watu wake,” amesema Mangula.

Aidha Mangula amevitaka Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika na watu wote wenye mapenzi mema kuendelea kupaza sauti hadi pale Zimbabwe itakapoondolewa vikwazo hivyo vya kiuchumi ambavyo havizingatii ubinadamu.

*KOMBORA*
 
Hivi shida za Zimbabwe zinatuhusu Nini? Gunia la mahindi limefika laki kisa Zimbabwe, mkichuma janga hamli nasisi ngo, mtakula wenyewe Hadi mvimbewe
 
Hao jamaa wana mioyo ya pekee ingekuwa ni sie waafrika tusingesitisha kuwasaidia kwa roho zetu mbaya.Unamuita MTU anaesaidia bajeti yako beberu hali kila kitu unategemea toka kwake.
 
Kama wanawezaendelea bila mabeberu vikwazo vinawazuia vipi kuendelea
 
Back
Top Bottom