Ukiona mtu anataka kusiwepo na adhabu dhidi ya wezi, basi mtu huyo huenda ni mwizi lakini hajajulikana, au ndugu zake ni wezi, au anataka kuanza kuiba au ni mnufaika wa wizi unaofanyika.
CCM, hata siku moja haiwezi kupinga ukiukaji wa haki za binadamu au uvurugaji wa misingi ya demokrasia au matumizi mabaya ya vyombo vya dola, kwa sababu na yenyewe ipo kwa sababu ya kuoshi kwenye huo ukiukaji.
Watawala wa Zimbabwe wazidi kubanwa mpaka pale watakapoweza kuheshimu haki na uhuru wa watu wao. Watawala wa Zimbabwe wamejifungamanisha na jeshi la Zimba qe na kulifanya kama kamati ya chama ili wawagandamize wanaotofautiana nao. Nimefika Zimbabwe, nimeishi na Wazimbabwe - wananchi wengi hawawaungi mkono watawala na chama chao tawala.
Kwa msimamo huo wa Mangula, CCM imejiunga na watawala dhalimu wa Zimbabwe dhidi ya wananchi wa Zimbabwe ambao wamelazimishwa kuishi kwenye mateso makali. Chama cha siasa kilicho makini husimama na umma na siyo na kakikundi dhalimu ka watu wachache.