Hicho ndio kipaumbele cha ccm? 🤔 we have a long way to go !Makamu mwenyekiti wa CCM mzee Phillip Mangula amesema CCM inataka kuyaona mataifa yaliyoiwekea Zimbabwe vikwazo yanaviondoa mara moja.
Mzee Mangula amesema ni wakati muafaka sasa nchi za Afrika kuunganisha nguvu ili kupambana na nguvu za mabeberu.
Hivyo CCM inaweka msimamo wa Diplomasia ya kimataifa kuhusu Zimbabwe na inataraji itaungwa mkono na vyama vyote vya kizalendo Afrika.
Source Channel ten mubashara!
CCM iko kitaifa na kimataifa tofauti na akina Chadema wa upepo wa kisulisuli!Hicho ndio kipaumbele cha ccm? 🤔 we have a long way to go !
Uwanja ni mzuri na demokrasia inaanzia kwenye vyama mfano ndani ya Chadema!CCM wekeni kwanza uwanja mzuri wa DEMOKRASIA ndipo mtasikilizwa otherwise mnaweza mkawekewa vikwazo na hao mabeberu na kuwa kama Zimbabwe.
Mambo ya 1960s unayaleta kwenye 2010's ? Wont work!Ndiyo, uzoefu tunao..tulishaongoza leberation struggle since 60s..nashauri pia serikali ya CCM ichukue hii kama foreign policy..
Namuona Nyerere akiweka tabasam usoni
Hamna ubavu huo.Makamu Mwenyekiti wa CCM BARA ataongea na umma juu ya msimamo wa chama na diplomasia ya kimataifa kutokea Ofisi ndogo za CCM - Lumumba.
UPDATE
Itakumbukwa kwamba Mkutano wa 10 wa Vyama vya Ukombozi vya Kusini mwa Afrika uliofanyika Zimbabwe tarehe9-12 Septemba 2019 uliazimia Vyama kupaza sauti kwa pamoja kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kuondoa mara moja vikwazo dhidi ya Zimbabwe
Kwa kutambua Jukumu letu ktk kuimarisha Umoja, Mshikamano wa Waafrika na kuendeleza mapambano dhidi ya Ukoloni Mamboleo, kupiga vita Ubeberu na Ubaguzi wa aina yoyote pamoja na kuimarisha uhusiano mwema na Vyama vyote vya Siasa vya Nchi nyingine vyenye itikadi kama ya CCM
CCM kinaamini kuwa vikwazo dhidi ya watu wa Zimbabwe ni muendelezo wa fikra na matendo ya uonevu na unyonyaji kwa Waafrika. Watu wa Zimbabwe wameonewa kiasi cha kutosha, na sasa tunaazimia kuwa uonevu huo ufike mwisho
Vikwazo dhidi ya Zimbabwe vimewekwa takribani miaka 19 sasa tangu mwaka 2000. Wanaadhibiwa wananchi ambao wengine hata walikuwa hawajazaliwa wala kusababisha kwa namna yeyote kuwekwa kwa vikwazo hivyo
CCM kama sehemu ya Vyama vya Ukombozi ktk Bara la Afrika na hasa kwa nafasi yake ya kuwa Chama Kiongozi wakati wote wa mapambano ya kulikomboa Bara la Afrika Kisiasa na sasa mapambano yanayoendelea ya kuikomboa Afrika na Tanzania Kiuchumi
CCM inatumia nafasi hii kupaza sauti na kushinikiza mataifa yote ambayo yameiwekea vikwazo Zimbabwe, kuhakikisha yanaondoa vikwazo hivyo bila masharti yoyote ili nchi hiyo iweze kupiga hatua za haraka za Kimaendeleo, Kiuchumi na Kijamii kwa watu wake
Tunatambua na kupongeza Serikali za Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) chini ya Uenyekiti wa Rais Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania kwa kutoa kauli moja kulaani vikwazo dhidi ya Zimbabwe na kutaka vikwazo hivyo kuondolewa maramoja.
Kwa tamko hili tunaweka msisitizo, kupitia kwa Serikali ya Tanzania, Serikali za Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC
na Nchi wanachama wa Jumuiya ya EAC kwamba ufike wakati Umoja wa Afrika uchukue nafasi yake na kusimamia haki za Nchi wanachama.
CCM inatambua juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Zimbabwe ikiwemo kuimarisha demokrasia na uongozi bora pamoja na kujitegemea kiuchumi; lakini kutokana na vikwazo hivyo nchi hiyo inashindwa kupiga hatua za maendeleo kiuchumi na kijamii kwa kasi inayostahili
Ustawi wa watoto, akina mama na vijana ndio ulioathirika vibaya zaidi, hawa wote wanaumizwa na vikwazo ambavyo vinaathiri Taifa lao
Mapinduzi ya Afrika ambayo lengo lake ni Ukombozi kamili wa Mwafrika yanapingana na Siasa za Kimataifa za kinyonyaji, za ukoloni-mamboleo na ubeberu ambazo kwa muda mrefu zimekwapua utajiri wa Afrika na kuutumia utajiri huo kwa maslahi ya Nchi zao badala ya kuwanufaisha waafrika
Kwa kuzingatia ukweli huo, kushiriki katika Mapinduzi ya Afrika na kushiriki katika ukombozi uliobaki, ukombozi wa kiuchumi ni jambo la msingi kwa Chama chetu
CCM kinaamini na kutambua kwamba Watanzania tunathamini sana uhuru wa Taifa letu, maana hapo ndipo ulipoanzia ukombozi wa wananchi wengi wa Afrika. Kwasababu hii tuna wajibu wa kuchukua hatua zote muhimu zitakazotuwezesha kulinda uhuru wetu
Chama Cha Mapinduzi, Vyama vya Ukombozi vya Kusini mwa Afrika na watu wote wenye mapenzi mema na watu wa Zimbabwe tutaendelea kupaza sauti hadi hapo Jamhuri ya Zimbabwe itakapoondolewa vikwazo hivyo vya kiuchumi
Hao jamaa wana mioyo ya pekee ingekuwa ni sie waafrika tusingesitisha kuwasaidia kwa roho zetu mbaya.Unamuita MTU anaesaidia bajeti yako beberu hali kila kitu unategemea toka kwake.aliykuwa katibu mkuu wa CCM, na pia aliyewahi kuneemeka na MAREKANI walipokuja kuingia mikataba ya kilaghai hapa Tanzania kwa kufua umeme SYMBION ni pamoja na PHILIP MANGULA lakini kwa sasa amejitoa ufahamu ama uzee umekuja ghafla na kuanza kuwatukana marekani.
huyu mzee watoto wake wamesoma marekani, aa akaunti ya fedha za kigeni huko kama ilivyo kwa viongozi wengine pamoja na baadhi ya makada kama chenge aliyeficha mabilioni yake huko visiwa vya JERSSEY.
MANGULA KAMA ILIVYO KWA JIWE, wamekuwa wakiitukana marekani na kuwaita "mabeberu" huku maekani wenyewe wakikaa kimya kwa kuwatazama kama watoto wadogo wasio jielewa.
URUSI, IRAQ, LIBYA, walianza hivi hivi, kilichowakuta sihitaji kusema .
CCM Yatoa Tamko Kulaani Vikavyo Vya Uchumi ilivyowekewa Zimbabwe*
*KOMBORA*
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM – Taifa), Philip Mangula ametoa tamko la azimio la chama hicho juu ya vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa Zimbabwe tangu mwaka 2000.
Mangula ametoa tamko hilo leo Jumatano Oktoba 24, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salam ambapo amesema kuwa vikwazo hivyo ni mwendelezo wa fikra na matendo ya unyojaji kwa Afrika na hivyo wameazimia kuwa uonevu huo ufike mwisho.
“Kwa kutambua jukumu letu katika kuimarisha umoja, ushikamano wa Waafrika na kuendeleza mapambano dhidi ya ukoloni mamboleo pamoja na kuimarisha uhusiano mwema wa vyama vya siasa vya nchi nyingine vyenye itikadi kama ya CCM, chama kinaamini kuwa vikwazo dhidi ya watu wa Zimbabwe ni muenedelezo wa fikra na matendo ya unyojaji kwa Afrika na sasa tuaazimia kuwa uonevu huo ufike mwisho,”.
“Ni miaka 19 ya kuwekewa vikwazo hata wale ambao walikuwa hawajazaliwa wanaadhibiwa na vikwazo hivi nadhani huu sio ubinadamu, sambamba na kutekeleza maamuzi hayo CCM kwa nafasi yake ya kuwa chama kiongozi wakati wote wa kulikomboa Bara la Afrika kisiasa inatumia nafasi hii kupaza sauti na kushinikiza mataifa yote yaliyoiwekea vikwazo Zimbabwe kuviondoa bila masharti yoyote ili nchi hiyo iweze kupiga hatua za haraka za maendeleo kiuchumi na kijamii kwa watu wake,” amesema Mangula.
Aidha Mangula amevitaka Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika na watu wote wenye mapenzi mema kuendelea kupaza sauti hadi pale Zimbabwe itakapoondolewa vikwazo hivyo vya kiuchumi ambavyo havizingatii ubinadamu.
*KOMBORA*