Uchaguzi 2020 CCM Vijijini Tundu Lissu ametikisa ngome ni muda wa CCM kubadili itikadi na mikakati

Mkutano wa Tundu Lissu huko Tunduru leo umenifanya nibadili taswira ya chama chetu ccm kuwa lazima sasa tubadilishe mfumo mzima wa itikadi na mawazo juu ya wananchi wa vijijini.
24 October 2020
Tunduru, Tanzania

LIVE # TUNDU LISSU ASEPA NA WAKAZI WA TUNDURU MAELFU WAJA KUMLAKI

 
Msamehe tu huyo kichwani hamna kitu kabisa na hajielewi ,ana miaka 34 lakini Bado analala sebureni kwa dada yake huyo ni mzigo kwa familia na nchi pia
 
Msaliti wa Nchi Lissu anasimama stend na sokoni
Hakuna mtu atapoteza muda kwenda kusikiliza matusi
Mkuu kwa hoja hii dhaifu nimeona ni busara zaidi nikae kimya.Lissu anaenda sokoni na stendi?Hivi mikutano na viwanja vya kufanyia mikutano so vinawekwa kwenye ratiba na NEC?Au NEC ndo wanampangia sokoni na stendi?
 
Mkuu kwa hoja hii dhaifu nimeona ni busara zaidi nikae kimya.Lissu anaenda sokoni na stendi?Hivi mikutano na viwanja vya kufanyia mikutano so vinawekwa kwenye ratiba na NEC?Au NEC ndo wanampangia sokoni na stendi?
 
Tunduru hii sio ya miaka ya 90,useme ni kijijini.. ni moja ya wilaya kongwe. Imepiga hatua sana.
 
Kwa ubabe 90% tumezibwa midomo..Lissu pekee ndie anaweza kuongea ukweli nchi hii..Na walidhani kwa kukandamiza Wangeshinda 100% ..Kumbe nchi c ya mmoja..28-10 nnajambo langu privatini
 
Unamaanisha huyu ndo awe rais wa JMT!!?? over my dead body.
 
Mleta mada umeandika vitu vya msingi sana, jambo moja pekee ninaloweza kukukosoa ni kuhusu namna ya kuirekebisha CCM.

CCM imeshafika kilele cha juu kabisa cha ulevi wa madaraka (ni level ya umateja) inaamini inaweza kufanya jambo lolote na hakuna mtu yoyote duniani mwenye uwezo wa kuwazuia. Kiwango hicho cha ulevi wa madaraka huwezi kukirekebisha kwa njia ya kukishauri au kukionya, njia pekee ni kukiadhibu vikali. Na adhabu pekee ni kukitoa kwanza madarakani, kipumzike (kiende soba) huko ndio kinaweza kujirekebisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…