CCM waanza mchakato wa kumshughulikia Luhanga Mpina, awasili mbele ya kamati ya maadili CCM

CCM waanza mchakato wa kumshughulikia Luhanga Mpina, awasili mbele ya kamati ya maadili CCM

Kwangu Mpina ndiye aliyekuwa mtu sahihi wa kuchukua fomu! Ni chapa ya Mwendazake!
Lakini ili asijimalize kabisa kisiasa ni vizuri aombe radhi abakie CCM! Asithubutu kwenda chama kingine, ajifunze kwa waliofanya hivyo wako wapi?
Huwezi ukapambana na CCM ukaweza! Iwe ndani au nje!
Nchi ni ya CCM, Vyombo vya Ulinzi na Usalama ni vya CCM, Serikali na taasisi zake ni za CCM!
Ataenda wapi? Atafanya nini?
Mawazo ya kipuuzi kama haya yako ndiyo yanaifanya CCM iendelee kubaki madarakani na kutafuna rasilimali za taifa. Ni lini watanzania mtaamka kutoka usingizini?
 
Mpina huyu huyu aliyechoma vifaranga na kupima samaki waliopikwa?
Kulanina zake.[emoji20]
Mkuu nakuomba urejee kwenye mada. Hapa hatuongei juu ya samaki na vifaranga bali tunaongea juu ya CCM kumfukuza Mpina kwa sababu ya kuetetea rasilimali za taifa.
 
Mkuu nakuomba urejee kwenye mada. Hapa hatuongei juu ya samaki na vifaranga bali tunaongea juu ya CCM kumfukuza Mpina kwa sababu ya kuetetea rasilimali za taifa.
Hakuna mtetezi hapo ni "sizitaki mbichi hizi" tu.
 
Ukiwa mtu wa haki hutakiwi ndani ya CCM
Inashangaza sana. Siku zote huwa najiuliza kwanini CCM hawawapendi watu wanaotetea rasimali za taifa na ustawi wa wananchi sipati jibu. Mtu yeyote akiwa mtetezi wa haki, huhusishwa na CHADEMA. Hivi huko CCM hakuna watu wenye uchungu na rasilimali za umma? Wao wapo tu kutetea matumbo yao binafsi bila kujali maendeleo ya wanachi? CCM ni majitu ya ovyo sana aisee!
 
Hakuna mtetezi hapo ni "sizitaki mbichi hizi" tu.
Kwa hiyo wewe unapenda kuona rasilimali za taifa zikitafunwa na mafisadi, machawa na makunguni wachache huku wananchi walio wengi wakiteseka na ugumu wa maisha?
 
Inashangaza sana. Siku zote huwa najiuliza kwanini CCM hawawapendi watu wanaotetea rasimali za taifa na ustawi wa wananchi? Mtu yeyote akiwa mtetezi wa haki, huhusishwa na CHADEMA. Hivi huko CCM hakuna watu wenye uchungu na rasilimali za umma? Wao wapo tu kutetea matumbo yao binafsi bila kujali maendeleo ya wanachi? CCM ni majitu ya ovyo sana aisee!
Kuwa CCM lazima uwe kati ya wauza unga, mirungi, tapeli, mwizi, jangili, mshirikina, muongo, mvivu au jambazi.
 
Huna lolote wewe.unawashwa na mambo usiyoyajua.unaokoteza stori za vijiweni unakuja kuropokea uku.Usifikiri watu wote ni wajinga.mbowe atatoka muda ukifika sio kwasababu ya nyie kunguni mnaosumbuliwa na chuki.
Wewe kondoo huna akili hujui kitu!! Hawezi kutoka kwasababu analında Saccos ya mkwewe! Uko ndoo wako ndio umekupofusha! Huoni wala husikii.
 
Mpina Kama uko jf. Ukiitwa kwenye hicho kikao Cha michongo epuka kula zile refreshments na kunywa maji, hata ikibidi usitumie Mike.
 
Kuwa CCM lazima uwe kati ya wauza unga, mirungi, tapeli, mwizi, jangili, mshirikina, muongo, mvivu au jambazi.
Kweli kabisa mkuu. CCM ni ukoo wa panya—babu mwizi, baba mwizi, watoto wezi, wajukuu wezi, vitukuu wezi, vilembwe wezi na vining’ina wezi! Ukoo huu wa panya walikuwa wanasafiri katika boti la muhogo, lakini kwa sababu ya uroho wao, walianza kulitafuna boti! Kilichofuata ni ukoo mzima wa kizazi cha panya kuzama na kuangamia.

CCM wameanza kuitafuna nchi tangu mwaka 1961 lakini ukomo wao wa kutafuna rasilimali za nchi zitafika tamati hivi punde kwani hakuna mtanzania mwenye hamu ya kuongozwa na chama cha kifisadi kama CCM ambacho kimeshindwa kuboresha maisha na ustawi wa watanzania. Wananchi wamechoka kubebeshwa ‘magunia ya misumari’ ya bei ya juu ya chakula, mfumuko wa bei wa kutisha, elimu duni, maisha duni, ufisadi wa kutisha na matatizo lukuki yanayosababishwa na panya (CCM) hawa wasiokuwa na haya! Kizazi kizima cha CCM kinakaribia kuzama na kusahaulika kabisa katika ardhi ya Tanzania.

It’s a matter of time before CCM dynasty comes to an end, and that’s when these unscrupulous rats will apprehend the significance and power of the people. Desolately, CCM have been ignoring and looking down their noses at common Tanzanians for many years. Time has now come when citizens can no longer endure CCM’s tyranny and corrupt rule. Everybody is tired of living like a slave on a land endowed with an assortment of natural wealth which only benefits minority looters and a few elites in power while majority Tanzanians lead very miserable lives.

What comes around goes around. Let CCM go to hell for good because they have absolutely failed to uplift the living standards of millions of Tanzanians at the expense of a few looters whose gargantuan stomachs never fill up! And no one should be blamed for the hatred and grudge that majority people hold against CCM and their crooked government except looters themselves who, horrifically, decided to gnaw the cassava boat by which they were sailing!
 
Wewe kondoo huna akili hujui kitu!! Hawezi kutoka kwasababu analında Saccos ya mkwewe! Uko ndoo wako ndio umekupofusha! Huoni wala husikii.
Mkuu hivi kwanini unapenda kumchokoza Moderator kwa kutoa lugha za matusi? Akikikupiga ban utasema kakuonea?

Hapa tunazungumza juu ya kufukuzwa kwa Mpina. Naomba ujikite kwenye mada husika usituletee mada mpya ambayo haihusiani na mada iliyo hewani.
 
Mpina Kama uko jf. Ukiitwa kwenye hicho kikao Cha michongo epuka kula zile refreshments na kunywa maji, hata ikibidi usitumie Mike.
Aige mtindo wa Gwajima alivyoitwa na kamati ya bunge!!
 
Mkuu are you serious? Ufisadi wa trilion 2 aliofanya Mwigulu kwenye SGR na uuzaji wa nchi kwa waarabu wa DP World ni mambo ya kufikirika? Kuwa serious walau kidogo basi. Mbona watu mnakosa uchungu na rasilimali za taifa kiasi hiki?
Trillion mbili maana yake Mwigulu ni dollar billionaire kwa hela hiyo anaingia kwenye exclusive club ya watu 3000 plus pekee duniani wenye kufikia iko kiwango cha hela na kuvuka.

Ndio atukatai Mwigulu ni lijizi kama wezi wengine huko serikalini ila hela hiyo hana. Sanasana anachoweza fanya apendelee tender apate hongo, lakini akwapue dollar billion moja bila ya madhara uwezo huo hata huyo ‘bi tozo’ hana.

Comparison zake Mpina za kuongezeka kwa gharama za mradi wa SGR per/km uliacha factors nyingi sana kama material inflation, exchange rate, operation costs na mambo kadha wa kadha. Kila akielimishwa huko bungeni aelewi somo yeye hataki kubadili msimamo na hoja zake which lack economic justifications.

DP World mimi na wewe hatujui kama tuna mkataba mzuri au la; tumeshaelezwa sana maswala ya ‘consideration’ ya kwenye mkataba (value of exchange) yatajadiliwa huko kwenye ‘concession agreement’ na makubaliano hayo hatujaona.

Otherwise IGA ni framework tu na ime cover sana kwenye maswala ya ‘stabilisation clauses’ ni muhimu kwenye kulinda uwekezaji na ni mambo ya kawaida sana kwenye international business law.

Mmeelimishwa na serikali amtaki kuelewa mnataka kuamini interpretation za Nshala, Madeleka, Mwabukusi na Twitter republic opinion, sasa serikali ifanye nini tena. Iachane na uwekezaji wenye tija kisa wananchi wameamua kuamini nadharia potofu.
 
Mpina Kama uko jf. Ukiitwa kwenye hicho kikao Cha michongo epuka kula zile refreshments na kunywa maji, hata ikibidi usitumie Mike.
Kweli kabisa mkuu. Hawa wauaji walikaribia kuwatoa roho Mwakyembe, Zitto na Samuel Sitta.
 
Mkuu hivi kwanini unapenda kumchokoza Moderator kwa kutoa lugha za matusi? Akikikupiga ban utasema kakuonea?

Hapa tunazungumza juu ya kufukuzwa kwa Mpina. Naomba ujikite kwenye mada husika usituletee mada mpya ambayo haihusiani na mada iliyo hewani.
Unless wewe mwenyewe ni moderatör!! Siku hizi kuna options nyingi za kufikisha ujumbe! Au hujui mambo ya AI? Pole
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, habari kutoka ndani ya CCM zinabainisha kuwa CCM wameishaanza mchakato wa kumfukuza uanachama mbunge wa Kisesa, ndugu Luhanga Mpina.

View attachment 2882194

Inasemekana kabla mama hajasafiri kwenda Indonesia alitoa maagizo kwamba akirudi asikumkute Mpina bado akiwa ndani ya CCM. Sababu za kufukuzwa ndugu Mpina hazijawekwa wazi lakini kwa siku za hivi karibuni Mpina amekuwa mwiba mkali kwa mafisadi na chawa wanaofisadi na kuuza rasilimali za taifa kwa wageni huku wananchi wakiendelea kutopea kwenye umaskini na huduma mbovu za jamii.

Habari zaidi zinasema kabla ya kufukuzwa ndugu Mpina atapewa nafasi ya kujitetea mbele ya kamati maalumu ya CCM iliyoteuliwa na Rais kushughulikia suala hili ambalo wao wameliita "tatizo la kinidhamu ndani ya chama". Haikuweza kufahamika mara moja kamati hiyo inaundwa na akina nani lakini chanzo kingine kutoka CCM kinadai katika kamati hiyo wamo Kinana, Makonda, Yusufu Makamba na wazee wengine mashuhuri wa CCM.

MAONI YANGU
Kufukuzwa kwa Mpina kutoka CCM kulikuwa dhahiri tangu alipoanza kuwavalia njuga mafisadi, wauza nchi na chawa wanaotafuna rasilimali za nchi bila kuhojiwa. Hili lilikolezwa na msimamo wake dhabiti wa kupinga uuzaji wa bandari kwa waarabu wa DP World.

Jambo ambalo mpaka sasa haliko dhahiri ni kwamba je akifukuzwa CCM atahamia chama gani? Possibly itakuwa CHADEMA kwa sababu baadhi ya wazalendo na wana intelejensia wanadai kuwa Mpina ni kada wa CHADEMA aliyetumwa kuingia ndani ya CCM kimkakati ili kukipeleleza chama hicho.

Lakini mpaka sasa hakuna mwenye uhakika 100% kuhusu chama ambacho mpina atatimkia ili kimteue kugombea kwenye uchaguzi mkuu 2025 pindi akitupiwa virago na CCM. Huenda hata akuibukia ACT-Wazalendo. You never know but time will tell. Let us wait until the end of the movie.

Pia soma:
1.
Tetesi: - Wabunge washauri Luhaga Mpina afukuzwe CCM

2.
Tetesi: - Karibu CHADEMA Luhaga Mpina, Kazi tulikutuma CCM umeitendea haki.
Kwani Chadema Wana sera za kupima samaki kwa rula? Halafu je, CHADEMA Wana sera za kuchoma moto nyavu za wavuvi?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Possibly itakuwa CHADEMA kwa sababu baadhi ya wazalendo na wana intelejensia wanadai kuwa Mpina ni kada wa CHADEMA aliyetumwa kuingia ndani ya CCM kimkakati ili kukipeleleza chama hicho.
Asiende CDM aanzishe chama chake aungane na smart boy Mbatia
 
Back
Top Bottom