CCM wanachekesha Sana, wanakwenda kuchagua bila kujua watamchagua nani!

CCM wanachekesha Sana, wanakwenda kuchagua bila kujua watamchagua nani!

Mama kawema majina yake kwenye sidiria.
Na hivi kajaliwa kifua kikubwa basi loh 😂😂
Sio yeye wajumbe wote wa kamati kuu na halmashauri kuu huwa na kifua cha majina husika hadi yafike mkutano mkuu
 
Chadema wanatufundisha sana namna ya siasa ya nchi hii zinapaswa kuwa.
Kabisa, kama kuna kitu cdm wamepatia ni huu mnyukano wa wazi wa kisiasa. Hivyo ndio ushindani wa kisiasa unapaswa kuwa. Sio watu wanaficha mambo halafu anayechaguliwa unakuta hata wajumbe hawajui amechaguliwa kwa sifa gani? Yaani ccm bado wanafanya siasa za kizamani mno.
 
Kwa siku mbili kati ya tarehe 18,19/01/2025, CCM itakuwa na mkutano wake maalum huko Dodoma.

Kwenye mkutano huo, pamoja na mambo mengine, wajumbe watapiga kura ya kumthibitisha (siyo kumchagua ) Makamo Mwenyekiti wa chama hicho kwa upande wa Tanganyika.

Leo siku tatu kabla ya mkutano huo kuanza, wajumbe hawajui ni nani wanayekwenda kumthibitisha awe Makamo Mwenyekiti wao kwa upande wa Tanganyika.

Katiba ya CCM inasema kuwa, Makamo wa Mwenyekiti atapendekezwa na Kamati Kuu kwa Halmashauri Kuu ya chama hicho ambayo ndiyo itapendekeza Kwa mkutano Mkuu, jina la anayetakiwa awe Makamo Mwenyekiti kwa ajili ya kuthibitishwa.

Sasa hao wajumbe mpaka Leo hawajui nani atakuwa Makamo wa Mwenyekiti wao, halafu CCM inajisifu kuwa yenyewe ni chama kikubwa.

Chama gani kikubwa kinachoendesha mambo kizamani sana kama jando au unyago?

Machawa wanangejea waletewe kiongozi wasiyemjua wala kumchagua, waanze kumpamba.

CC.

Machawa wote.
Inaweza ikawa mbinu nzuri ya kuepusha mtu kujitafutia kura za uongo
 
CCM: Kituko cha Karne kwenye Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti

Katika mazingira ya kisiasa ya Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimejipatia umaarufu mkubwa, lakini pia kimekuwa na changamoto nyingi.

Hivi karibuni, chama hicho kimejipanga kufanya mkutano mkuu wa uchaguzi wa makamu mwenyekiti wa taifa. Kinachoshangaza ni kwamba, licha ya umuhimu wa nafasi hiyo, hakuna aliyejaza fomu au kuomba rasmi nafasi hiyo.

Kwa hakika, hali hii inatoa taswira ya kituko ambacho hakijawahi kushuhudiwa katika historia ya siasa za Tanzania.

Muktadha wa Uchaguzi

Mkutano huu mkuu unakuja wakati ambapo CCM inakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na kudhoofika kwa uaminifu wa umma na mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea.

Hali hii inaongeza uzito wa uchaguzi wa makamu mwenyekiti, kwani mtu atakayechaguliwa atakuwa na jukumu muhimu katika kuongoza na kuimarisha chama katika kipindi hiki kigumu.

Kichwa cha Ndani na Kukosekana kwa Wagombea

Kinachoshangaza ni jinsi CCM inavyoenda kwenye uchaguzi huu bila wagombea rasmi. Hii ni hali isiyo ya kawaida, kwani katika vyama vingi vya siasa, wagombea hujaza fomu na kufanya kampeni ili kujipatia uungwaji mkono. Lakini hapa, inavyoonekana, kuna mpango wa kuchagua mtu bila hata kujua ni nani atakayekuwa na nafasi hiyo.

Je, hii ni dalili ya kukosekana kwa viongozi wenye uwezo, au ni mkakati wa kisiasa wa ndani wa chama?

Kituko au Mkakati?

Wengi wanaweza kuona hali hii kama kituko cha karne, lakini kuna wale wanaodai kuwa huenda ni mkakati wa kisiasa.

Chama kinaweza kuwa na mtu maalum ambaye tayari amekwishakubaliwa kwa makubaliano ya ndani, na hivyo hawahitajii mchakato wa kawaida wa uchaguzi.

Hii inaweza kuashiria udhaifu katika demokrasia ndani ya chama, ambapo maamuzi makubwa yanachukuliwa bila ushirikishwaji wa wanachama.

Athari za Kukosekana kwa Ushindani

Uchaguzi huu wa makamu mwenyekiti unatoa nafasi muhimu kwa viongozi wapya kujitokeza na kuonyesha uwezo wao. Kukosekana kwa ushindani kunaweza kukatisha tamaa wanachama ambao wangependa kuona mchakato wa wazi na wa haki. Aidha, hali hii inaweza kuathiri sana uaminifu wa umma kwa CCM, kwani watu wanaweza kuanza kuhoji uhalali wa uchaguzi na maamuzi yanayofanywa na viongozi wao.

Mwelekeo wa CCM Katika Siasa za Baadaye

Ikiwa CCM itaendelea na mtindo huu wa uchaguzi, inakabiliwa na hatari ya kupoteza uungwaji mkono wa wananchi. Katika nyakati za sasa ambapo wananchi wanahitaji uwazi na uwajibikaji zaidi kutoka kwa viongozi wao, hali hii inaweza kuleta madhara makubwa. Ni muhimu kwa chama hicho kufikiria upya kuhusu njia zao za uchaguzi na kuhakikisha kuwa wanachama wanahusishwa kikamilifu katika mchakato wa kuchagua viongozi.

Hitimisho

Kwa hivyo, mkutano huu wa CCM ni kituko cha karne, lakini pia ni kengele ya kuamsha dhamira ya mabadiliko ndani ya chama.

Ni wakati wa CCM kufungua milango kwa wagombea wengi na kuhakikisha kuwa mchakato wa uchaguzi unakuwa wa haki na wa uwazi.

Vinginevyo, chama hicho kinaweza kujikuta katika changamoto kubwa ya kuimarisha uhusiano wake na umma. Wakati huu wa kihistoria unahitaji maamuzi ya busara na kuzingatia maslahi ya wanachama na taifa kwa ujumla.
 
Siyo kweli. Mwenyekiti ndiye hupendekeza jina la anayetaka awe Makamo mwenyekiti.

One person show party.
Ndio hateui anapendekeza kamati kuu ndio huidhinisha na halmashauri kuu na mkutano mkuu

Lazima liende vikao kuidhinishwa au kukataliwa sio akisema tu yeye basi soma katiba ya CCM wewe mbona sisi CCM tunaijua katiba ya Chadema haina ukomo wa Mwenyekiti aweza kugombea halafu nyie ukiwemo wewe hamjui.hata katiba yenu ohh mbowe asigombee tena miaka aliyoongoza ohh inatosha .Hata katiba yenu tu hamjui mnatia huruma.Mbowe ruksa kugombea kwa mujibu w katiba ya Chadema

Ya kwenu katiba yenu inawashinda kuelewa ndio mtayawweza ya katiba ya CCM?
 
Wewe ndiyo mpendekezaji wa hilo jina? Najua unasuburi atajwe uanze kumpamba.

Huu ni udhaifu mkubwa sana kwa CCM. Yaani maelfu ya watu wanakwenda Dodoma kigiza giza bila kuelezwa wanakwenda kumthibitisha nani?

Hata hao Kamati Kuu wenyewe hawajui ni nani atakuwa Makamo Mwenyekiti wao. Sasa wapo kwenye chama kwa kazi gani?
Yaani ni kitu cha ajabu sana kwa watu wazima na wenye (kama wanazo) akili timamu kusafiri pasi kujua unaenda kumchagua nani!!!!

Na kwa nini wasigombee!!??

Kweli kama alivyowahi kusema marehemu Prof. C. S. Chachage kuwa uoga na kutojiamini ndio kunakopelekea mtu mmoja kuwa amiri jeshi mkuu na mwenyekiti wa chama twawala.
 
Kweli kama alivyowahi kusema marehemu Prof. C. S. Chachage kuwa uoga na kutojiamini ndio kunakopelekea mtu mmoja kuwa amiri jeshi mkuu na mwenyekiti wa chama twawala.
Bila ya kuwa muoga, mnafiki na mtu wa kujipendekeza, huwezi kuwa mwana CCM.
 
Hivi hawa watu hawajui haya mambo au wanadharau tu?

Wao si ndio wenye taarifa zote?
MaCCM hayana maarifa, wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii, wana vichwa lakini ni vya kufugia nywele tuu.
 
Ndio hateui anapendekeza kamati kuu ndio huidhinisha na halmashauri kuu na mkutano mkuu
Yeye ndiye muanzisha mwendo... Kwa maana nyigine hakuna mjumbe mwingine wa kamati kuu ya chama chenu Mwenye jina la anayetaka awe Makamo wa mwenyekiti wa chama chenu isipokuwa Mwenyekiti wenu Taifa.

Hivyo vikao vyenu havina nguvu Wala ubavu Mwenyekiti wenu. Vingekuwa na ubavu huo, Lowassa angekuwa mgombea wa chama chenu kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.

Vikao vya CCM ni "rubber stamp" tu ya maamuzi ya Mwenyekiti wa chama chenu. Ndiyo maana Magufuli aliwapelekesha sana.
 
Back
Top Bottom