Sina vithibitisho ila hiyo idadi ya 16M Kama ulivyoelezea inatia mashaka.
Jambo moja anapaswa ajue ni kwamba , Kura Ni Siri ya mtu.
Ingekua idadi ya wanachama ndio kura. Basi NEC / Sheria ingehitaji ijulikane tu idadi ya wanachama kwa kila Chama. Kisha chenye wanachama wengi. Au sahihi zaidi Kama Kuna chenye wanachama wanao zidi nusu ya idadi ya, wenye kupiga kura Basi Chama chenye wanachama hao wangetangazwa tu washindi, hasa kwenye Uraisi.
Lakini mtu aweza kuwa mwanaChama wa Chama Fulani lakini asiafiki sera ya Chama hiko hivyo kumpigia mwengine
Swala kubwa zaidi ajue wengi hao wenye Kadi za CCM ambao ndio wanahesabiwa Kama wanachama, wanazo kwa Maslahi binafsi tu.
Wapo wenye kadi ila hawaafiki sera na itikadi za Chama, na hataipipigia CCM.
Wapo wenye Kadi za CCM ila hawakubaliani na Mgombea au wagombea wao wataka ashinde mwingine tofauti na wa kwao. Hawataipigia CCM.
Wapo wenye Kadi, hawaafiki sera na itikadi, hawaafiki mgombea, na Wala hawaipendi CCM ila wanakadi ili Mambo yao yaende..na Hawa wapo wengi tu.
Hawa hawataipigia CCM.
Wapo wale wasanii zaidi. Wana kadi ya Chama zaidi ya kimoja
Aidha wapo kimaslahi , au kwa sababu nyingine tu lakini si kwamba Ni wapenzi wa CCM.
Hawa pia wengi tu hawataipigia CCM Wala kuwapigia Kampeni za chini kwa chini. Zile za mkono kwa mkono.
Hivyo CCM wasijidanganye. Wao waendelee tu kufanya Kampeni kwa nguvu kushawishi watu waipigie kura.
Kisha wasubiri Box la Kura ndio Litasema ukweli na kutupa ukweli. Waache box ndio litaamua.