CCM wote ni walewale, lakini kwangu mimi Naona afadhali kuongozana na Rais Samia kuliko aliyepita

CCM wote ni walewale, lakini kwangu mimi Naona afadhali kuongozana na Rais Samia kuliko aliyepita

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Nchi sasa imepumua, hakuna kupotezwa, hakuna kutekwa, hakuna kutukanwa,hakuna kufokewa hakuna uongo, hakuna vitisho, hakuna kubaguliwa hakuna kunyanyaswa kwenye nchi yeti wenyewe. Kama ukiniuliza kati ya wawili hao mimi ni bora samia.Yule jamaa hakua mtu.

Hofu inapungua taratibu kwa sababu alipandikiza watu wake kila sehemu na bado wapo.

Narudia tena CCM sio watu ila ni bora samia kuliko yule jamaa.
 
Dawa ya CCM ni moja tuuuu - KATIBA MPYA.

Hata wao kwa wao wanaogopana na kutishana sababu ya katiba hii...we uliona wapi duniani Spika wa Bunge analia lia.

Rais wa Tanzania ni Mungu mtu..anaweza kuamua hatima yako muda wowote akitaka...
 
..hakuna hotuba za kikabila.

..au kila mteuliwa kutajwa kabila lake.

..na vijembe vya kutwezana kikabila.

..pia ibada za jumapili zimetuliwa hakuna kuvamiwa.

..halafu hata Kingereza hakichukiwi kama wakati ule.

..Na lugha yetu ya Kiswahili tunaienzi kwa kuzungumza kwa ufasaha.
 
Tumuache apumzike Sasa, Sasa ni wakati wa kuondoa mapandikizi yake. Yeye alishafukukiwa.
Sawa Mkuu ila nia yangu ni kumsifia Samia inatokea ni lazima umlinganishe na aliemtangulia.

Hamna namna kama alifanya vizuri au vibaya atatajwa tu kwa Maisha yote.

Mbona Nyerere kila mara tunamtaja?
 
Hata mimi aisee,kwanza sijaona mwingine Kwa sasa labda angekuwa Mwinyi,waliosalia wengi wao ni wapuuzi.
Tena kuna wengine Magufuli akasome.

Mfano yule alietaka kumfunga Lwakatare kwa Ugaidi wa kuchonga au liemzingua Abdul Nondo akiwa Raisi tutahama nchi sisi wenye Mawazo mbadala.
 
..hakuna hotuba za kikabila.

..au kila mteuliwa kutajwa kabila lake...
Let the man rest, hizi nyuzi zenu za kumhusu jamaa ambaye hayupo tena haziwezi kuponya majeraha yenu.
 
Back
Top Bottom