CCM yaanza kuzifanyia kazi hoja za Lissu

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
3,366
Reaction score
5,209
Wadau wa Jf mnakumbuka wakati wa kampeni Lissu alipinga suala la wamachinga kupewa vitambulisho ambavyo havina picha wala majina. Sasa baada ya kuumbuka kwa kutoa vitambulisho ambavyo havina picha wala jina la mhusika Serikali ya CCM imeamua kujirekebisha baada ya Lissu kuwashambulia wakati wa kampeni.

Kama mtakumbuka wakati wa kampeni rais JPM alidai vitambulisho vya wamachinga vinaweza kutumika kuchukua mikopo. Jambo ambalo lilileta taharuki.

Kwa kuwa Lissu aliwakosoa wanaCcm sasa wameamua kutengeneza vitambulisho vitavyokuwa na majina na picha za wamachinga.

Hii ni wazi kuwa sio kila hoja ya wapinzani haifai,ndio maana Ccm wamejirekebisha.
 
Lissu ni Baba Lao!! Yeye ndiye kiumbe pekee mwenye uthubutu wa kumpa makavu muda wowote ule, yule malaika mkuu.

Baada ya kumaliza tu misheni yake ya kuwapiga za uso mafisi yetu, akajua hujuma za Kisutu zitamuandama! Huyo akaenda zake ubalozini! Kama kawaida yake, jamaa kichwa chake ni sawa na akili za wafuasi milioni 1 wa hicho chama cha mafisi;

Akapaa zake kwenda mahali salama!! Akirudi tena 2025, hakika patachimbika!! Nina imani kwa muda wote huu Mh. Tundu atakuwa ameshatengeneza tayari Baraza lake la Mawaziri! Karibu sana Mr. President 2025.
 
Una maana gani?
Nina maana kuwa kuna kitu kinaitwa M&E kwa chama makini. Si kweli kuwa chama chochote kinaweza kuwa na sera zote madhubuti. Hivyo chama kinachoingia madarakani sharti kifanye tathimini na kuboresha sera zake ikiwa ni pamoja na kukopa kutoka zile za wapinzani wake.

Ni chama mfilisi kitakacho ng’anga’ania sera zake za awali. Na ni ubinafsi mkubwa kwa chama ambacho hakikupata ridhaa ya kuongoza kuficha au kukataa sera zake zisitumike na chama kilicho madarakani. Ujanja ni kuja baada ya miaka 5 kujinadi kwa kueleza kuwa ingawa hamkutuchagua lakini sera zetu ndizo walizochukua na maendeleo yakapatikana. Hivyo mkituchagua safari hii mtapata mengi etc. Cc mama D
 
Nawaza tu itachukua mda gan!? Nkiwa kama machinga nauliza picha tunapigia wap niwahi kesho asbh
 
Aliyekuwa mbunge wa CUF Suleiman Bungala "Bwege" aliwahi kusema akiwa bungeni "serikali ya CCM ni kama patasi, haiwezi kufanya kazi hadi igongwe". Hii ndo maana yake.
🤣🤣igongwe kwa nyuma
 
Lissu ni Baba Lao!! Yeye ndiye kiumbe pekee mwenye uthubutu wa kumpa makavu muda wowote ule, yule malaika mkuu.

Baada ya kumaliza tu misheni yake ya kuwapiga za uso mafisi yetu, akajua hujuma za Kisutu zitamuandama! Huyo akaenda zake ubalozini! Kama kawaida yake, jamaa kichwa chake ni sawa na akili za wafuasi milioni 1 wa hicho chama cha mafisi;

Akapaa zake kwenda mahali salama!! Akirudi tena 2025, hakika patachimbika!! Nina imani kwa muda wote huu Mh. Tundu atakuwa ameshatengeneza tayari Baraza lake la Mawaziri! Karibu sana Mr. President 2025.
Yaaani vijana wa bavicha/ bawacha ni na nani aliyewaloga???

Pamoja na mbwembe zote huyu jamaa ameishia kupata Mbunge mmoja, halafu mna mawazo ya yeye kuwa Rais.

Okey by the way labda Rais wa CDM.
 
Nina maana kuwa kuna kitu kinaitwa M&E kwa chama makini. Si kweli kuwa chama chochote kinaweza kuwa na sera zote madhubuti. Hivyo chama kinachoingia madarakani sharti kifanye tathimini na kuboresha sera zake ikiwa ni pamoja na kukopa kutoka zile za wapinzani wake.

Ni chama mfilisi kitakacho ng’anga’ania sera zake za awali. Na ni ubinafsi mkubwa kwa chama ambacho hakikupata ridhaa ya kuongoza kuficha au kukataa sera zake zisitumike na chama kilicho madarakani. Ujanja ni kuja baada ya miaka 5 kujinadi kwa kueleza kuwa ingawa hamkutuchagua lakini sera zetu ndizo walizochukua na maendeleo yakapatikana. Hivyo mkituchagua safari hii mtapata mengi etc. Cc mama D
Umefafanua vizuri mkubwa chukua peps unywe .
 
Yaaani vijana wa bavicha/ bawacha ni na nani aliyewaloga???

Pamoja na mbwembe zote huyu jamaa ameishia kupata Mbunge mmoja, halafu mna mawazo ya yeye kuwa Rais.

Okey by the way labda Rais wa CDM.
Mnadhani hakuna asiyejua namna mlivyotumia vyombo vya usalama pamoja na tume yenu mbovu ya uchaguzi kuingiza kura bandia kwenye vituo vya kupigia kura, kupiga kura hewa kwa wagombea wenu na pia kuwatangaza makada wenu walio shindwa na kuwa washindi feki?

Kiama cheni kinakaribia. Ni suala tu la muda.
 
Nina maana kuwa kuna kitu kinaitwa M&E kwa chama makini. Si kweli kuwa chama chochote kinaweza kuwa na sera zote madhubuti. Hivyo chama kinachoingia madarakani sharti kifanye tathimini na kuboresha sera zake ikiwa ni pamoja na kukopa kutoka zile za wapinzani wake.

Ni chama mfilisi kitakacho ng’anga’ania sera zake za awali. Na ni ubinafsi mkubwa kwa chama ambacho hakikupata ridhaa ya kuongoza kuficha au kukataa sera zake zisitumike na chama kilicho madarakani. Ujanja ni kuja baada ya miaka 5 kujinadi kwa kueleza kuwa ingawa hamkutuchagua lakini sera zetu ndizo walizochukua na maendeleo yakapatikana. Hivyo mkituchagua safari hii mtapata mengi etc. Cc mama D

I wish wangekua wanakuelewa😍😍
 
Mnadhani hakuna asiyejua namna mlivyotumia vyombo vya usalama pamoja na tume yenu mbovu ya uchaguzi kuingiza kura bandia kwenye vituo vya kupigia kura, kupiga kura hewa kwa wagombea wenu na pia kuwatangaza makada wenu walio shindwa na kuwa washindi feki?

Kiama cheni kinakaribia. Ni suala tu la muda.
Nikuhakikishie hata Mbowe au Lissu au Olesosopi wakiwa ndiyo wasimamizi wa wa uchaguzi CCM itaendelea kuwa palepale.

Ukweli ninkwamba tangu uchaguzi kupitia mfumo wa vyama vingi uanze mwaka 1995 hakuna uchaguzi ambao wapinzani wamewahi kukubali kushindwa.

Si alisema asiposhinda atawaingiza mifugo sorry wafuasi wake barabrani??? Si alisema Magufuli ataondoka madarakani iwe kwa heri au kwa Shari? si alisema huu ni uchaguzi muhimu sana kwa upinzani kwani CCM inategemea mapolice tu ?
 
Back
Top Bottom