Hiyo ndio habari mpya toka mkutano Mkuu wa CCM Taifa kuwa Dkt Emmanuel Nchimbi ndio Mgombea mwezi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu Ujao.
Mabadiliko haya yatakuwa na effect kuanzia mwezi July baada ya Bunge kuvunjwa hivyo Dkt Mpango na Dkt Emmanuel Nchimbi wataendelea katika nafasi zao hizo hizo.
===
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameridhia kwa kauli moja kumpitisha Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea mwenza (Makamu wa Rais) kwa Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mgombea urais, Samia Suluhu Hassan alimpendekeza Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 2025 baada ya Makamu Wa Rais, Dkt. Philip Mpango kuomba kupumzika.
Soma: Breaking News: - Uchaguzi 2025 - Dr. Mpango aomba apumzike kuwa Makamu wa Rais, Rais Samia aridhia ombi hilo
Dkt. Nchimbi aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Januari 15, 2024 katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho kilichofanyikia Unguja, visiwani Zanzibar.
Dkt. Nchimbi alichukua nafasi iliyoachwa wazi na Daniel Chongolo aliyejiuzulu Novemba 29, 2023.
Rais Samia amempendekeza Dk Nchimbi leo Jumapili, Januari 19, 2025 katika mkutano mkuu maalumu jijini Dodoma.