Pre GE2025 CCM yamchagua Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza katika Uchaguzi wa Oktoba 2025

Pre GE2025 CCM yamchagua Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza katika Uchaguzi wa Oktoba 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hahaha kasahau kusema Majaliwa atakuwa waziri mkuu, na Tulua Ackson atakuwa spika wa bunge lijalo.
 
Kwahiyo likitokea la kutokea huyo Nchimbi ndiyo anakuwa Raisi wa Tanzania
Hii nchi ina vituko sana,si ajabu hawajawaza kabisa kuhusu hilo!

Hilo la kutokea na litokee kabla ya July tuone kama Isdor atapumzika akache urais.

At 67 unapumzika nini wakati Wasira yuko 80 na hana habari!

Kutuongezea gharama tu za kuhudumia wastaafu kibao bila sababu ya msingi.

BTW:Mbowe ana la kujifunza!
 
Wapinzani wajipange, bingwa anakabia juu kulinda ubingwa wake....mbinu nzuri sana ya kujihami.
wanatengeneza mashambulizi mfululizo haina kupoa. Mwendo mpela mpela😄😄
 
Naona CCM wamejaribu kuzima hekaheka za chadema. Ngoja tuone. Huu mwaka utakuwa na matukio sana.
 
Nchimbi ni moja wapo ya vijana walioandaliwa muda mrefu sana kushika nafasi kama hizo.

Hivyo sio jambo jipya kwa wengine, ni kutimia kwa jambo lenyewe tu.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Wapinzani wajipange, bingwa anakabia juu kulinda ubingwa wake....mbinu nzuri sana ya kujihami.
wanatengeneza mashambulizi mfululizo haina kupoa. Mwendo mpela mpela😄😄
Wanateua majina mapema ili kura feki zikaprintiwe mapema ili wapate ushindi wa kishindo 🤣🤣🤣
 

Hiyo ndio habari mpya toka mkutano Mkuu wa CCM Taifa kuwa Dkt Emmanuel Nchimbi ndio Mgombea mwezi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu Ujao.

Mabadiliko haya yatakuwa na effect kuanzia mwezi July baada ya Bunge kuvunjwa hivyo Dkt Mpango na Dkt Emmanuel Nchimbi wataendelea katika nafasi zao hizo hizo.
===

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameridhia kwa kauli moja kumpitisha Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea mwenza (Makamu wa Rais) kwa Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mgombea urais, Samia Suluhu Hassan alimpendekeza Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 2025 baada ya Makamu Wa Rais, Dkt. Philip Mpango kuomba kupumzika.

Dkt. Nchimbi aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Januari 15, 2024 katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho kilichofanyikia Unguja, visiwani Zanzibar.

Dkt. Nchimbi alichukua nafasi iliyoachwa wazi na Daniel Chongolo aliyejiuzulu Novemba 29, 2023.

Rais Samia amempendekeza Dk Nchimbi leo Jumapili, Januari 19, 2025 katika mkutano mkuu maalumu jijini Dodoma.

Ana bahati sana
 
Back
Top Bottom