Pre GE2025 CCM yamchagua Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza katika Uchaguzi wa Oktoba 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
View attachment 3206619
Hiyo ndio habari mpya toka mkutano Mkuu wa CCM Taifa kuwa Dkt Emmanuel Nchimbi ndio Mgombea mwezi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu Ujao.

Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Dkt Philip Esdori Mpango ameomba kupumzika,

Mabadiliko haya yatakuwa na effect kuanzia mwezi July baada ya Bunge kuvunjwa hivyo Dkt Mpango na Dkt Emmanuel Nchimbi wataendelea katika nafasi zao hizo hizo.
Isee
 
kwa nini siyo P.Mpango? haijawahi kutokea tanzagiza raisi akabadilisha mgombea mwenza ngwe ya pili, nafikiri kuna kitu kinaendelea na sii kidogo kwenye nchi yetu, mficha ugonjwa kifo kitamuumbua …
Ila hajavunja sheria yeyote
 
CHADEMA nao wamalize uchaguzi wao kwa kuteua moja kwa moja mgombea urais wao kama ccm wamemaliza kila kitu. ligi inaanza mapema januari hii. ACT wameishajipanga tayari wana mgombea wao. ni dhahiri kampeni kali zinaanza kabla ya muda rasmi. Hakuna kuzubaa, zubaa uachwe solemba. CCM wameishamaliza kazi na mbio wamezianza kuelekea uchaguzi mkuu
 
kwa nini siyo P.Mpango? haijawahi kutokea tanzagiza raisi akabadilisha mgombea mwenza ngwe ya pili, nafikiri kuna kitu kinaendelea na sii kidogo kwenye nchi yetu, mficha ugonjwa kifo kitamuumbua …
Fuatilia historia, nyerere alikuwa na makamu wangapi?
 
View attachment 3206619
Hiyo ndio habari mpya toka mkutano Mkuu wa CCM Taifa kuwa Dkt Emmanuel Nchimbi ndio Mgombea mwezi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu Ujao.

Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Dkt Philip Esdori Mpango ameomba kupumzika,

Mabadiliko haya yatakuwa na effect kuanzia mwezi July baada ya Bunge kuvunjwa hivyo Dkt Mpango na Dkt Emmanuel Nchimbi wataendelea katika nafasi zao hizo hizo.
Hongera Sana Mama Samia umeupiga mwingi mno. Nchimbi ni jembe Kweli Kweli
 
#Repost @mwananchi_official
——
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mgombea urais, Samia Suluhu Hassan amempendekeza Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 2025.

Dk Nchimbi ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Januari 15, 2024 katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho kilichofanyikia Unguja, visiwani Zanzibar.

Dk Nchimbi alichukua nafasi iliyoachwa wazi na Daniel Chongolo aliyejiuzulu Novemba 29, 2023.
Rais Samia amempendekeza Dk Nchimbi leo Jumapili, Januari 19, 2025 katika mkutano mkuu maalumu jijini Dodoma.

#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifa
 
View attachment 3206619
Hiyo ndio habari mpya toka mkutano Mkuu wa CCM Taifa kuwa Dkt Emmanuel Nchimbi ndio Mgombea mwezi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu Ujao.

Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Dkt Philip Esdori Mpango ameomba kupumzika,

Mabadiliko haya yatakuwa na effect kuanzia mwezi July baada ya Bunge kuvunjwa hivyo Dkt Mpango na Dkt Emmanuel Nchimbi wataendelea katika nafasi zao hizo hizo.
Sasa yakitokea ya Magufuli nani atashika nafasi?
 
Back
Top Bottom