Pre GE2025 CCM yamchagua Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza katika Uchaguzi wa Oktoba 2025

Pre GE2025 CCM yamchagua Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza katika Uchaguzi wa Oktoba 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ilikuwa swala la muda tu maana aliponea chupuchupu wakati jina Mh. Filipo linapendekezwa.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mgombea urais, Samia Suluhu Hassan amempendekeza Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 2025.
View attachment 3206628
Dkt. Nchimbi ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Januari 15, 2024 katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho kilichofanyikia Unguja, visiwani Zanzibar.

Pia, Soma: Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025

View attachment 3206644
Dkt. Nchimbi alichukua nafasi iliyoachwa wazi na Daniel Chongolo aliyejiuzulu Novemba 29, 2023. Rais Samia amempendekeza Dkt. Nchimbi leo Jumapili, Januari 19, 2025 katika mkutano mkuu maalumu jijini Dodoma.
Ilikua asilimia nyingi kipindi kile awe makamu, ila isionekane alikua mbali na magufuli ndio ikabidi iwe mpango, na majaribio kadhaa ya lazima na yasio ya lazima ya kuondoa yalifanyika ila hayakufanikawa kwa sasa nafasi imepatika isiyo na walaki.

In shoy nchi haina makamu wa rais
 
Hiyo ndio habari mpya toka mkutano Mkuu wa CCM Taifa kuwa Dkt Emmanuel Nchimbi ndio Mgombea mwezi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu Ujao.

Mabadiliko haya yatakuwa na effect kuanzia mwezi July baada ya Bunge kuvunjwa hivyo Dkt Mpango na Dkt Emmanuel Nchimbi wataendelea katika nafasi zao hizo hizo.
===

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameridhia kwa kauli moja kumpitisha Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea mwenza (Makamu wa Rais) kwa Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mgombea urais, Samia Suluhu Hassan alimpendekeza Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 2025 baada ya Makamu Wa Rais, Dkt. Philip Mpango kuomba kupumzika.

Soma: Breaking News: - Uchaguzi 2025 - Dr. Mpango aomba apumzike kuwa Makamu wa Rais, Rais Samia aridhia ombi hilo

Dkt. Nchimbi aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Januari 15, 2024 katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho kilichofanyikia Unguja, visiwani Zanzibar.

Dkt. Nchimbi alichukua nafasi iliyoachwa wazi na Daniel Chongolo aliyejiuzulu Novemba 29, 2023.

Rais Samia amempendekeza Dk Nchimbi leo Jumapili, Januari 19, 2025 katika mkutano mkuu maalumu jijini Dodoma.

Kwa nin na wabunge wasiteuliwe waliopo ili tuende nao kabsaa??
 
Kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM imempitisha Dr. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza wa urais katika uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu.

Kama CCM watashinda uchaguzi huu Dr. Nchimbi atakuwa makamu wa rais hadi 2030. Na baada ya hapo uwezekano ni mkubwa akapenda kugombea urais wa JMT.

Kwa hiyo kuanzia 2030 uwezekano ni mkubwa kuwa CHADEMA wakawa wanapambana na Nchimbi. Huu utakuwa wakati mzuri kwa CHADEMA kuweza kufurukuta, kuna uwezekano mkubwa. Kwa ujumla Nchimbi ni mwanademokrasia lakini pia ni mtu dhaifu. CHADEMA jipangeni vizuri.
Nchimbi ni dhaifu? Jidanganye
 
kwa nini siyo P.Mpango? haijawahi kutokea tanzagiza raisi akabadilisha mgombea mwenza ngwe ya pili, nafikiri kuna kitu kinaendelea na sii kidogo kwenye nchi yetu, mficha ugonjwa kifo kitamuumbua …
Unaambiwa aliomba kupumzika na akakubaliwa!
 
Hii Haraka Ya Hiki Chama Kuanza Papara Namna Hii
Lazima Kuna Mengi Sana Tuvute Subira
 
Hiyo ndio habari mpya toka mkutano Mkuu wa CCM Taifa kuwa Dkt Emmanuel Nchimbi ndio Mgombea mwezi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu Ujao.

Mabadiliko haya yatakuwa na effect kuanzia mwezi July baada ya Bunge kuvunjwa hivyo Dkt Mpango na Dkt Emmanuel Nchimbi wataendelea katika nafasi zao hizo hizo.
===

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameridhia kwa kauli moja kumpitisha Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea mwenza (Makamu wa Rais) kwa Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mgombea urais, Samia Suluhu Hassan alimpendekeza Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 2025 baada ya Makamu Wa Rais, Dkt. Philip Mpango kuomba kupumzika.

Soma: Breaking News: - Uchaguzi 2025 - Dr. Mpango aomba apumzike kuwa Makamu wa Rais, Rais Samia aridhia ombi hilo

Dkt. Nchimbi aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Januari 15, 2024 katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho kilichofanyikia Unguja, visiwani Zanzibar.

Dkt. Nchimbi alichukua nafasi iliyoachwa wazi na Daniel Chongolo aliyejiuzulu Novemba 29, 2023.

Rais Samia amempendekeza Dk Nchimbi leo Jumapili, Januari 19, 2025 katika mkutano mkuu maalumu jijini Dodoma.

Chongolo alijiuzuru na Mpango ameomba apumzike?
I smell a rat.
 
Back
Top Bottom