Ni hivi,wapinzani, baada ya Membe kufukuzwa CCM, nawashauri ikiwezekana hata katika vyama vyenu msimpokee na hata mkimpokea,kamwe msimpe uongozi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Kwa sassa ukiwa kiongozi ndani ya CCM, thamani yako huwa ni ya kawaida kabisa, ila ukitoka CCM na kujiunga upinzani,basi thamani yako nayo inapanda na CCM huanza kukutamani na kutaka kukurudisha ndani ya chama chao ambapo ukisharudi,thamani yako inashuka tena(unakuwa wa kawaida tu).
Na hii si kwa wana-CCM tu,bali hata kwa viongozi wa upinzani katika ngazi mbalimbali na ndio maana hufanyika juhudi kuwafanya wahame vyao na kujiunga na CCM ambapo baadh yao hupewa vyeo.
Hivyo, huyu Membe leo hii CHADEMA au ACT-Wazalendo mkimpokea na kumpa cheo,basi mjue thamani yake itapanda tena na CCM wataanza juhudi za kumrejesha au wanaweza kumfikisha Mahakamani kwa tuhuma za kisasa(uhujumu uchumi).
Last but not least, wanasiasa,hasa hawa wa CCM si watu wa kuwaaminiki kwani hizi zinaweza pia kuwa ni mbinu tu za kuelekea uchaguzi mkuu wa baadae mwaka huu hivyo "msilogwe" kumpa nafasi Membe ya kugombea uongozi hasa uraisi iwapo atataka kufanya hivyo kupitia upinzani-mnaweza kuuziwa mbuzi kwenye gunia.
Tambueni hili:Wanasiasa wa Tanzania hawana urafiki wala uadui wa kudumu, bali wana masilahi binafsi ya kudumu wao kama wao.