CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

hawa ndugu walitofautiana kambi toka wakati uleee! mmoja alikuwa timu Membe ambaye ni Membe mwenyewe mwingine alikuwa timu Lowasa na ukiangalia timu Lowasa wote wanarudi kundini. hawajawahi kukubaliana na sasa inaonekana timu Lowasa wananguvu katika chama (hii ni kwa jinsi nionavyo mimi)
 
kama ni mshindi ahamie ACT watu wakutane kwenye ballot paper, mi nimefurahi sana, jamaa alikuwa akijimwambafayi mno....aanzishe chama chake aone kama wale waliokuwa wakiongea chobis watamfata huko.
Ni dhahiri Membe wamefukuza kwa sababu wamemwogopa..

Kwa hili Membe ni mshindi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dunia hugeuka sana leo Membe kafukuzwa chamani na Pole Pole siku nyingine ni Mwingine ha haaa
 
Sasa Chdema wampokee na kumsafisha, then Magufuli atatangaza kumsamehe, Finally anaunga Mkono Juhudi, hapo Chadema watadai walimshtukia tomea mwanzo.
 
ukweli ndo huo hakuna sababu ya msingi athari zake wataziona mbeleni
Leo hii ukimuuliza mwanachama yeyote wa CCM kwanini Membe kafukuzwa hana jibu. Magufuli kamfukuza kwa chuki binafsi kwa kuwa membe ni mpinzani wake ndani ya chama. Wana CCM kuweni makini sana magufuli kaiweka CCM mfukoni mwake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samurai ukimusikiliza Sumaye baada ya kutoka Chadema nako ni mchang'anyiko pia sasa Wa Tz twende wapi au ni wapi penye unafuu?
 
Kosa la membe ni lipi? Au na wewe maamuma unafuata mkumbo kwa sababu magufuli kaamua?
 
Katika siasa za Afrika ni chama kimoja tu cha kijamaa kimebaki na nguvu na hiki ni CCM bila shaka! Nguvu kubwa ya vyama hivi ilikuwa ni Chama KUSHIKA HATAMU! Na katika KUSHIKA HATAMU vyama hivi kupitia propaganda vilizalisha wafuasi wajinga wengi sana!ambao wao huwaambii kitu kuhusu VYAMA VYAO! Vanguard Party!
Bahati mbaya sana Dunia ya KILIBERARI inakua kwa kasi ya ajabu ! Hata CCM Kuendelea kuwepo hai/Imara hadi leo kulinganisha na wenzake kama UNIP,MPLA ni matokeo ya akili kubwa ya Nyerere!
Lakini tunakoelekea, nguvu ya ushawishi wa CCM inapukutika kwa kasi,kutokana na nature' ya viongozi wa sasa na hali ya kisiasa ya leo,ndio maana tunashuhudia CCM ikichagua viongozi kwa kupima upepo na Sio wale makada waliondaliwa ,hata hii ya kuchukua viongozi wa upinzani inadhihirisha kuishiwa pumzi kwa Vanguard Party!
Kwa hiyo siku chache zijazo tutegemee kupungua kwa nguvu za CCM,na kuibuka upinzani imara ambao kama alivyotabiri Nyerere utatoka ndani ya CCM!
Mtikisiko huu ulianza polepole kipindi cha Lowasa na sasa anakuja Membe!
Mwisho tutafikia kama Kenya ambako wanasiasa wanatambaa kama Kambale kwenye dimbwi!
Na ikifikia hatua hii ndipo utaona umuhimu wa Katiba ya Wananchi kama alivyopendekeza Jaji Warioba!
 
Haya mambo ni ya kisiasa zaidi, hao upinzani waendelee na yao na mikakati yao huyo asubiri uchaguzi upite ndio ajiunge na kama watampokea basi asipswe nafasi ya ushauri na si kugombea kama yule mwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…