CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

Hawa akina Abrahman Kinana na Yusuf Makamba walipaswa wawe washauri wake na siyo kushauriwa na Pole Pole na Bashiru Ally au Makonda. Hata waliyoyaongea kwenye simu alizowarekodi kijinai bado ni ushauri mzuri wa kukijenga chama, Mwenyekiti wa CCM kama angekuwa na akili nzuri angechukulia mawazo ya wale wazee positively kuliko kuwadhalilisha kwa kuyaanika na kutaka wamuombe msamaha.

Hili likiendelea usijeshangaa siku nyingine ikatokea akamdhalilisha JK na Mkapa.

Huyu Jiwe analazimisha kupendwa wakati kiukweli wananchi wamemchoka sana.
Hahahah eti wananch wamemchoka hahahahahahahaah hahahahahahahaah Hahahah wananch tunavyo wasingizia mungu anatuona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ccm ni chama chenye mizizi hakitetereki na wala hakuna mkubwa zaidi ya chama!
 
Kazi ipo.CCM ni maji, Membe ni kama samaki. Samaki ataweza ishi akiwa nje ya maji?Labda Mkapa,Jk waingilie. Tutaona mengi.
Sisi ni wapenzi watazamaji na wasikilizaji tu. Ngoja tutege masikio na tukodoe macho kodo.
 
Wasalam wananzengo

Utajiri wa misemo ya kiswahili huweza kutumika kufikisha ujumbe mujarabu kwa muhusika pasi kutokwa na jasho. Naam Mzee wangu Bernard Camilius Membe yamemkuta yale yaliyotarajika.

Alimuiga nzi akavaa KOTI KUBWA SANA ILA HAKUJUA KWAMBA MATAKO YA WAZI kwa jeuri alisikika akisema ndio "ile sauti ni yakwangu 100%" akawaaminisha vijana kwamba "kazi huendana na Bata" chakubanga Zitto Kabwe kama ilivyo kawaida yake akalibebea bango kupata tu-mileage twa kisiasa yake yakapita.

Naona mitandaoni leo tunasoma wasifu wa Membe kuonyesha wema na utumishi wake uliotukuka hata wengine wakiamua kujitoa ufahamu na kumtwika majukumu ya Amiri Jeshi Mkuu, na Mkuu wa Majeshi katika baadhi ya operation hasa ile ya kumtoa Mohammed Bakari wa Anjuani na Lile saga la Majeshi ya Tanzania na Waasi wa M23 nchini DRC.

Mzee wangu Bernard, tafuta chama cha upinzani ukawepo huko ila si kwa ubaya usiende CHADEMA afadhali uende hata CHAUMA.

Wasalaaam

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huoni mzuka kwa sababu ya wivu wa Meko kuwapiga pin wapinzani wake kwakutumia mkono wadola plccm,sasa subiri kipenga kipulizwe uone mzuka ulivyo mwingi,kwanza mitaani watu walivyomiss amshaamsha ya wapinzani ungejua
Pamoja na hilo ila WaTz wengi wamechoshwa na namna siasa zinavyoenda,unafiki ni mwingi kuliko uhalisia iwe kwa wapinzani au chama tawala wote ni wachumia tumbo tu
 
Sionagi chochote Cha maana kwa Hawa watu mpaka mumuite Jasusi mbobezi

Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu unajua kwa nini amefukuzwa? Hakuomba msamaha. Tatizo ni kwamba huyu mtu yeye alikuwa ameogopa, sasa akawa anajitutumua kwa maneno kwenye media, ili aonekana kuwa hajaogopa. Hata siku ile alivyotoka kuhojiwa, namna alivyokuwa anaongea na waandishi wa Habari ilikuwa inaonyesha wazi kabisa kuwa anatumia maneno kufunika uoga aliokuwa nao. Asingekuwa ameogopa, angechukua hatua mapema na asingefukuzwa. USIOGOPE!
 
Hahaha wote wanaotishia kuchukua form kugombea Urais ndani ya ccm lazima wafukuzwe.
Mkiwafukuza wanayo haki kugombea kupitia vyama vingine.
 
Hape sasa Membe atakuwa free kuchagua anagombea urais kwa kupitia chama gani kati ya vile ACT au Chadema
Nadhani this time around ACT ndio wanahitajika kuwa main opposition party, watapata viti vingi kuzidi Chadema..Membe kapewa jukumu Hilo....CCM wanafanya Mambo Yao tena... Hatari sana.
 
Sina hasira ila nawashangaa badala ya kuhoji mnapelekeshwa Kama kiroba cha chumvi. Hii itawatesa sana msipoliangalia hili mtu mmoja ana amua kumfukuza mtu bila sababu za msingi. Eti mnaambiwa ni Siri kuwa mwenendo wake haukuwa mzuri tangu 2014. Waambieni waweke wazi sababu za kumfukuza ni zipi.
Mkuu mbona una hasira sana? Mchukueni ninyi huyo Membe.

Tuliwaambia hii ndio ccm haitazami mtu usoni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwiteni kwenye lichama lenu, kufidia waliondoka, najua yeye ana mtaji wa wanachama milioni 10, tofauti na Lowasa aliyekuwa na mtaji wa wafuasi mil 6 kutoka ccm.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa nyiyi hamujielewi timu yenu kila siku inahaha kununua wachezaji kwa harama yoyoe ile lkn na shangaa muna fukuza benchi la ufundi wanao wapa mbinu za ushindi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom