Makada wa CCM ni wakati sasa wakutubu na kusimamia haki na kuacha mambo yenu ya gizani gizani.
Makada wa CCM ni wakati sasa wakuisimamia Tanzania sio CCM, Tanzania kwanza CCM baadaye.
CCM lazima mtambue CCM ni genge la watafuta maslahi, na kila wakati lazima magenge haya yatofautiane.
CCM kwa sasa ina genge jipya linalojaribu kupambana na magenge mengine, Genge moja lakina Rostam na El tayari limeshacompromise na maslahi yao yamehakikishwa, Genge lingine lakini Membe limeleta jeuri na halitaki kucompromise zaidi ya ofisi kubwa hapo mziki ndio ulipo na anayeumia ni Tanzania na Watanzania.
Ni ukosefu wa akili mtu timamu kusimama mbele za watu na kuiambia dunia eti CCM ni taasisi imara inayojielewa, labda kama unaongozwa na hisia za ushabiki na wewe ni mnufaika wa magenge maslahi ya siasa za CCM na Bongo kiujumla.
Ni wakati sasa wa Watanzania kustuka na kuachana na hili Genge la CCM na baadala yake nchi iende kwa magenge mengine ili heshima irudi kwa wananchi. CCM aiheshimu tena utu wa WAtanzania zaidi ya maslahi ya CCM na watu wake..