CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

Haya ni Mabadiliko makubwa ya kisiasa ndani ya CCM,. Yaani mahojiano yamekamilika mpaka matokeo hawaja Mkolimba hata mmoja wa wahojiwa? 😀😀😀😀
 
Timu Lowasa ishakufa mda . Lowasa tumsahau kwenye ulimwengu wa siasa..
Saiz tudili na timu membe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria iliyopitishwa na wana Lumumba ni kwamba mtu haruhusiwi kugombea mpaka awe ametimiza walau miaka miwili ndani ya chama.
Alafu na anawekewa ulinzi mkali kila akimove taarifa zipo na marufuku kusafiri bila idhini .
Naomba niishie hapo
 
Hii ndio CCM aliyoiacha Baba wa Taifa Mwalimu J.K Nyerere. Chama hiki ni lazima kiheshimike, asitokee mtu mmoja mpuuzi anayejaribu kuvuruga Chama. Pongezi kwa Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi kwa maamuzi hayo.
 
Hana lolote Mamba nguvu zake ziko majini huku nje mweupe tu.!
 
Huwa naamini hakuna sias nje ya chama cha cha ccm,,,ukitaka siasa basi uwe mwanachama wa ccm.
This is monopolistic.

Membe atulie kabisa.maana hakuna serikali mbaya kama ya sasa.they can do anything to set him silent.
Bora uzima.
 
Hii ni wazi kabisa Magufuli aliona Membe ndio mpizani mkubwa kwake, ilikua inatafutwa sababu tu.
Mtukufu Rais akae akijua ana miaka mitano mingine na yeye yatakuja kumkuta tu.
 
You are wrong...uamuzi huu siyo was kuwakomoa Hawa ma-komredi...hii no adhabu kwa makosa ya uchochezi, usalti na hata uhaini...kumsema Rais kuwa 'amechanganyikiwa' ni kosa kubwa kabisa ...it is insubordination of the highest degree...

Nina uhakika kabisa kuwa ingekuwa ni China mmoja au wawili wangefungwa maisha na pengine hata kupigwa risasi...na siyo China tu hata Rwanda au Uganda ukifanya kosa Kama hili mhusika unaipata fresh....binafsi huwa nashangaa kuona namna baadhi yetu tusivyoelewa unyeti wa nafasi ya Rais...wdngine wanadhani Rais ni sawa na cheo cha katibu kata au balozi wa nyumba ambao unaweza 'kuwasema' utakavyo...

Rais wa nchi yetu ni 'muziki' mwingine kabisa...ni head of state and commander in chief of the armed forces.,ni Rais wa nchi na kioo Cha taifa...ndiye mwajiri mkuu na 'mwenye' fedha za nchi kwa mujibu wa katiba...he is very powerful....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…