Ccm Ni chama dume, ni chama kikongwe... Membe ni mwanachama wa muda mrefu wa ccm, kwa hiyo hiki chama Kiko ndani ya damu yake, piga ua hawezi kujiweka nje ya ccm na akifanikiwa kimwili basi kiroho lazima abaki ccm.
Kuna mifano mingi ya watu wengi Sana waliojiondoa au kuondolewa ccm na dakika,/siku/miezi/miaka ya mwanzo mwanzo wakajitutumua kwa hasira, misimamo, mikakakati na malengo kibao kwa ajiri ya mapambano ila hasira zikitulia wanaanza kujuta, kujilaumu na kujiona wamepungukiwa na vitu vingi sana.
msione anajikaza, huko alipo yuko anajipima afanye nini asalimu amri ama aendeleze ubishi wa kimapambano matokeo yake abadili lifestyle yake yote aliyoizoea yeye na familia yake.
kupitia sakata lake tunajifunza mambo mengi Sana kwamba pamoja na kupambana kwa ajiri ya unazoona ni haki zako lakini kumwangalia kwa kina unayepambana nae ni Jambo la msingi sana.
MWANA KUYATAFUTA, MWANA KUYAPATA.
USIGOMBANE NA BABA YAKO.
uzi tayari......
Sent using
Jamii Forums mobile app