CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

Mimi kinachonishangaza Sana ni musiba, hakuna wa kumgusa
Na hata katika videos zake alishawahi kupendekeza kwamba Membe afukuzwe uanachama, na ndicho kilichotokea.
Labda Musiba ni oracle. Zitto alisema anamtaka mwenye mbwa. Nami ningebahatika kumwona Zitto ningemwambia kuwa ukitaka kumpata mwenye mbwa, kamata hiyo mbwa funga mnyororo penye mti kaa pembeni utaona mwenye mbwa anakuja kuchukua mbwa wake. Au piga hiyo mbwa sana vunja mguu wa mbele na meno mwache aondoke anachechemea halafu fuata nyuma, utaona nyumba atakakoingia ndiko kwa mwenyewe. Sijui Zito anakwama wapi!
 
Chadema wakimchukua nitajua ni wagonjwa wa akili.
Mh Membe kapoteza sifa ya kuwa mwanachama wa CCM na SIYO sifa yakuwa mwanasiasa. Milango iko wazi kwake kwenda chama chochote cha siasa Tanzania.

Mfano akija Chadema tutamsafisha kisha ninyi kama kawaida yenu mtamtamani tena na mtamnunua kwa bei mbaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfukuzwaji atulie, sidhani kama atapata sympathy kwa jamii kubwa kama anavyofikiria. Ajiandae kuomba uanachama upya wa Chama chake hicho kilichomfukuza.
 
Ni dalili dhahiri, hata oct 2020, anataka kupita bila kupingwa. Yupo level ya juu ya kutukuzwa. Watakaojitokeza nje kupambana watapewa note vinginevyo kadi nyekundu, hakuna mechi uraisi bali ushindi wa mezani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kimpango, Ingekuwa hivyo wasingmfukuza uanachama wangekuja mtosa kwenye kura ya maoni kama lowasa .
 
CHAMA KWANZA,,, MISINGI MIIKO NA MAADILI YA CHAMA LAZIMA YAZINGATIWE. HAKUNA KUPEPESA MACHO KWA WASALITI WA CHAMA KIKUBWA KAMA CCM. PONGEZI KWA HALMASHAURI KUU KWA MAAMUZI SAHIHI, TUPO NYUMA YENU. 2020 HATUACHI KITU.

Folded hands


Folded hands


Folded hands


Folded hands
 
Huyu mzee haaminiki kabisa anaweza kujitokeza na kukanusha yote tuliyoyasikia ngoja tusubiri.
 
Ni dalili dhahiri, hata oct 2020, anataka kupita bila kupingwa. Yupo level ya juu ya kutukuzwa. Watakaojitokeza nje kupambana watapewa note vinginevyo kadi nyekundu, hakuna mechi uraisi bali ushindi wa mezani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nasikia eti hata ubunge aligombea na wengine ile awamu ya kwanza tu, zilizofuata tatu zote alipita bila kupingwa.
 
Ni hakika wazi membe alikuwa anaendeleza chini chini compain ya urais,

na kwa makundi aliyokuwa nayo yalikuwa nyuma yake kumuunga mkono,wengi wanaitazama ccm kama imeimalika sana kwasababu ya wapinzan kuhamia huko,lakin ukwel ni kuwa hakuna wakat mgumu kama huu ambao serikali ya CCM inachukiwa na baadh ya watu ndani na nje ya nchi,
kwa uoga wa kufunguliwa mashtaka na kukosa mkate wanaamua kuunga sera zote ziwe rafia au zisizo rafik.

Kufukuzwa kwa membe ni salam kwa wengine lakin kutasababisha makundi ambayo yataongezeka chini kwa chini na hatimaye siku mmoja kuibukia pasipo kujulikana yalikuwa wapi...
 
Kampeni meneja mwaka huu wa mgombea uraisi wa CCM anakuwa nani? Mh. Kinana ametumika kama kampeni meneja wa Mh Kikwete na baadaye Mh Magufuli; jee CCM itamteua nani kuchukua nafasi ya Kinana?
Mku wao walisasema kwamba CCM ni kiwanda wanao watu wengi tu
 
Habari zinazoenezwa kila mahali ni kuwa nchi imepata maendeleo makubwa kwa miaka hii minne. Mtu tunayeambiwa ameyaleta haya yote anamwogopa nini mtu ambaye katika miaka hiyo minne alikuwa tu nyumbani kwake hajaleta maendeleo yoyote? Hivi hawa wawili wanaweza kushindanishwa uzani mmoja? Sasa hofu ya nini mbona mimi sielewi?
Au labda tunayoambiwa ni mafanikio sio kweli?
Ushamba wa yule jamaa unaligharimu taifa big time
 
Back
Top Bottom