CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

Boniphace Kichonge,
Naonya CCM wasifanye Maamuzi ya Hasira na Kukomoa dhidi ya hawa Makada Waandamizi kwani wanaweza wakaja Kujuta kama si Kujutia hapo baadae.

Nimeonya hivi hasa baada ya kupata za chini chini kuwa Maamuzi yatakayotolewa dhidi yao yatakuwa ni ya Kuwakomoa zaidi badala ya kuwa ya Kibusara kwa Afya na Ustawi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
CCM ni chama kikubwa sana, hao watu hawana ubavu wa kufanya Ccm iyumbe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bu'yaka,
Nadhani kwa maana nyingine tunafahamu wewe jeuri lakini kwasasa tunakuhitaji na hatutakuachia lakini muda mwafaka ukifika utajuta kuzaliwa- KARIPIO. 🙂
 
Kilichofanyika ni divide and rule!! Utatu wao kwishney! Mmoja nje wawili ndani huku midomo imefungwa! Chezea chichiyemu weye!
 
IGWE,
Hilo ni onyo kwa kumstahi tu, kwa sababu aliiogesha ccm ikawa safi ila akajichanganya kwa kukaa na membe siti moja......HANA NGUVU ILA HEKIMA NA BUSARA TU ZIMEMLINDA
 
MR KUO,
Ccm ni wanachama. Mfumo umeundwa na unafanya kazi kupitia wanachama. Ss huyu uwezekano ni mkubwa kuwa yupo nje ya jina CCM ila mfumo bado unambeba.

Hawezi fanana na aliye nje ya mfumo wa ccm. Akitoka nje ya mfumo hapo hata matamko utayaona ni ya kujimwambafai.

Ukisikia kajiunga na chama chochote nje ya CCM basi ujue either mfumo umemtenga au yupo kwenye kazi maalum. Ila kwa sasa bado.
 
Kilichofanyika ni divide and rule!! Utatu wao kwishney! Mmoja nje wawili ndani huku midomo imefungwa! Chezea chichiyemu weye!
Akili kubwa ilitumika. Wangepigwa nyundo zinazofanana madhara yangeonekana haraka sana, ila sasa hapa waliotakiwa kuleta madhara wanatakiwa wachague A au B.
 
Iwapo Membe baada ya ya mchakato wa 2015 yeye bado ana kinyongo, basi huyo siyo yo kiongozi wa nchi hata kidogo. Kumtoa CCM ni jambo jema kabisa, na ningeshauri hata CHADEMA wasimkaribishe ingawa wana addiction ya kubeba yoyote anayekataliwa na CCM, ni afadhali safari hii wagome kufanya hivyo.
 
Bw.membe karibu Ubaoni,Ikiwa Azma ya ccm itatekelezwa na halmashauri kuu na kuungwa mkono,basi tuko wengi ubaoni nje ya ccm,tena wengine hatuipendi hata kuiona duniani.
Lakini ujuwe unapokuwa madarakani lazima utengeneze escape root ili baadae ambo yakikuchachia uwe na pa kutokea.
CCM ina wahuni wengi sana siku hizi,kule kustahianakumetoweka kabisa nakujali mchango wako wa muda mrefu katika chama ,au uzee wako kama mzee kinana pia haupo tena ndani ya ccm.
WELCOME ABODE COMRED MEMBE
 
Dah, tayari amesha malizwa kisiasa, mimi naamini nje ya Ccm kamwe huwezi fanikiwa kisiasa, hakika huo ndio mwisho wa ndoto zake. Alipaswa asome alama na pia alipaswa apate ushauri Kwa walio mzidi uzoefu ndani ya ccm huenda yasinge mkuta yaliyo mkuta! Pole sana ndugu membe, nakushauri kuna maisha baada ya siasa sio lazima uwe mwana siasa, kila la heri
 
Ama kwa hakika CCM ni chama kikubwa chenye demokrasia pana tofauti na Chadema.

Awamu iliyopita akiwa Katibu mkuu wa CCM mzee Kinana alinukuliwa mara kadhaa akiwaita mawaziri wa serikali yake kuwa ni mizigo lakini leo yeye ndio amegeuka kuwa mzigo mbele ya Wasomi wanaokiongoza chama kwa sasa.

Niishie hapo Tafadhali.

Maendeleo hayana vyama!
 
Ama kwa hakika CCM ni chama kikubwa chenye demokrasia pana tofauti na Chadema.

Awamu iliyopita akiwa Katibu mkuu wa CCM mzee Kinana alinukuliwa mara kadhaa akiwaita mawaziri wa serikali yake kuwa ni mizigo lakini leo yeye ndio amegeuka kuwa mzigo mbele ya Wasomi wanaokiongoza chama kwa sasa.

Niishie hapo Tafadhali.

Maendeleo hayana vyama!
Maendeleo hayana chama
tapatalk_1579804615718.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom