CCM yatoa Baraka zote kwa DP World kufanya uwekezaji wa Bandari

Kuna ukinzani sana na hii "IGA" na taarifa hiyo hapo juu!

CCM must go. Wameshindwa kuiongoza Serikali na wanashindwa kujiongoza....in short wanashindwa NCHI

Mwenye taarifa kamili ya hiko kipengele cha ilani ya CCM kinachosema....Bandari igawiwe kwa Waarabu wakiweke hapa
Mama anaifungua nchi mnataka muendelee kupiga hela kila ripoti inayokuja? Mwarabu alikuwa na hiyo bandari toka 1896,

Mlisema waarabu wataleta ugaidi sasa ndio wanakuja kukuleteeni maendeleo na kukustaarabisheni, mulimtukana sana maalim seif sasa mumeenda huko huko kukomboa nchi yenu
 
Bandari yako unayo mwenyeo, ile dar es salaam anapewa mwarabu, mama anakufungulieni nchi, mtapata ajira

Mlisema waarabu na waislam ni magaidi sasa mumeenda kuwapigia magoti washike
Bandari mpate maendeleo, dar es salaam itabadilika itakuwa kitov cha biashara east africa na nchi majirani

Bandari hailiwi tokeni ushamba mupate maendeleo
Kwa hiyo mnachotetea hapa ni Uislamu na Uarabu?
 
Wewe unaongea nini? Hujui kama tumekopa trillion zaidi ya 1 World Bank? Na hiyo pesa imeshafanya kike kinachodaiwa kitafanywa na DP World, sasa kama sio uwendawazimu huo ni nini?

Pia hawa waty wameridhiana kupewna misamaha ya kodi kwa mapato wanayoingiza wao, sasa si ukausome mkataba..?!
Acha uzushi, huelewi chochote. Endelea kula chakula cha shemeji tu hapo kwa dadaako. Huna unachojua
 
Hamashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana katika kikao chake cha kawaida makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma leo Jumapili, Julai 9, 2023, chini ya Uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mambo mengine imejadili mkabata wa makubaliano ya uwekezaji na uendelezaji wa bandari nchini.

Mkataba huo ni baina ya Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni yake ya Dubai Port World ambao tayari Bunge la Tanzania limeridhia ushirikiano huo.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema amewaambia waandishi wa habari kuwa, Halmashauri Kuu imepokea na kujadili kwa kina taarifa ya makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari na kuazimia ifuatavyo; uwekezaji na uendeshaji wa bandari ni kwa manufaa ya uchumi wa nchi.

Uwekezaji huo ni utekelezaji wa vitendo wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020–2025, ibara ya 59, ukurasa wa 92. Serikali iongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhalisia uliomo katika makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji huo wa bandari,” amesema Mjema.

=====
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) imepokea na kujadili kwa kina taarifa ya makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari baina ya Serikali ya Tanzania na ya Dubai wakibariki mchakato huo.

Katika kikao chake kilichoketi makao makuu ya CCM, jijini Dodoma leo Jumapili Julai 9, 2023 chini ya Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan, kikao hicho kimesema uwekezaji na uendeshaji wa bandari ni kwa manufaa ya uchumi wa nchi.

Taarifa fupi iliyosomwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema mbele ya waandishi wa habari ilesema uwekezaji huo ni utekelezaji wa vitendo wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25, Ibara ya 59, ukurasa wa 92.

Hata hivyo, Mjema amesema kikao kimekubaliana kuwa, Serikali iendelee kutoa elimu kwa kwa wananchi katika jambo hilo.

"Serikali iongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhalisia uliomo katika makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji huo wa bandari," amesema Mjema.

Halmashauri hiyo ilifanyika baada ya kutanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ambapo pia imezipongeza Serikali zote mbili za Chama Cha Mapinduzi, Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi.

Katika mkutano huo na waandishi, Mjema amesema siyo siku ya kujibu maswali kwani yeye amesoma kile ambacho wamekubaliana na Halmashauri na mambo mengine yasubiri wakati wake.

Pia soma: Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World
DOKEZO - Malalamiko ya mkataba wa DP World yapelekwe CCM, Rais Samia hana makosa sababu anatekeleza sera za chama chake
Wanaotakiwa kuelimishwa na pia kuonywa ni viongozi hso wa ccm. Wao wameamua kusaliti itikadi ya chama chao na kukabidhi uhuru wa nchi kwa kampuni ya nje kwa madharti ya kibeberu. Tena kuna kila dalili za kampuni hiyo kuhonga vigogo na usalama wa wanaowapinga uko hatarini. Ni kukaribisha umafia nchini.
 
Ok waendelee,Ila mie Kama raia huru,niliyesoma na kugradueate kwa ufaulu wa kipekee toka shule ya msingi hadi chuo kikuu,nakataa mkataba huu🙏sababu ninazo,nia ninayo pamoja na dhamira Safi🙏pamoja tuijenge Tanzania yetu🇹🇿🇹🇿
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Safi
 
Hamashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana katika kikao chake cha kawaida makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma leo Jumapili, Julai 9, 2023, chini ya Uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mambo mengine imejadili mkabata wa makubaliano ya uwekezaji na uendelezaji wa bandari nchini.

Mkataba huo ni baina ya Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni yake ya Dubai Port World ambao tayari Bunge la Tanzania limeridhia ushirikiano huo.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema amewaambia waandishi wa habari kuwa, Halmashauri Kuu imepokea na kujadili kwa kina taarifa ya makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari na kuazimia ifuatavyo; uwekezaji na uendeshaji wa bandari ni kwa manufaa ya uchumi wa nchi.

Uwekezaji huo ni utekelezaji wa vitendo wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020–2025, ibara ya 59, ukurasa wa 92. Serikali iongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhalisia uliomo katika makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji huo wa bandari,” amesema Mjema.

=====
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) imepokea na kujadili kwa kina taarifa ya makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari baina ya Serikali ya Tanzania na ya Dubai wakibariki mchakato huo.

Katika kikao chake kilichoketi makao makuu ya CCM, jijini Dodoma leo Jumapili Julai 9, 2023 chini ya Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan, kikao hicho kimesema uwekezaji na uendeshaji wa bandari ni kwa manufaa ya uchumi wa nchi.

Taarifa fupi iliyosomwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema mbele ya waandishi wa habari ilesema uwekezaji huo ni utekelezaji wa vitendo wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25, Ibara ya 59, ukurasa wa 92.

Hata hivyo, Mjema amesema kikao kimekubaliana kuwa, Serikali iendelee kutoa elimu kwa kwa wananchi katika jambo hilo.

"Serikali iongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhalisia uliomo katika makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji huo wa bandari," amesema Mjema.

Halmashauri hiyo ilifanyika baada ya kutanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ambapo pia imezipongeza Serikali zote mbili za Chama Cha Mapinduzi, Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi.

Katika mkutano huo na waandishi, Mjema amesema siyo siku ya kujibu maswali kwani yeye amesoma kile ambacho wamekubaliana na Halmashauri na mambo mengine yasubiri wakati wake.

Pia soma: Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World
DOKEZO - Malalamiko ya mkataba wa DP World yapelekwe CCM, Rais Samia hana makosa sababu anatekeleza sera za chama chake
Ahaa! CCM ikataliwe Tanzania!
 
CCM chama Cha mambwa koko, chama Cha kipumbavu sana. Rais wa hovyo kaja na . mikataba ya hovyo. Kashindwa kukusanya Kodi na kuendesha nchi. Hovyo kabisa anatafuta njia nyepesi za kitumwa
 
Kidumu Chama Cha Mapinduzi. Mama Samia kanyaga twende. Tumechelewa sana kuhusu bandari.
 
Chama cha Mapinduzi kimeweza kuruka mtego wa Wapinzani kuhusu uwekezaji ndani ya Bandari ya Dar es saalam na kuwaacha Wapingaji Wapotoshaji na Wapinzani wakipigwa na butwaa usiku wa leo.Ni maamuzi ambayo hayakutarajiwa na Wapinzani wa mradi huo muhimu,CCM imeshachukua points tatu muhimu so far.

Maamuzi hayo ya Chama yanaenda kumuimarisha zaidi Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2025 Mh Samia Suluhu Hassan,ambaye ndie Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Dhana dhima ya uwajibikaji wa pamoja imeenda kuuwa uongo na propaganda ya Ubara na Uzanzibari.

Ni wazi kuwa maamuzi haya yenye ukomavu mkubwa wakisimama kwenye dhana ya Uongozi na Utekelezaji wa Maamuzi mazito yaani "Selection & Maintainance of Aim" moja ya Principle muhimu katika dhana ya ushindi katika mambo magumu kama hili ya Uwekezaji wa Bandari ya Dar es saalam.

Ni wazi sasa kwamba maazimio ya NEC ya usiku wa leo wanaenda sambamba na mabadiliko katika baadhi ya sehemu ndani ya Chama ili kukabili Upotoshaji na Usaliti wa wazi ndani ya Serikali na ndani ya Chama.Uenda lolote linaweza kutokea usiku huu au kesho baada ya NEC kuazimia na kuigiza Serikali kuongeza kutoa elimu kuhusu Mkataba wa Bandari na DP World.

Ni wazi kuwa baadhi ya Maofisa ndani ya Serikali na ndani ya Chama wanaweza kuingizwa au kupangiwa majukumu mengine kupisha "Makomando" wa CCM kuingia kazini haraka iwezekanavyo mwezi huu.

The suprise is coming hasa katika eneo la Elimu,Mawasiliano na Habari kwa Umma ambalo this time lilionekana kupwaya kwa viwango vya juu sana.

Hii ndio CCM Kaka.

+255746726484.
 
Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
We mwizi tu hakuna lolote ccm Ni janga
 
Back
Top Bottom