CCM yatoa Baraka zote kwa DP World kufanya uwekezaji wa Bandari

CCM yatoa Baraka zote kwa DP World kufanya uwekezaji wa Bandari

Chama cha Mapinduzi kimeweza kuruka mtego wa Wapinzani kuhusu uwekezaji ndani ya Bandari ya Dar es saalam na kuwaacha Wapingaji Wapotoshaji na Wapinzani wakipigwa na butwaa usiku wa leo.Ni maamuzi ambayo hayakutarajiwa na Wapinzani wa mradi huo muhimu,CCM imeshachukua points tatu muhimu so far.

Maamuzi hayo ya Chama yanaenda kumuimarisha zaidi Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2025 Mh Samia Suluhu Hassan,ambaye ndie Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Dhana dhima ya uwajibikaji wa pamoja imeenda kuuwa uongo na propaganda ya Ubara na Uzanzibari.

Ni wazi kuwa maamuzi haya yenye ukomavu mkubwa wakisimama kwenye dhana ya Uongozi na Utekelezaji wa Maamuzi mazito yaani "Selection & Maintainance of Aim" moja ya Principle muhimu katika dhana ya ushindi katika mambo magumu kama hili ya Uwekezaji wa Bandari ya Dar es saalam.

Ni wazi sasa kwamba maazimio ya NEC ya usiku wa leo wanaenda sambamba na mabadiliko katika baadhi ya sehemu ndani ya Chama ili kukabili Upotoshaji na Usaliti wa wazi ndani ya Serikali na ndani ya Chama.Uenda lolote linaweza kutokea usiku huu au kesho baada ya NEC kuazimia na kuigiza Serikali kuongeza kutoa elimu kuhusu Mkataba wa Bandari na DP World.

Ni wazi kuwa baadhi ya Maofisa ndani ya Serikali na ndani ya Chama wanaweza kuingizwa au kupangiwa majukumu mengine kupisha "Makomando" wa CCM kuingia kazini haraka iwezekanavyo mwezi huu.

The suprise is coming hasa katika eneo la Elimu,Mawasiliano na Habari kwa Umma ambalo this time lilionekana kupwaya kwa viwango vya juu sana.

Hii ndio CCM Kaka.

+255746726484.





Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
Hoja hujibiwa kwa hoja
 
Safi sana.

Baada ya hayo, Tunawatakia kila la heri TPA na DP World katika vikao vyenu vya kuunda mikataba.
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Inauma lakini maendeleo inabidi yafanyike.

Pole sana.
 
Hiyo kamati ya wajinga imekutana ikiongozwa na mawazo ya msaliti, ndio maana wamekuja na maazimio batili.

Kamati badala ituambie watanganyika, hayo manufaa ya uwekezaji wa bandarini yapo kwenye kifungu gani kwenye ule mkataba wa hovyo na waarabu, wanatuambia manufaa yapo kwenye ilani ya CCM, ibara ya 59, ukurasa wa 92!.

Kwani waarabu walisaini kwenye ilani ya CCM ya 2020-2025, au kwenye IGA?!

Halafu kuna wajinga wanaotaka hawa vilaza wakosolewe kwa sauti za kubembelezwa, Samia ni msaliti asiye na huruma na watanganyika.
Kumbe unaijuwa IGA? sasa subiri HGA.

Kazi iendelee.
 
Ujinga Pro Max ilani ya CCM siyo katiba ya Nchi
Achana na wajinga tu hao, sisi tukawahi vikao vyetu ofisi mpya za masaki.

Siku hizi ukijiandikisha kule wantuma muda wa dat, moja kwa moja kwenye simu, hakuna mambo ya vocha tena. Data kwa kwenda mbele.
 
Safi sana. Wabongo kazi kulia mkabithi hiyo bandari hajui pa kushika nasemaje mwekezaji aje
 
Kuna ukinzani sana na hii "IGA" na taarifa hiyo hapo juu!

CCM must go. Wameshindwa kuiongoza Serikali na wanashindwa kujiongoza....in short wanashindwa NCHI

Mwenye taarifa kamili ya hiko kipengele cha ilani ya CCM kinachosema....Bandari igawiwe kwa Waarabu wakiweke hapa
Subiri 2025.

Sisi tunasubiri Khanga na Tshirts za 2025 zifikie bandari mpya ya DPW TPA Dar.
 
Mwenzako anasema ni IGA, kinachofatia ni HGA halafu ndiyo mikataba.


Unawahi sana kufikia mwisho, jizuie kidogo. Kitabu ndiyo kwanza chapter ya kwanza.
I support bandari apewe mwekezaji. Wabongo waachiwe insta wapige umbea hakuna tunachoweza period
 
Mnadai kuwa tupewe elimu. Juu ya nini? Walichochambua wanazuoni mlitakiwa mkijibu kisheria sio kutoa majibu ya juu juu tu.
f2520d124f264398b8335dde54e37def.jpg
 
Sawa, sitaki kuwa mnafiki mimi ni capitalist naingiza pesa kwenye hali yoyote.
Japo kama Mtanzania łazima niseme ukweli tuna viongozi wasiokuwa na maono na wanajua hilo.
Pia tuna Watanzania wengi sana wapo duniani kula na kufa.
Kwanini hauwi kiongozi ili tupate kiongozi mwenye "maono"?
 
Wamedhamiria kuuza bandari zetu. Najua kamati hiyo ya CCM walio wengi hawaafiki, wanaogopa na kutetea matumbo yao.
Suluhisho pekee ni nguvu ya wananchi. Tunafanyaje ? Mapendekezo:
1. Waandikie DP World na dunia nzima kwa ujumla kuwa watanzania wamekataa upuuzi wao, na hawatakaribishwa.
2. Watakutana na physical confrontation
3. Polisi na majeshi nanyi teteeni nchi yenu Tanganyika na vizazi vyenu vijavyo. Msikubali kuwaumiza watanganyika kwa faida ya wazazibari na matumbo ya watu wachache.
 
Back
Top Bottom