CCM yatoa Baraka zote kwa DP World kufanya uwekezaji wa Bandari

CCM yatoa Baraka zote kwa DP World kufanya uwekezaji wa Bandari

we unaona jinsi nchi inavyoenda ni sawa? hatukatai uwekezaji sisi shida ipo kwenye mkataba jambo ambalo hata hawataki kulisikia. swala la kuiba ni miaka 60+ nchi inaongozwa na wao hivyo madudu ni ya kwao 100% unajua jinsi tunapambania nchi yetu kwenye ule uzi wa jukwaa la kenya ila kiukweli tulipaswa kuwa mbali zaidi ya hapa na wakulaumiwa ni wao ccm, sio mpaka upinzani wawepo ila wanatakiwa wahoji kwa maslahi ya taifa kuna shida kubwa sana.
acha unafiki mkataba wenyewe haujausoma, watanzania wanapenda kudandia vitu kutafuta kiki utafikiri wanajua kila kitu kumbe nothing, Samia twende wasikucheweshe
 
Bado huja justify kwa nini waarabu wapewe makubaliano yasiyoisha, mind you hatujakataa uwekezaji, Ila uwekezaji wenye lengo la kunufaisha upande mmoja NO, Hafu usiniwekee link za kijinga Sio lazima tuwaige wao, kwa nini wasituige sisi,,,, mwisho Una ID ya kikristu halafu Sio mkristu tunawajua Nyie
shida ya mtu ambaye hajafika hata Kenya, huna exposure yoyote utashauri nini weye?
 
Uwekezaji wa DPW ni mkubwa kulinganisha na haya makampuni yetu. DPW kawekeza Uingereza na Marekani kwa teknolojia za kisasa, hawezi akaingia tu Tanzania kama wawekezaji wengine wadogo wadogo.

Kwa kuwa unajua kiasi kikubwa hicho atakachowekeza, ambacho ni nje ya kiwango kilichowekwa kwa Sheria, Kanuni na Taratibu zetu za uwekezaji, ITAPENDEZA ukikitaja humu JF.

Je, unakielewaje KIFUNGU CHA 4: UPEO WA USHIRIKIANO NA VYOMBO VYA UTEKELEZAJI, kifungu kidogo cha 5. DPW na taasisi tanzu zitawajibika kutafuta ufadhili kwa Makampuni ya Miradi husika kwa ajili ya kuendeleza Shughuli za Miradi.?

Kwenye kifungu kidogo hicho, DPW itatumia Makampuni mengine kutekeleza miradi bandarini, Je, JMT haina uwezo na ujuzi wa kutafuta makampuni kwa miradi ya kuboresha bandari, ikiwekeza kupitia wafadhili?

Kutokana na kifungu hicho, na kwa hoja yako kuwa uwekezaji wa DPW utakuwa mkubwa, wakati itahitajika kutafuta wafadhili, Je, ni nani mwenye uhalali wa kufadhiliwa kati ya nchi (JMT) au kampuni (DPW)?

Nawaza pia kwa sauti na kuuliza, Je, nchini hakuna wawekezaji wa nje, km wa madini, ambao pia gharama za uwekezaji ni kubwa?
 
Hamashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana katika kikao chake cha kawaida makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma leo Jumapili, Julai 9, 2023, chini ya Uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mambo mengine imejadili mkabata wa makubaliano ya uwekezaji na uendelezaji wa bandari nchini.

Mkataba huo ni baina ya Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni yake ya Dubai Port World ambao tayari Bunge la Tanzania limeridhia ushirikiano huo.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema amewaambia waandishi wa habari kuwa, Halmashauri Kuu imepokea na kujadili kwa kina taarifa ya makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari na kuazimia ifuatavyo; uwekezaji na uendeshaji wa bandari ni kwa manufaa ya uchumi wa nchi.

Uwekezaji huo ni utekelezaji wa vitendo wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020–2025, ibara ya 59, ukurasa wa 92. Serikali iongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhalisia uliomo katika makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji huo wa bandari,” amesema Mjema.

=====
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) imepokea na kujadili kwa kina taarifa ya makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari baina ya Serikali ya Tanzania na ya Dubai wakibariki mchakato huo.

Katika kikao chake kilichoketi makao makuu ya CCM, jijini Dodoma leo Jumapili Julai 9, 2023 chini ya Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan, kikao hicho kimesema uwekezaji na uendeshaji wa bandari ni kwa manufaa ya uchumi wa nchi.

Taarifa fupi iliyosomwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema mbele ya waandishi wa habari ilesema uwekezaji huo ni utekelezaji wa vitendo wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25, Ibara ya 59, ukurasa wa 92.

Hata hivyo, Mjema amesema kikao kimekubaliana kuwa, Serikali iendelee kutoa elimu kwa kwa wananchi katika jambo hilo.

"Serikali iongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhalisia uliomo katika makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji huo wa bandari," amesema Mjema.

Halmashauri hiyo ilifanyika baada ya kutanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ambapo pia imezipongeza Serikali zote mbili za Chama Cha Mapinduzi, Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi.

Katika mkutano huo na waandishi, Mjema amesema siyo siku ya kujibu maswali kwani yeye amesoma kile ambacho wamekubaliana na Halmashauri na mambo mengine yasubiri wakati wake.

Pia soma: Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World
DOKEZO - Malalamiko ya mkataba wa DP World yapelekwe CCM, Rais Samia hana makosa sababu anatekeleza sera za chama chake
Yaani mwenyekiti wa CCM (ambaye pia ni rais, Samia) amempa baraka rais wa Tanzania (ambaye ndo huyo huyo mwenyekiti wa CCM, Samia) kuendelea na uwekezaji wa hawa DP world pale bandarini.!!!

Yaani kwamba tulitegemea SAMIA amgomee SAMIA kuwakubali hawa DP world..!!!

TANZANIA SIHAMI NG'O..!!
 
Hapo kwenye halmashauri kuu ya chama kuna watalaam wa masuala ya mikataba?
 
Hizo trillion ni ngapi? Ina maana kila mwaka bandari itakuwa inauzwa? Sijitoi ufahamu ni kwamba hueleweki au huo mkataba hujauona unatupigia tu kelele hapa?
ni kutafutie trillions ngapi kwani unanilipa ? huwezi kutafuta mwenyewe serikali itategemea kupata shillingi ngapi kila mwaka kwenye hizo bandari ambayo ndio price watanganyika have to pay!....kama hunielewi tulia, usinipotezee muda na kichwa chako kama cha konokokono...
 
Yaani mwenyekiti wa CCM (ambaye pia ni rais, Samia) amempa baraka rais wa Tanzania (ambaye ndo huyo huyo mwenyekiti wa CCM, Samia) kuendelea na uwekezaji wa hawa DP world pale bandarini.!!!

Yaani kwamba tulitegemea SAMIA amgomee SAMIA kuwakubali hawa DP world..!!!

TANZANIA SIHAMI NG'O..!!
Kwa vile huna uzoefu labda nikupe mfano wa ukaribukaribu. Mwaka 2015 CHADEMA na CUF walikubaliana sera ya UWAKA kumsimaisha mgombea mmoja kutoka CCM jina lake Lowassa. Kama wangeshinda kungelikuwa na Rais wa Muungani Lowassa toka CCM, wa Tanganyika ni mbowe kutoka CHADEMA na wa Zanzibar ni Maalim Seif. Vilao vya kupongezana na kuweka Ilani kisheria vyote vingemtekea Rais Lowassa toka CCM.
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Hakuna mwenye uwezo wa kutupa majibu ya maswali haya., narudia tena hayuupo. Maana wanafuata irani yao ya chichiem nahawafuati Katiba ya Nchi. Masikio yaliyoziba ipo siku watayafungua tu, time will tell.
 
Kwa vile huna uzoefu labda nikupe mfano wa ukaribukaribu. Mwaka 2015 CHADEMA na CUF walikubaliana sera ya UWAKA kumsimaisha mgombea mmoja kutoka CCM jina lake Lowassa. Kama wangeshinda kungelikuwa na Rais wa Muungani Lowassa toka CCM, wa Tanganyika ni mbowe kutoka CHADEMA na wa Zanzibar ni Maalim Seif. Vilao vya kupongezana na kuweka Ilani kisheria vyote vingemtekea Rais Lowassa toka CCM.
Sasa ndo umeandika nini..!!?? Umefuka moshi wa kuni mbichi..!!
 
Yaani serikali ya CCM imetoa maagizo kwa serikali yake [emoji23].

Mwenyekiti wa chama (Rais) katoa maagizo kwa Rais wa serikali yake [emoji23], yaani aliyesaini mkataba anatoa maagizo kwa aliyesaini mkataba daaa, [emoji23] live longer to wonder the worlds!.
ndo shida ya kofia mbili
 
Back
Top Bottom