Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
Mkuu hao DP wamekubali kuja kuendeleza sekta nzima ya bandari. Kutoa utaalam wa masuala ya uendeshaji kwa chuo cha bandari DMT. Kuongeza uwezo wa wafanyakazi wa bandari pia ni jukumu lililoandikwa kwenye mkataba.Kwa kuwa unajua kiasi kikubwa hicho atakachowekeza, ambacho ni nje ya kiwango kilichowekwa kwa Sheria, Kanuni na Taratibu zetu za uwekezaji, ITAPENDEZA ukikitaja humu JF.
Je, unakielewaje KIFUNGU CHA 4: UPEO WA USHIRIKIANO NA VYOMBO VYA UTEKELEZAJI, kifungu kidogo cha 5. DPW na taasisi tanzu zitawajibika kutafuta ufadhili kwa Makampuni ya Miradi husika kwa ajili ya kuendeleza Shughuli za Miradi.?
Kwenye kifungu kidogo hicho, DPW itatumia Makampuni mengine kutekeleza miradi bandarini, Je, JMT haina uwezo na ujuzi wa kutafuta makampuni kwa miradi ya kuboresha bandari, ikiwekeza kupitia wafadhili?
Kutokana na kifungu hicho, na kwa hoja yako kuwa uwekezaji wa DPW utakuwa mkubwa, wakati itahitajika kutafuta wafadhili, Je, ni nani mwenye uhalali wa kufadhiliwa kati ya nchi (JMT) au kampuni (DPW)?
Nawaza pia kwa sauti na kuuliza, Je, nchini hakuna wawekezaji wa nje, km wa madini, ambao pia gharama za uwekezaji ni kubwa?
Pia kuendeleza kitengo cha majahazi ambacho ni kama kimekufa pale TPA. Wanakuja na mengi ya kisasa ambayo hatunayo muda huu.
DPW wapo mpaka Uingereza na Marekani, unauliza nani mwenye haki ya kufadhiliwa kati ya Tanzania na Dubai?. mkuu punguza masihara.
Huwezi kujenga reli ya SGR yenye kula matrilioni ya pesa halafu uwe na bandari yenye ufanisi ule ule wa kizamani wenye kuwapa mianya wapigaji na wazembe wanaozoea maisha rahisi ya wizi hapo bandarini.
Ni changamoto mpya kuipokea hii kampuni kwa maana ya kwenda sambamba na dunia isiyotusubiri mpaka tuamke vichwani.