CCM yatoa Baraka zote kwa DP World kufanya uwekezaji wa Bandari

Mkuu hao DP wamekubali kuja kuendeleza sekta nzima ya bandari. Kutoa utaalam wa masuala ya uendeshaji kwa chuo cha bandari DMT. Kuongeza uwezo wa wafanyakazi wa bandari pia ni jukumu lililoandikwa kwenye mkataba.

Pia kuendeleza kitengo cha majahazi ambacho ni kama kimekufa pale TPA. Wanakuja na mengi ya kisasa ambayo hatunayo muda huu.

DPW wapo mpaka Uingereza na Marekani, unauliza nani mwenye haki ya kufadhiliwa kati ya Tanzania na Dubai?. mkuu punguza masihara.

Huwezi kujenga reli ya SGR yenye kula matrilioni ya pesa halafu uwe na bandari yenye ufanisi ule ule wa kizamani wenye kuwapa mianya wapigaji na wazembe wanaozoea maisha rahisi ya wizi hapo bandarini.

Ni changamoto mpya kuipokea hii kampuni kwa maana ya kwenda sambamba na dunia isiyotusubiri mpaka tuamke vichwani.
 
Hii hoja ingekua na mashiko kama ungeleta fact kua DPW anawekeza kiasi gani kinachomfanya yeye kua mwekezaji wakipekee zaidi ya apo maneno yako yanabaki kua ni mtazamo wako na ayana maana yeyote
Kwenda bungeni Dodoma ili azimio la uwekezaji wake lipitishwe na bunge ni taarifa tosha kabisa ya ukubwa wa kampuni waliyonayo.
 
Huu ni uwekezaji na hakuna price yoyote ya kulipwa na yoyote. Huu unaoitwa utanganyika ni siasa zilizofilisika zinazotumiwa na huyo Mwabukusi ambazo zinawapata watu wasiofikiria kwa kina.

Ufanisi na utendaji mzima wa bandari unakwenda kubadilika kwa faida ya hao hao wanaojiita watanganyika.
 
Kama hauna "kipawa" cha uongozi utaujuwaje "uongozi" mpaka uweze kusema wenzako hawawezi?
Mungu wangu mbona swali lako ni la kitoto sana. Uongozi siyo udaktari. Naishi ndani ya Jamhuri na mlipa Kodi mzuri najua pale jamii yangu inapokuwa na uongozi mbovu. Sihitaji kuwa na kipawa cha uongozi kujua hilo.
 
Hapo amepata baraka ya CCM nzima ya kuendeleza bandari. Hao kina Mzee Warioba, Mzee Shivji na Mzee Malecela ni sehemu ya CCM nzima.

Ni majibu kwa mitazamo tofauti ya watu wa ndani ya chama. Kwamba kaanza kwanza na chama chake.
 
Ni huo ufanisi ambao utaingiza hizo trillions ndio zilimfanya mama akauza bandari zetu kwa muda usio na kikomo,, hii ni price watanganyika have to pay,ni bandari za Tanganyika tu ndizo ziko kwenye hayo makubaliano na sio za zanzibar unajuaje kama watanganyika ndio wanufaika na sio wazanzibar?
 
Hapo amepata baraka ya CCM nzima ya kuendeleza bandari. Hao kina Mzee Warioba, Mzee Shivji na Mzee Malecela ni sehemu ya CCM nzima.

Ni majibu kwa mitazamo tofauti ya watu wa ndani ya chama. Kwamba kaanza kwanza na chama chake.
Kuna mwana CCM wa kumgomea mwenyekiti wake? Atafukuzwa uanachama asubuhi na mapema..!!! Hayo ya kusema amepata majibu ya watu ndani ya chama NI UNAFIKI KAMA UNAFIKI MWINGINE TU..!!!
 
Uelewa tu unakusumbua nenda Israel mwaka jana wao wameiuza kabisa bandari yao Haifa port kwa Adani group kwa bilioni 1.2 USD .unataka kuniambia waisraeli hawawezi kuijenga nchi yao?View attachment 2683361
Kwa nini mnatolea mifano kwa Nchi ambazo unaona wametangaza hata bei haya huku kwetu imeuzwa kwa bei gani na kwa muda gani ukiona mzungu kaingia mkataba anakua kakagua vitu vingi sana sio sawa na mswahili asiejua kusoma na kuandika umasikini upo kwenye damu wanafanya vitu sio kwa ajili ya vizazi vijavyo ni kwa ajili ya wakati wa sasa...
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Anita hoja haipigwi rungu
 
Hoja yangu haihusu bandari kutokuboreshwa, ikizingatiwa uwezo na ufanisi wa SGR.

Pia hoja siyo ukubwa na uwezo wa DPW kuendesha bandari.

Sababu hizo 2 ndio msingi wa utetezi wa uwekezaji wa DPW kupitia mgongo wa nchi yao, Emirate ya Dubai, bila kutilia maanani vifungu batili vya makubaliano (IGA). Yaani tuko wanyonge ("hopeless") kiasi cha kuingia aina hiyo ya makubaliano. Mimi, na wenye mawazo kama mimi, nasema HAPANA.

Kuna njia sahihi za "nipe-nikupe" ("win-win situation") kuboresha bandari zetu, ikizingatiwa nchi ilivyo na utajiri wa rasimali. Nimetoa mapendekezo kadhaa, ambayo unakwepa kuyahoji, km JMT kutafuta mitaji na kutumia makampuni yenye uwezo, ikiwemo DPW, kuboresha bandari zetu kwa masharti yetu wenyewe kuliko kujiona wanyonge wa kujisalimisha kwa makubaliano yenye kudharilisha.

HAPANA kwa hayo makubaliano (IGA). Serikali iandae kongamano, wadau tujadili yaliyomo kwenye IGA.
 
Povu kama lote!
Mtateseka sana mwaka huu ikiwa ndo mtaishia humu nyuma ya keyboard.
If you're really serious tokeni humu mchukue hatua, otherwise nyie ni debe tupu mwajichosha tu
Mawakili wameshafungua kesi ya kikatiba......ni mwanzo mzuri
 
Mwenyekiti wa Kikao alikuwa ni nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…