CCM yatoa Baraka zote kwa DP World kufanya uwekezaji wa Bandari

Walioingia huu mktaba ovu ni ccm, wanaobariki ni ccm.
ILA CCM wanatakiwa kufahamu kuwa "Raslimali za Tz ni za wa Tz na sio za CCM.
Wameshauza nyingi sana, wamedhulumu sana, raslimali zetu kama zao peke yao!
Wakumbuke mwisho wake ni mbaya sana sana kwao !
 
CCM ni Taasisi yenye madhumuni, imani na Sera ambazo haziungi mikataba ya hovyo. Kama utaweza kutoa mfano hata mmoja tu, hoja yako itakuwa na nguvu.


Kilicho na ukweli ni aina ya wanasiasa walio na uongozi ndani ya CCM na vyama vyote vya siasa nchini, wasiokuwa na "utashi wa kisiasa". Wengi wao ni wanasiasa chumia tumbo.
 
Haya ya kutafuta mitaji unayoyasema ni siasa za miaka yote, zimeshajaribiwa na kushindwa kwenye utekelezaji mzima.

Mtanzania ana sifa ya kuharibu anapopewa kuendesha kitu kwa vitendo lakini ana sifa ya kuonyesha uwezo na umahiri pale unapopata nafasi ya kujenga hoja za maneno.

Rwanda na DRC wameshasaini kuanza kwa biashara hii pana sana, tuwape nafasi ya kutekeleza huu mradi kwa faida ya nchi zetu.

Hivi tunavyopiga kelele eti tufanye sisi wenyewe, Marekani anatumia ushawishi wake huko kusini kwa kuivuta Zambia, Malawi na Angola wasafirishe kwanza mzigo wa Zambia halafu uzoefu ukiwa mzuri kibiashara wahamie kusafirisha mzigo wa DRC maana yake bandari yetu ikose soko maana yake SGR iwe mapambo tu!.

Samia alipokwenda Malawi juzi kwenye sherehe ya uhuru wao lengo lake haswa ni kuivuta Malawi iendelee kutumia bandari yetu, akapiga siasa na Rais Chakwera lakini ndani ya moyo wake alichofata kule ni kuwasihi Malawi wasiungane na Zambia katika kuipa mzigo bandari ya Lobito ya Angola.
 
Imeisha hiyo! We endelea kutokwa povu Mama anachanja mbuga katika kuwaletea maendeleo Watanzania.
 
Kuuza rasilimali ni neno la jumla linaloandikwa kiuchochezi zaid kuliko kujengewa hoja yenye mantiki huo uuzaji wenyewe maana yake ni nini haswa.

Wakati tunapiga hizi siasa za midomoni na humu JF tukumbuke kuwa Rwanda, Congo wameshaipokea hii kampuni kwa kusaini mikataba ya kuanza kazi.

Sisi tunapoteza muda bila ya kuangalia kwa mapana ni kipi tunachokwenda kukipoteza kama taifa. Tunapoteza muda kwenye siasa za harakati wakati dunia halisi haina muda wa kutusubiri eti tuondokane na ujinga kwanza uliomo vichwani mwetu.
 
Hakuna mtu anakataa mkataba, watu wanahoji vifungo hovyo vilivyopo kwenye mkataba......
 
Amebarikiwa sana aliyevujisha mkataba wa Sirikali na DP World.

Wakati wao wakiendelea na propaganda uchwara, huku vijiweni wananchi wanajadili mkataba orijino uliovuja.

Tutaona nani boss, kati yasirikali ya CCM na wananchi.
 
acha unafiki mkataba wenyewe haujausoma, watanzania wanapenda kudandia vitu kutafuta kiki utafikiri wanajua kila kitu kumbe nothing, Samia twende wasikucheweshe
kama hujausoma ni wewe usifikiri kila anayeandika humu yupo kama wewe punguwani wewe
 
HATOGOMBEA .
 
Wewe umeelewa kwanini walipeleka Bungeni huu mkataba?
Bungeni ilikwenda agreement ya IGA, ipate baraka ya wananchi ili miradi ya HGAs iweze kuanza kusainiwa kati ya wanasheria wazalendo na wale wanasheria wa wawekezaji.

Uwekezaji mkubwa siku zote michakato huanzia bungeni. Nadhani unakumbuka namna hayati JPM alivyoshambuliwa akiambiwa kanunua ndege bila ya ridhaa ya bunge.

Sasa suala la ndege lilipigiwa kelele na wadau sembuse huu uwekezaji unaokwenda kuingiza mabilioni ya pesa kila mwaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…