CCM yatoa Baraka zote kwa DP World kufanya uwekezaji wa Bandari

Yamegawana Vipande Vya Dinari Zao Kupitia DP World, Wote Wameoza Na Kupungukiwa Utukufu Wa Mungu
 
Wamebariki mkataba maana bila kufanya hivyo chama chao ccm kitaanguka maana bila fedha za ufisadi ccm itaanguka kwenye uchaguzi na wao hawataki hilo litokee.
 
nimewaona manara,mwijaku,kitenge,zembwela na gerald hando wakichapa mikeka kujibu hoja zako.
 
Ndio kwani wewe unaona insendaje?
 
Wasaliti hao
Hata kama waliyasema hayo yaliyoandikwa kwenye gazeti, tayari wamekwishaonyesha wazi kwamba mpango wa wezi umekwishagunduliwa.

Hilo la "kutoa elimu kwa wananchi" wao wanadhani elimu ya kupotosha ukweli ndiyo itakayokubaliwa na wananchi?

Elimu gani itakayofuta kwenye fikra za wananchi waliyojisomea wao wenyewe kwenye maandishi ya "Makubaliano"?

Watawaeleza wananchi kwamba hayo yaliyomo kwenye nyaraka ile ni maigizo tu, kwa vile "mikataba" itakayofuata ambayo wananchi hawataiona ndiyo itakuwa na maslahi zaidi kwa nchi yao?

Serikali imetumia nguvu nyingi sana kufanya upotoshaji huo, lakini kelele ndiyo zinazidi kuongezeka. Sasa hawa wajumbe wanafikiri serikali itatoa elimu ya aina gani hadi watu wabadili uelewa wao!
 
Nani anahitaji hayo majibu?
 
Uelewa tu unakusumbua nenda Israel mwaka jana wao wameiuza kabisa bandari yao Haifa port kwa Adani group kwa bilioni 1.2 USD .unataka kuniambia waisraeli hawawezi kuijenga nchi yao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…