NDG CHILIGATI, NASEMA SITAKI
Mara baada ya kusoma hayo mawazo ya Kpt Chiligani, kwa haraka haraka, nyuma ya ujumbe wake huo, nimebaini kwamba haswa ndiye 'MSOMI WA VYUO VIKUU MKOA WA DODOMA' aliyetukarimia TAMKO zuri lile. Kama huamini, rudia kuusoma huo ujumbe hapo juu na ulinganishe upepo ulioko kwenye KOO na LADHA ya MATAMSHI inayotoka mdomoni na utagundua kitu.
Sasa kwa kuridhika na hicho nilichokigundua kwenye taarifa hizo mbili, na CUF kukimbilia kiti cha Upinzani Bungeni hata kabla Guu la mwisho la Mwana-CHADEMA kuishia mlangoni wanavyotoka nje na CUF pamoga na NCCR-MANUNUZI kuendelea kuisakama kusikoisha CHADEMA, nasema kwa nguvu hapa (kama Mhariri Mkuu wa Daily News alivyoonyesha uwezo Mkubwa kuliko Sheik Yahaya KUTABIRI kwamba Dr Slaa HATOINGIA ikulu AFTER-ALL) kwamba kwa dakika hii Werema, Mkono na yule Ringo Tenga mkubwa WANAKAMILISHA MUSWADA kwa ajili ya CCM kuwapokonya RASMI Umma wa Tanzania hata huo uwakilishi mdogo walioipa CHADEMA. Kwa msingi huu, ndi maana nasema:
(1) Sitaku Kumzungumza Kpt Mstaafu John Chiligati kwa kuwa taaluma yake ni UTII KWANZA maswali baadaye, na wala HAKI na DEMOKWASIA ni sayari nyingine kabisa kwake,:bump:
(2) Sitaki kumzungumza Chiligati Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM kwa kuwa PROPAGANDA ndio silaha yake ya kufanyia kazi hiyo, nasema
(3) Sitaki kumzungumza Waziri wa Zamani wa Ardi na Maendeleo ya makazi anayetumia muda wake 80 % kwa chama na 10% mapunziko 5% ofisini, na wala
(4) Sitaki kumjadili mheshimiwa sana huyu kwa vigezo vya lipi CCM ina uwezo wa kufanya bungeni kwa sababu CHADEMA haikupata ridhaa ya uwakilishi Bungeni ili watekeleze maelekezo SAHIHI ya chama hicho kwa kuwa naelewa fika kwamba Tanzania yangu sio kisiwa wa kutekeleza UKIRITIMBA WOWOTE usioafikika na Jumuiya ya Kimataifa,
Ninachoomba jamvini hapa, nipeni tu mawazo yake aliyoyatoa kwenye kioo TBC na pia Wanasheria wetu tumwagieni VIFUNGU ndio tupate KUTENDEA HAKI STAHILI mawazo yake hayo. Kumbukeni, Chiligati anayo haki ya kutetea anachokipenda, CCM nacho kama taasisi pia kina haki ya kusikilizwa humu jamvini lakini haki zote hizo zinakosa nguvu na ushawishi wowote mbele ya UMMA mpaka KWANZA WATANGULIE KUTUAMBIO KWA DHATI KABISA NINI WANACHOKIJUA KUHUSU MADAI YA 'MPANGO MZIMA WA UCHAKACHUAJI UCHAGUZI KULE HOTEL LAKAIRO' Mwanza ambayo ndi imetufikisha hapa tulipo leo hii.
Wana JF, Bila VIFUNGU sahihi hapo nembo yetu ya GREAT THINKERS itachuja, Bila majibu ya Njama za Kuiba Kura Uchaguzi Mkuu 2010 kama ambavyo tulivyoshuhudia sote nako tunasema si CCM wala Chiligati anapata MORAL STANDING ya kusikilizwa humu licha ya kuonekana LEGALLY existing.
Niwashilishe kwenu ...