Elections 2010 CCM yatoa tamko kuhusu kitendo cha wabunge wa CHADEMA

Hakuna kitu kama hicho..
Pia Chadema naiamini kwa kubeba wanasheria makini..
 
Inanikumbusha enzi zile tukitaka kugoma shuleni, tunatishiwa kufukuzwa na wakati haki tunayo. Leo ndo nashtukia kumbe ilikuwa system ya ccm kutupandikiza nidhamu ya woga. CHADEMA kaza buti babake...!
 
CCM ni chama sio watanzania, watu ndio power; so hakuna kuogopa, hawana lolote kwani wnageacha kuloloma?
 

Hapa umesema the 'ideal substance!' katiba ni tukufu...kama CDM waliapa kuilinda, hawa wahuni na wachakachuaji wanaoingia madarakani kwa kuifisadi katiba, sio tu wabunge wa chadema kuwakataa, bali watanzania wote wawapinge hata waendapo ktk ziara zao mikoani...hakuna tena woga kwa haki ya kila mtanzania. pamoja daima, bila dhuluma.
 
Nawashangaa watu wana deal na matamshi sijui ya chiligati, hee wake up comrades, hamna issue ya kujadili wa kujitetea hapo, wewe una dhahabu anatokea m2 anakuambia hiyo si dhahabu ni chupa tu nipe mimi nikupe dhahabu(tubadirishane) na kumbe ndo ukapewa chupa haswaa (by baba wa taifa). Kama chiligati ana uwezo huo aendelee na kitakachotokea sisi hatumwambii in advance! Chadema hiyo ilikuwa day 2, sasa tunatakiwa tuingie day 3 na day 4 na kuendelea ya harakati. Ccm ni kama mashetani fulani ambayo yamezoea kutenda maovu mbalimbali.
 
sidhani kama mtu mwenye akili timamu anaweza kutoa tamko kama hilo
 
Maalim Seif nae anadiriki kuilaumu CHADEMA. Je Maalim Seif yupo tayari kubeba damu ya watu waliouawa zanzibar kwa ajili ya kudai demokrasia? Leo hii maalim ni CCM, kina Chiligati wapo wengi
 
We ni kada wa cccm
 
By th way kama huyu Chiligati ndo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM. Basi tatizo la hiki chama ni kubwa kuliko nilivyo dhani coz nikiunganisha na akina Kinana ndo naelewa kuwa kimeoza kuanzia kwenye shina lake.
 

Na ndiyo itakuwa kaburi la ccm. refer madhara waliyoyapata kwa kumsimamisha Zito Kabwe. Huyo alikuwa mmoja tu Je wabunge 46?
 
Hawana ubavu huo hata kidogo Wanaona aibu tu kwa kuumbuliwa na madudu ambayo wanaendelea kuyafanya.
Hana mamlaka ya kuwazuia watu wasicheze KIDUKU CHAO. Awaache waendelee kucheza wakimaliza tutawauliza iwapo hicho ndicho tulichowatuma.
 
Nafikiri huyo Chiligati alikuwa anatumia mdomo kwa sababu anao. Ungekuwa unalipia maneno unayoongea naamini hasingeweza kupoteza hela yake kwa kuongea upupu huo. Kama wanaweza kuwafukuza sasa wanasubiri nini?? Bunge halina huo ubavu huo. Mahakama inaweza imuondoe mbunge kama kulikuwa na petition halali iliyokuwa inahusiana na uchaguzi wake.

Tofauti na hapo CCM wanataka kutumia tu midomo yao kwa sababu wanadamu tulipewa.
 

hapo kwenye rangi am part of the public and i say they are damn right well done chadema
 

hapa nadhani nampigia mbuzi gitaa lakini i will try:-
1. Chadema ilipata wabunge wachache sababu ya kuchakachua na wizi thats why wanaprotest
2. Wangeleta hoja bungeni isingesikiliwa ingezimwa tu, thats why wametumia the perferct way, message sent, and media coverage kibao thats why we are now talking about it now. Nadhani umeelewa dont worry hii ni elimu ya bure natoa
 
Inaonekana elimu ya uraia bado haijawaingia watanzani,kuna umuhimu kwa watanzania kuisoma katiba ili kujua mapungufu yaliyomo.Tuna kazi kubwa ya kuwaelimisha watanzania.Kitendo kilichofanywa na chadema kimemfanya Kikwete kuongea,pinda ameongea,chiligati ameongea,UVCCM wameongea,wanaojiita wasomi wa dodoma wameongea lakini spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania mh.Anne Makinda amenyamaza kimya..Why,kwanini hajaongea?Ni kwa sababu anajua walichofanya chadema kina maana gani katika kukuza demokrasia.Watanzania wengi ni waoga kwa sababu hawazijui haki zao
 
Chiligati = CCM Chili sauce, ni huyu Chili source alimfukuza uanachama wa CCM Bashe, aibu ikamrudia, ukitaka kujua anaongelea MDOMO na Si Ubongo wake, ni kanuni au sheria ipi ambayo eti wabunge wa CCM wanaweza kuwafukuza wabunge wa CHADEMA,...!!!!? anazeeka vibaya kweli huyu OLD DUDE, hawa CCM hawasomi nyakati wanalala, kuanzia uongozi wao wote madudu, sasa mwambie wajaribiu aliyoyasema ataona how it will Backfire the whole country, c'mon Chili do it, unajidanganya kweli
 
a party of emotional youth. Kila action inayofanyika ni kama ya mtoto aliyekarika na kuanza kuvunja glass na sahani. Hasira ikiisha ataomba maji ya kunywa wakati hana glass. Simple example. People are not happy in whatever words you put.
Naona kama vile hapa unajisemea mwenyewe, yaani you are talking to yourself kama yule mwendawazimu vile.
 
Tusome Ibara ya 71 ya katiba ya tanzania,imeeleza wazi sababu zinazoweza kumfanya mbunge apoteze kiti chake cha ubunge,kitendo cha wabunge wa chadema hakiwezi kuwafanya wapoteze nafasi zao .Kesho nabandika kanuni
 
Hayo aliyoyasema Chiligati ni kujitutumua, CCM inajua ikileta hoja hiyo itakuwa imefungulia CHADEMA mlango wakupeleka kesi yao kwa wananchi na hilo litawasha moto nchi nzima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…