Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ilikuwaje mkavipokea kama ni vibovu ukute mlishateganisha na ndoa za watu kwa kutoa DNA za uongo.Hao ni vibaraka wa mabeberu!!
Umeona eh! Na lau kama matusi na kejeli ingekuwa ni vibao ina maana hiyo habari ingekuja wakati bado hata maumivu ya vibao hayajatulia!Sio muda umetoka kutukanwa!!
Na mimi simo!View attachment 1442908
Bodi imekataa madai hayo kuwa si ya kweli na hayana msingi wowote.
My Take
Hii ni aibu tunavuna baada ya Rais kukimbilia kwenye media wakati wangeweza kufanya consultation na wataalamu wakajiridhisha na kuja na hitimisho lisilo na shaka. Kwenye orodha ya wanaopata aibu mnitoe
Hatupendi kuingiliwa kwenye mambo yetu, sisi ni taifa huru!!Ilikuwaje mkavipokea kama ni vibovu ukute mlishateganisha na ndoa za watu kwa kutoa DNA za uongo.
Ndiyo walewale. Hawa si ndiyo wanaisagia meno Tz?Nkengasong sio beberu huyo ni mkikuyu wa kenya
Ukimsikia Mpumbavu yeyote anasema hana Chama, fahamu huyo ni mwanachama wa CCM. Sijui hicho Chama kilishakuwa Cha mashetwani ndiyo maana hawataki kujinasbisha nacho!!?Kwa hiyo na wewe na akili unazojinadi nazo unaamini Corona ya Mafenesi?
Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo la kuchnganya sias, sayansi na kutegemea matokeo mazuri ya kisiasa.Tatizo Rais wetu haoni shida ofisi kupotezewa heshima?
Yeye angeyaacha haya mambo kwa wataalam wanasayansi. Yeye siyo mwanasayansi. Kama ana mashaka yoyote, alistahili kueleza mashaka yake kwa wanasayansi. Wanasayansi ndiyo wangeifanya kazi ya quality control and analysis. Kosa kubwa ni pale Rais anapofikiria kuwa TISS wanaweza kumpa majibu ya uhakika. TISS wengi tunawafahamu, siyo wanasayansi. Wengine hata hawastahili kuwepo huko TISS. Wameigeuza kazi ya Intelligence kuwa sawa na umbea/majungu.
Rais Magufuli amesoma masomo ya Sayansi lakini hajawahi kuwa mwanasayansi.
Tangu amalize PhD yake, hajawahi kuingia maabara kufanya study yoyote ya Sayansi, hajawahi kushiriki conferences zozote za kisayansi ambazo huelezea maendeleo katika fani mbalimbali za Sayansi, hajawahi kushiriki kufanya research zozote za Sayansi.
Kimsingi, yeye ni mwanasiasa. Muda wake mwingi wa maisha yake umeutumia kwenye siasa. Ni mwansiasa kuzidi hata waliosomea masomo ya siasa ambao hawajawahi kufanya siasa.
Ni kosa kubwa kufikiria kuwa ukisomea masomo tu ya sayansi, basi wewe ni mwanasayansi au ukisomea tu masomo ya sheria basi umekuwa mwanasheria, japo unakuwa na advantage ndogo ya uelewa yakiwa yanaongelewa mambo ya fani ambayo masomo ya fani hiyo ulipata kuyasoma.
Rais ni mwanasiasa. Anashinda anaongea siasa, anawaza siasa, analala akiota siasa. Huyu ni mwanasiasa. Asisahau kuwa kuna watu ni wanasayansi, kuna watu ni wataalam wa maabara. Wanashinda kwenye maabara, mazungumzo yao karibia yote yanahusu mambo ya maabara, semina na conferences zote wanazohudhuria, zinahusu maabara, makala nyingi wanazosoma zinahusu maabara, hawa ni wataalam wa maabara.
Vifaa vya maabara havinunuliwi kama mashati. Mtengenezaji wa vifaa vya maabara ili vifaa vyake viweze kufanya kazi iliyokusudiwa, hufanyiwa majaribio, na huidhinishwa na WHO. Kama kweli kuna hitilafu ya uwezo wa vifaa vinavyotumika maabara yetu ya Taifa, wa kwanza tunaotakiwa kuwashutumu ni WHO ambao wameruhusu vifaa hivyo vitumike. Wengine wanachanganya kati ya vifaa vya maabara kwaajili ya kupima Covid 19 na quick test kits za Covid 19. Kuja baadhi ya nchi wamelalamikia quick test kits LAKINI siyo vipimo vya maabara kama hiki tunachokilalamikia sisi. Sasa wewe kulalamikia kitu ambacho hakijaonesha hitilafu sehemu nyingine yoyote, unastahili kufanya scientific tests hasa, na hizi za kuoima mafenesi na kwale wakati mtengenezaji hajaeleza kama kifaa hicho kinaweza kupima hivyo vitu.
Huwezi kwenda kuilaumu WHO kwa namna alivyofanya Rais wetu. Kulistahili kufanyika detailed scientific studies kuweza kuzidisqualify idara za WHO zilizoidhinisha kutumika kwa vifaa hivi.
The whole approach to this matter has been disgracefully wrong. Mwisho wa yote ni aibu kwa Rais wetu na kwa Taifa kwa ujumla.
Sent using Jamii Forums mobile app
Haya sasa aibu yetu aibu yao?
Sisi Watanzania tunamsikiliza rais wetu Magufuli
Rais alisema kuna mawili, yaweza kuwa ni vipimo kutokuwa sawa, au wataalamu kwa makusudi kuhujumu, bado tume haijatoa ripoti ya uchunguzi wao, hakuna mahala ambapo Rais moja kwa moja alisema vifaa ndio tatizo.Sisi Watanzania tunamsikiliza rais wetu Magufuli
TrueRais alisema kuna mawili, yaweza kuwa ni vipimo kutokuwa sawa, au wataalamu kwa makusudi kuhujumu, bado tume haijatoa ripoti ya uchunguzi wao.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi mtu uhujumu vipimo ili iwe nini?!Rais alisema kuna mawili, yaweza kuwa ni vipimo kutokuwa sawa, au wataalamu kwa makusudi kuhujumu, bado tume haijatoa ripoti ya uchunguzi wao, hakuna mahala ambapo Rais moja kwa moja alisema vifaa ndio tatizo.
Sent using Jamii Forums mobile app