mlingoti west
JF-Expert Member
- Mar 16, 2020
- 252
- 195
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tatizo Rais wetu haoni shida ofisi kupotezewa heshima?
Yeye angeyaacha haya mambo kwa wataalam wanasayansi. Yeye siyo mwanasayansi. Kama ana mashaka yoyote, alistahili kueleza mashaka yake kwa wanasayansi. Wanasayansi ndiyo wangeifanya kazi ya quality control and analysis. Kosa kubwa ni pale Rais anapofikiria kuwa TISS wanaweza kumpa majibu ya uhakika. TISS wengi tunawafahamu, siyo wanasayansi. Wengine hata hawastahili kuwepo huko TISS. Wameigeuza kazi ya Intelligence kuwa sawa na umbea/majungu.
Rais Magufuli amesoma masomo ya Sayansi lakini hajawahi kuwa mwanasayansi.
Tangu amalize PhD yake, hajawahi kuingia maabara kufanya study yoyote ya Sayansi, hajawahi kushiriki conferences zozote za kisayansi ambazo huelezea maendeleo katika fani mbalimbali za Sayansi, hajawahi kushiriki kufanya research zozote za Sayansi.
Kimsingi, yeye ni mwanasiasa. Muda wake mwingi wa maisha yake umeutumia kwenye siasa. Ni mwansiasa kuzidi hata waliosomea masomo ya siasa ambao hawajawahi kufanya siasa.
Ni kosa kubwa kufikiria kuwa ukisomea masomo tu ya sayansi, basi wewe ni mwanasayansi au ukisomea tu masomo ya sheria basi umekuwa mwanasheria, japo unakuwa na advantage ndogo ya uelewa yakiwa yanaongelewa mambo ya fani ambayo masomo ya fani hiyo ulipata kuyasoma.
Rais ni mwanasiasa. Anashinda anaongea siasa, anawaza siasa, analala akiota siasa. Huyu ni mwanasiasa. Asisahau kuwa kuna watu ni wanasayansi, kuna watu ni wataalam wa maabara. Wanashinda kwenye maabara, mazungumzo yao karibia yote yanahusu mambo ya maabara, semina na conferences zote wanazohudhuria, zinahusu maabara, makala nyingi wanazosoma zinahusu maabara, hawa ni wataalam wa maabara.
Vifaa vya maabara havinunuliwi kama mashati. Mtengenezaji wa vifaa vya maabara ili vifaa vyake viweze kufanya kazi iliyokusudiwa, hufanyiwa majaribio, na huidhinishwa na WHO. Kama kweli kuna hitilafu ya uwezo wa vifaa vinavyotumika maabara yetu ya Taifa, wa kwanza tunaotakiwa kuwashutumu ni WHO ambao wameruhusu vifaa hivyo vitumike. Wengine wanachanganya kati ya vifaa vya maabara kwaajili ya kupima Covid 19 na quick test kits za Covid 19. Kuja baadhi ya nchi wamelalamikia quick test kits LAKINI siyo vipimo vya maabara kama hiki tunachokilalamikia sisi. Sasa wewe kulalamikia kitu ambacho hakijaonesha hitilafu sehemu nyingine yoyote, unastahili kufanya scientific tests hasa, na hizi za kuoima mafenesi na kwale wakati mtengenezaji hajaeleza kama kifaa hicho kinaweza kupima hivyo vitu.
Huwezi kwenda kuilaumu WHO kwa namna alivyofanya Rais wetu. Kulistahili kufanyika detailed scientific studies kuweza kuzidisqualify idara za WHO zilizoidhinisha kutumika kwa vifaa hivi.
The whole approach to this matter has been disgracefully wrong. Mwisho wa yote ni aibu kwa Rais wetu na kwa Taifa kwa ujumla.
Sent using Jamii Forums mobile app
Umetukosea si mawazo ya Tanzania wengi hata ukifanyq utafitiDuh! Nilijua tu hili sakata we would be the losers! Hii nchi inaonesha ya vilaza kweli kweli; kila kitu politics badala ya kuzingatia utaalamu.
Tafadhali tunaomba utujuze "waadhili" ndio akina nani!?Utakapopimwa halafu uambiwe una Corona wakati huna ndio utajua Nao jamaa wanatoa tamko hili ili wapige hela za Waadhili
Mabeberu na wafuasi wao wamechakazwa vibaya mnoHii inaitwa Aibu juu ya Aibu. Baba kavuliwa nguo hadharani Aibu tunasikia watoto.
Ahhh baba uliye juu tuepushie hiki kikombe!
Sent using Jamii Forums mobile app
Palepale chattleHuyo Dr. ameongea hayo akiwa nchi ipi
Amepoteza.mwelekeo. Anaweza kudanganya watu wa vijijini wanaopewa t-shirts, kofia n.k. Lakini kwa watu wenye uelewa amebugi!
Utadhani wao ndiyo walivitengeneza. Hivi vifaa vyetu havijulikani hata aina yake wao wanasemaje kwamba havifai??Wredawazimu tu hao kwani wao ndio walivipokea hivyo vifaa? Wanavijuaaje kama bora au la? Wajinga hao
Ccm mngewekeza kwenye technology kuliko kuwekeza kuwashughulikia wapinzani,mngetengeneza vya kwenu na sio kutumia vya mabeberuWredawazimu tu hao kwani wao ndio walivipokea hivyo vifaa? Wanavijuaaje kama bora au la? Wajinga hao
View attachment 1442908
Bodi imekataa madai hayo kuwa si ya kweli na hayana msingi wowote.
My Take
Hii ni aibu tunavuna baada ya Rais kukimbilia kwenye media wakati wangeweza kufanya consultation na wataalamu wakajiridhisha na kuja na hitimisho lisilo na shaka. Kwenye orodha ya wanaopata aibu mnitoe