CDC Africa: Vipimo vya Corona Virus vinavyotumika Tanzania vinafanya kazi vizuri

There is no way in hell COVID 19 test reagents zikapatikana ILALA AMANA halafu zikakosekana IKULU....
 

Kituo cha CDC Afrika na WHO zapingana na Tanzania kuhusu ubora wa vipimo vya corona

Virusi vya corona: Vipimo vinavyotumika kupima corona Tanzania havina hitilafu

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (CDC) kimesema kwamba vifaa vya kupimia virusi vya corona nchini Tanzania havina shida yeyote. Leo Alhamisi, Mkuu wa Afrika CDC amewaambia waandishi wa habari kuwa ofisi yake inavijua vilivyo vipimo hivyo.

"Vipimo ambavyo Tanzania inatumia tunajua kwamba vinafanyakazi vizuri," Dkt. John Nkengasong amesema hivyo katika mkutano na wanahabari wa njia ya mtandao.

Kauli hiyo ya Mkuu wa Africa CDC, inapingana na kauli ya rais wa Tanzania ambaye alisema huenda vipimo hivyo vikawa na matatizo.

Kituo hicho cha Africa CDC pamoja na wakfu wa Jack Ma, Shirika la msaada la bilionea wa China, lilisambaza vifaa hivyo, Nkengasong amesema na kuongeza kwamba vilidhinishwa na wanachojua ni kwamba vinafanya vizuri.

Kituo hicho kiko chini ya Umoja wa Afrika kina majukumu ya kuratibu mapambano dhidi ya mlipuko wa mangonjwa barani Afrika.

WHO inasema nini?
Kwa upande wake Shirika la Afya Duniani kupitia Mkuu wake wa bara la Afrika Dkt Matshidiso Moeti limesema halikubaliani na kauli ya Rais Magufuli kuwa vifaa vya kufanyia vipimo vya corona vina maambukizi ya virusi.

''Tunaamini kwamba vifaa vya kufanyia vipimo vilivyotolewa vinazingatia ubora wa kimataifa na zimenunuliwa kupitia WHO na zile zilizotolewa kama msaada na WHO Jack Ma hazijaingiwa na virusi'' alisema Dkt. Moeti

Aliongeza kusema, '' Samahani sikubaliani na kauli ya [Rais wa Tanzania] kwamba vifaa vya kufanyia vipimo vilivyopo vina maambukizi ya virusi. Kwa kweli hatukubaliani na kauli hiyo.Rais Magufuli atilia mashaka ufanisi wa maabara, uchunguzi kufanyika.

Siku ya Jumapili, rais Magufuli alikihutubia taifa alitilia mashaka ufanisi wa vifaa vya kupima corona katika maabara kuu ya nchi hiyo.

Magufuli alieleza kuwa aliagiza sampuli za Wanyama na matunda kupewa majina ya binadamu na umri kisha kupelekwa ili zipimwe bila wataalamu wa maabara hiyo kujua na matokeo yakarudi kuwa baadhi ya sampuli hizo zimekutwa na maambukizi ya corona.

"…Lazima ugundue kuna mambo ya ajabu yanafanyika nchi hii. Ama wahusika wa maabara wamenunuliwa na mabeberu, ama hawana utaalamu jambo ambalo si kweli kwa kuwa maabara hii imetumika sana katika magonjwa mengine. Ama zile sampuli zinazoletwa maana vifaa vyote vinatoka nje, hivyo lazima kuna kitu fulani kinafanywa," alisema Magufuli.

Magufuli amesema kutokana na taarifa hizo anaamini kuna watu ambao walipewa majibu yasiyo sahihi.

"Lazima kuna watu wameambiwa positive lakini si wagonjwa wa corona, na inawezekana wengine wakafa kwa hofu."

Jambo hili linaweza kuwa ni moja ya sababu kuu ya kutotolewa kwa takwimu mpya kufikia sasa.
 
Tatizo la kuchnganya sias, sayansi na kutegemea matokeo mazuri ya kisiasa.

Mama Agela Merkel wa Ujerumani ni Physicist-Mtaalam wa Fizikia.

Lakini katika hili janga la corona amekaa mbali kabisa na kuwaachia mabingwa wa tibabu na afya wapambane na janga hili kwa kuitumia serikali ya Ujerumani.

Matokeo ni ya kuridhisha hata kuliko mataifa makubwa zaidi ya Uingereza na Marekani.
 
Shirika la afya duniani limethibitisha kuwa vifaa vinavyotumika Tanzania ndio hivyo vinatumika Afrika yote na vina ubora unaotakiwa

Taarifa kamili unaweza kusoma hapa

Africa disease centre rejects Tanzania's allegation that its coronavirus tests faulty

Je kwa huu ukimya wa kutangaza nini kinaendelea mitaani naona watu wameamua kutovaa barakoa

Story za vijiweni bila barakoa zimerudi kwa kasi

Watu hawajali tena corona mitaani,Kama kweli ipo basi kuna siku system zetu za afya zinaweza elemewa

Raia chukueni tahadhari sana ya kujilinda ,Tusirahisishe mambo
 
Sisi Watanzania tunamsikiliza rais wetu Magufuli
Wataalamu wetu wamepima sample za papai likakutwa na Corona!. Hata kama baada ya kuingiza sample ambazo sio za human, mashine ilionyesha error, halafu wapima wakatumia manual control command kutoa majibu ya uongo, bado kwetu ni the end justifies the means, hivyo maadam rais wetu kasema testing kits ni defective zinatoa majibu ya uongo, then kwetu hizo mashine kweli ni defectives!.
P
 
Sasa mbona hivi vinatoa majibu tofauti?

Jr[emoji769]
 
Rais alisema kuna mawili, yaweza kuwa ni vipimo kutokuwa sawa, au wataalamu kwa makusudi kuhujumu, bado tume haijatoa ripoti ya uchunguzi wao, hakuna mahala ambapo Rais moja kwa moja alisema vifaa ndio tatizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi mtu uhujumu vipimo ili iwe nini?!

Tuache porojo... Magufuli HATAKI taarifa zijulikane, PERIOD!!

Kila mwenye macho aliona na mwenye masikio alisikia!

Baada ya mwanzoni wizara kusua sua kutoa updates, watu wakaanza kulalamikia usiri!

In response, wizara wakaanza kutoa updates and within 2 weeks, number of cases ika-shoot from less than 50 to more than 300!

Nini kilifuata?! Magufuli akambadilisha Katibu Mkuu wa wizara huku akitoa tuhuma kwamba wizara inatangaza maambukizi mapya tu lakini kuna watu wengi wamepona lakini hawatangazi!

Tangia hapo wizara wakaufyata!!

Kule Karimjee watu wamejiendea kwenye maombi, Kassim Majaliwa na kiherehere chake akataja takwimu mpya na kutaja total cases then ni 480!!

Magufuli yule yule ambae aliibuka na kumtoa Katibu Mkuu baada ya kutangaza idadi kubwa, hapa napo cku chache baadae akaibuka na simulizi zake za matikiti maji na hapo hapo akaagiza watu wa maabara wachunguzwe!!

Ummy angefanya nini! Akalazimika kuwasimamisha kazi Watendaji!!

So, simple and clear... Magufuli hataki kusikia habari za maambukizi zinatolewa hususani kama maambukizi ni makubwa! Yaani yupo radhi kuona watu wanakufa kimya kimya kuliko kuweka mambo wazi ili watu wawe makini zaidi, na ikibidi tupate support kutoka kwa wenzetu!!

Watu tukisema huu ukweli wanatokea Wapumbavu utasikia eti tunamchukia Magufuli... Very Stupid!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…