CDF Mstaafu Mabeyo ametaka kufikisha ujumbe. Je, wananchi tumeuelewa ujumbe?

CDF Mstaafu Mabeyo ametaka kufikisha ujumbe. Je, wananchi tumeuelewa ujumbe?

Ni miaka 3 imepita tangu Rais Magufuli afariki. Ni jambo la kawaida, hasa siku ya maziko au wakati wa kutangaza kifo, kutolewa taarifa za kina za mazingira ya kifo cha marehemu, na kama pengine marehemu alitoa kauli yoyote. Haikuwa hivyo kwa Hayati Magufuli.

Wengi walipenda na walikuwa na shauku, msiba tu ulipotokea, wafahamu kwa kina aliugua lini, alifikishwa hospitali lini, jitihada zilizofanywa katika harakati za kuokoa uhai wa marehemu, mpaka kushindikana, na hatimaye kuyapokea mapenzi ya Mungu. Kukosekana kwa taarifa hizo, kumesababisha maneno mengi, ya kweli na yasiyo ya kweli.

Miaka 3 baadaye, baadhi ya taarifa za kina zimetolewa na CDF. Siamini kama taarifa hizi zimetolewa tu ili kujifurahisha, bali kuna ujumbe umetumwa kwa wananchi.

UJUMBE MUHIMU
Kuna shida kwenye katiba ya nchi. Kuna vitu havijawa sawa na kwa uwazi. Kwa maelezo ya CDF, ni kwamba ni yeye CDF ndiye aliyetoa msisitizo wa kuwa ni Makamu wa Rais ndiye anatakiwa kuwa Rais, na siyo mwingine yeyote. Tena ameeleza kuwa ni yeye CDF ndiye aliyeelekeza kuwa inabidi makamu wa Rais aapishwe kabla ya maziko ya Rais maana bila hivyo jeshi haliwezi kumtambua kama ndiye Amiri Jeshi Mkuu.

Lakini pia Rais mstaafu Kikwete, wakati Ndugai alipoondolewa kwenye nafasi ya uspika, alieleza kuwa Rais alipofatiki, spika alimwendea na kumwambia kuwa kwa mujibu wa katiba, yeye spika ndiye anatakiwa kuwa Rais. Yeye Kikwete alimkatalia.

Lakini pia zipo habari ambazo hazijawekwa wazi, huenda zikawekwa wazi siku za mbeleni, kuwa wale waliokuwa wakipinga Makamu kuchukua nafasi ya Urais baada ya kifo cha Rais, walieleza kuwa katiba inasema kuwa Rais akitoka bara, makamu atatoka visiwani. Na kwa vile aliyefariki alikuwa anatoka bara, urais ulikuwa nafasi ya bara, nafasi ya visiwani ilikuwa ni umakamu, hivyo makamu aendelee kuwa makamu.

HATARI ILIYOPO
Tusistegemee nyakati zote tutakuwa na CDF wa aina ya Mabeyo. **** siku tutakuja kuwa na CDF mwoga wa kutoa maamuzi na wanadiasa wakatii, au tukawa na CDF mwenye tamaa ya madaraka, anaweza kutumia nafasi ya kukosekana maelewano miongoni mwa wanasiasa, akayanyakua madaraka yeye CDF.

HITIMISHO
Tumepewa ujumbe ambao ni angalizo, kuwa tunatakiwa kuiweka sawa katiba ili kila jambo liwe wazi kwenye katiba, na katiba izibe mianya yote ya tafsiri zisizokusudiwa.

Mapungufu yetu ya katiba hayapo tu pale ambapo Rais atafariki akiwa madarakani, yapo maeneo mengi. Tangu enzi za Tume ya Jaji Nyalali, mapungufu ya katiba yamekuwa yakiainishwa, lakini wafanya maamuzi wamekuwa magumegume, wanafanya mabadiliko madogo madogo kwenye maeneo yale tu wanayoona yanawahakikishia kubakia madarakani hata bila ya matakwa ya umma.

Hata Samia ambaye nusura asiwe Rais kwa sababu ya sintofahamu za katiba, baada ya kuipata Urais, hataki katiba mpya kwa vile anaona iliyopo inamhakikisha mamlaka ya kuwa hata dikteta akitaka, bila ya kubughudhiwa. Amesahau kuwa bila ya hekima ya CDF huenda asingekuwa Rais. Manufaa yake binafsi yamefifisha hekima yake katika kuyaangalia maslahi ya Taifa.

Ni lini tutampata Rais mzalendo anayelitazama zaidi Taifa kuliko madaraka yake binafsi na manufaa ya chama chake? Kuwa na hawa viongozi wanaojali zaidi madaraka kuliko madlahi ya Taifa, kuna siku nchi itakwenda kwa namna isiyotarajiwa. Pongezi kwa CDF kwa kujali maslahi ya Taifa.
Paragraph hizi mbili za mwisho ni muhimu sana sana zizingatiwe sana kama wapo bado watu wenye akili nzuri na wanaoitakia mema Nchi hii nzuri iitwayo Tanzania 🇹🇿 !

Vinginevyo ipo siku mtu ataokota Dodo chini ya muarobaini and that will be that !
Katiba mpya bora ni muhimu kuliko kitu chochote kwa wakati huu before it’s too late ⏰ time is running out !!
 
CDF alitukosea heshima sn tulipaswa kufanya uchaguzi
Uchaguzi mlishafanya 2020 mkamchagua Samia kuwa ndiye Rais wa backup (Makamu wa Rais) na Rais Magufuli akifa muda wowote Samia amrithi bila uchaguzi mwingine.

Au mlifikiri Makamu wa Rais ni muimba hooks wa mapambo tu?

Ndiyo concept nzima ya kuwa na "running mate" na kuipigia kura tiketi ya CCM ya "John Pombe Magufuli/ Samia Suluhu Hassan".

Pale hakupigiwa kura Magufuli, ilipigiwa kura tiketi ya CCM ya Magufuli na Samia. Walipewa mandate ya kutawala ya miaka mitano.

Urais ni taasisi, si mtu.

Usicjoelewa ni kipi hapo?
 
Magufuli alikosea kumchagua Samia Kama mgombea mwenza.
 
Hapo alitakiwa mtu strong sn
 
Magufuli alikosea kumchagua Samia Kama mgombea mwenza.
Wale wagombea huwa mara nyingi hawachagui wagombea wenza, huwa wanabambikiwa na chama.

Ukimsikiliza Makonda alivyosema katika vile vikao vya kuzungumzia katiba mpya, ni kama alisema kuwa "Watch this Samia woman, you are going to hear her name a lot".

Alinikumbusha mwaka 1984 kuna Uncle wangu mmoja alikuwa Usalama wa Taifa aliniambia kuwa huyu Mwinyi atakuja kuwa rais wa Tanzania.

Kwa hivyo Samia alikuwa anaandaliwa tangu awali, kabla Magufuli hajapata kuwa mgombea wa urais, watu walishampanga Samia kuwa mgombea mwenza.

Na huu ujinga wa kubambika watu wasioendana kwenye tiketi moja umeleta matatizo sana. Kwa sababu tumepata rais ambaye haendani na Makamu wa Rais, wamelundikwa pamoja tu.

Matokeo yake ndiyo hizi habari alizotuambia Makamba kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais ilitengwa mpaka salamu watu walikuwa hawapewi.

Ni hatari sana Rais na Makamu wake kufanya kazi bila ushirikiano wa karibu. Kuna mambo mengi sana yanaweza kuharibika vibaya sana.
 
Hapo alitakiwa mtu strong sn
Ndiyo mjifunze sasa kwamba Makamu wa Rais si pambo tu.

Siyo mtu wa kukata utepe kufungua miradi ya serikali, kuhudhuria sherehe na kupigia kelele habari za muungano na mazingira tu.

Ukimuweka mtu kuwa mgombea mwenza na Makamu wa Rais, umempitisha kuwa Rais muda wowote Rais akifariki.

Yani nchi inaweza kuwa kwenye vita, Rais akafariki, halafu huyo Makamu wa Rais akawa Rais na Amiri Jeshi Mkuu aongoze vita.

Imagine Vita vya Kagera tunapigana na Nduli Idi Amin Dada halafu Rais wetu Samia !
 
Mkuu hatutarudia hili tulifanya kosa kubwa sn tunajuta
 
Back
Top Bottom