Cecil Mwambe ashindwa vibaya uchaguzi Kanda ya Kusini

Cecil Mwambe ashindwa vibaya uchaguzi Kanda ya Kusini

Makapi yadhibitiwe kwa ili nipo na chadema 100% sio kufanya uchaguzi leo mwakani mtu anaunga mkono juhudi ili halikubaliki hata kidogo makapi yachujwe yote.

Vipi walioshinda hawataunga mkono juhudi? Mimi naona wanajiongezea tu thamani, wote ni hao hao! Wasakatonge.
 
Bahati nziuri natumia akili kufikiri situmii utumbo kuniambia nisubiri 2020 nikudhani natumia utumbo kuwaza kama ww nani kakwambia 2020 kuna uchaguzi
utaelewa baada ya uchaguzi wa 2020 kwamba aliyeiua CHADEMA ni Mbowe na alifanya hivyo mwaka 2015 makusudi Kabisa.
Ninamashaka pia kama huyu Mbowe sio Mrema namba 2.
Uzuri wa waTanzania kufikiri huwa tunaahirisha na tunasahau haraka.
 
Ni kweli wanatakiwa kwenye Chama, maana Chama makini kitamhitaji kila mtu. Tatizo ni tabia za wanasiasa uchwara wa Tanzania na siasa zao za kutaka kukomoa. Yaani mtu anashindwa kihalali katika sanduku la kura, bado mtu huyo analaumu na kumtupia lawama mtu mwingine asiyehusika huku moyoni ana nia ya kuhama ili kuwakomoa!!!
Ndipo nikasema waende tu kama ndiyo lengo lao.

Mkuu uko sahihi, eti mtu anataka kushinda tu, akishindwa anataka abembelezwe kwa kitisho eti atahamia ccm. Mtu wa hivyo awahi huko ccm haraka sana bila kubembelezwa.
 
Wafundishe hayo masokwe. Hayajui nini maana ya ushindani. Katika demokrasia ni kitu cha kawaida kabisa kushindwa au kushinda. Lakini wao wana mfanya mpinzani ni adui.

Nawaona hata viongozi wao wa kitaifa nao wako hivyo hivyo. Wakishindwa wanakuwa na kisirani. Wanaanza kutukana ovyo ma kujaribu kutafuta kila mbinu ili kuleta machafuko. Aisee! Hawa watu washukuru kwamba watanzania wana huruma.

Namshangaa kwa mfano mtu kama Tundu Lissu, anathubutu hata kumchukia Boss wake Speaker wa Bunge letu tukufu Mh. Ndugai. Ni mtu ovyo sana. Halafu anategemea Speaker amchekee tu na kumpenda yeye? Kama yeye hataki kuthamini na kutambua nyazifa za wengine, kwanini na wao wasimdharau vile vile?

Sijawahi kuona mbunge aliyekosa uzalendo kwa nchi yake na viongozi wake kama Tundu Lissu. Mbunge na mwana sheria mwenye akili timamu asinge wezaji panda ndege na kusafiri mpaka Washington DC, Amerika ili kuwapakazia uongo Rais wa nchi yake na Kiongozi wa Bunge lake badala ya kurudi mara moja kwao na kukutana na Boss wake ili kumaliza tofauti walizo kuwa nazo.

Mtu kama huyo eti bado ana taka awe kiongozi na jemedari mkuu wa nchi. Itawezekana kweli? Hicho ni kichekesho kikubwa sana.
Wakati mwingine ujitahidi kuficha ujinga wako walau ubakie na heshima kidogo. Subiria baba yako apigwe risasi halafu wewe kacheke na ndugai.
 
Nawapongeza walioshinda lkn Zaidi kwa Kaka angu Mario Milinga kuwa mweka hazina
 
Huo utetezi wa kwamba cdm inamuhitaji sana Mbowe wakati huu hata hauniingii akilini, akifa kesho basi jumanne asubuhi chama kinakufa? Siko na ccm kabisa kuhusu nafasi ya Mbowe, huenda ccm wanataka Mbowe aondoke kwa sababu zao, na mimi nina sababu zangu hata kama wote tumetaka hilo sasa. Mbowe ajilaumu mwenyewe kushindwa kuandaa succesion plan, kwani alipaswa kujua hiyo ni taasisi. Chama kinachomtegemea mtu mmoja kuwaongoza na sio mifumo ya uongozi, hicho sio chama bali kundi la wajanja linalofanya siasa. Naamini kwenye cdm taasisi na sio kwa cdm mtu.
Ndugu yangu tindo, usijitoe akiri , Mimi ninakanuni moja mtu yeyote anayekataliwa na ccm jua yuko vizuri sana kichwani .
 
Back
Top Bottom