Cecil Mwambe ashindwa vibaya uchaguzi Kanda ya Kusini

Cecil Mwambe ashindwa vibaya uchaguzi Kanda ya Kusini

Alipaswa kuacha nafsi hiyo wazi kwa mwanacdm halisi. Nijuavyo mimi watu hushawishiwa kuchukua nafasi, na watu hao wapo ndani ya cdm. 2010 Slaa hakuwa amejiandaa kugombea urais, bali alishawishiwa. Hata sasa hilo lilipaswa kufanyika.
Swala LA kuacha ni haki yake, pia kutoacha ni haki yake.cha msingi anayetaka kumpinga achukue fomu wanachadema wataamua wanamtaka nani.angalau kwa hili niwapongeze chadema, kuliko ccm nafasi ya mwenyekiti marufuku mwingine kuchukua fomu.
 
Wangalau hizo kura zihesabiwe hadharani, japo hata iwe vipi kiongozi kukaa madarakani zaidi ya miaka 15 kwangu hainiingii akilini. Tena ikibidi hao viongizi watakaogombea wawe sehemu ya wahesabu kura. Kinyume na hapo kwangu huo uchaguzi ni igizo kama maigizo mengine.

Nimewapongeza sana cdm pale walipopiga kura za ndio na hapana kwa mgombea mmoja. Pale wamefanya demokrasia ya hali ya juu. Na sasa nataka hizo kura za mwenyekiti zihesabiwe hadharani tena wagombea wengine wakiwa sehemu ya kuhesabu kura hizo. Tunahitaji cdm wawe mfano wa kuheshimu box la kura na hata nchi nzima ijue hilo.
 
Kama huyo Mwambe ameshindwa hiyo ni habari nzuri sana, sina imani na mtu yoyote toka ccm kupata nafasi yoyote ndani ya cdm. Bado Nyalandu, hao wanaccm 95%+ ndio waliorudi kuunga mkono juhudi, huu uchaguzi umenifurahisha sana. Ila doa langu kubwa ni kwa Mbowe kuendelea kulazimisha kuwa mwenyekiti wa cdm. Katika hilo simuelewi Mbowe wala siawaelewi kabisa cdm. Ifahamike cdm ni taasisi, iweje mtu mmoja akae madarakani zaidi ya miaka 15?
Mkuu kwa vile katiba yao haina ukomo MTU kugombea uongozi sio mbaya, cha msingi ashindanishwe Na wengine.akishinda aendelee.sio ccm mwenyekiti hapingwi...
 
Mkuu kwa vile katiba yao haina ukomo MTU kugombea uongozi sio mbaya, cha msingi ashindanishwe Na wengine.akishinda aendelee.sio ccm mwenyekiti hapingwi...

Unajua ni kipi kilifanya hicho kifungu cha ukomo kisiwepo? Sikosei ninaposema muda wa Mbowe kukaa madarakani umepita. Uliza upate ukweli kwanini hicho kifungu cha ukomo hakipo. Kwa taarifa yako hicho kifungu kilitolewa kinyemela bila ridhaa ya vikao halali. Amka boss, usitoe nafasi ya siasa chafu kuendelea cdm.
 
Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba Mwenyekiti wa Kanda ya Kusini Chadema Cecil Mwambe ameshindwa kutetea nafasi yake baada ya kuangushwa vinaya na mpinzani wake Suleiman Mathew.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imekwenda kwa Salum Baruhan ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Lindi mjini kupitia CUF

Kushindwa kutetea nafasi yake kwa Cecil Mwambe ambaye pia ni mgombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa inaonyesha ni salaam maalum za wanachadema kwake kuelekea uchaguzi mkuu wa chama hicho Desemba 18
Sasa kama uenyeikiti wa kanda kadondokea pua,je taifa si atadondokea "KALIO"?
 
Kukaa miaka 15 sio hoja, hoja akubalike Na watu.wako wabunge wamekaa zaidi ya vipindi vitano bungeni.cha msingi washindanishwe Na watu.

Mkuu hata wabunge kwenye katiba pendekezwa tuligoma wao kukaa zaidi ya miaka kumi, tena tulienda mbali zaidi kuwa iwapo mbunge atashindwa kutekeleza wajibu wake, apigwe chini hata kabla ya muda wake wa miaka mitano kuisha. Ila maoni yale yakachakachuliwa. Ni hivi kaka, kiongozi kukaa madarakani zaidi ya miaka kumi ni uhuni kama uhuni mwingine. Hapa haijalishi Utetezi wowote ule. Na mara nyingi kiongozi yoyote akikaa zaidi ya miaka kumi huanza kuchezea box la kura na figisu zisizo na aibu.
 
Nimeamini kweli kuwa yeyote atakaye jaribu na aliyejaribu kuchukua fomu ya kugombea uwenyekiti taifa kuna figisu lazima afanyiwe.
Na naamini yale maneno ya sumaye kuwa sababu ni kutangaza nia ya kugombea kiti ndio maana kura za hapana zilimiminika kama njugu.
Kwahiyo ndugu zangu yeyote atakayejaribu kusimama na mbowe ni pandikizi si ndio?
Aya bhana uwanja ni wenu pambaneni.
KUNA KITU KINAITWA safisha gala Ndo tunamalizia
 
..cdm mnatakiwa mvumiliane.

..ushindani ktk uchaguzi isichukuliwe kuwa ni uadui.

..siyo vibaya kushangilia ushindi, lakini pia mhakikishe wale wanaoshindwa mnawa-embrace na kuwatia moyo.
Wafundishe hayo masokwe. Hayajui nini maana ya ushindani. Katika demokrasia ni kitu cha kawaida kabisa kushindwa au kushinda. Lakini wao wana mfanya mpinzani ni adui.

Nawaona hata viongozi wao wa kitaifa nao wako hivyo hivyo. Wakishindwa wanakuwa na kisirani. Wanaanza kutukana ovyo ma kujaribu kutafuta kila mbinu ili kuleta machafuko. Aisee! Hawa watu washukuru kwamba watanzania wana huruma.

Namshangaa kwa mfano mtu kama Tundu Lissu, anathubutu hata kumchukia Boss wake Speaker wa Bunge letu tukufu Mh. Ndugai. Ni mtu ovyo sana. Halafu anategemea Speaker amchekee tu na kumpenda yeye? Kama yeye hataki kuthamini na kutambua nyazifa za wengine, kwanini na wao wasimdharau vile vile?

Sijawahi kuona mbunge aliyekosa uzalendo kwa nchi yake na viongozi wake kama Tundu Lissu. Mbunge na mwana sheria mwenye akili timamu asinge wezaji panda ndege na kusafiri mpaka Washington DC, Amerika ili kuwapakazia uongo Rais wa nchi yake na Kiongozi wa Bunge lake badala ya kurudi mara moja kwao na kukutana na Boss wake ili kumaliza tofauti walizo kuwa nazo.

Mtu kama huyo eti bado ana taka awe kiongozi na jemedari mkuu wa nchi. Itawezekana kweli? Hicho ni kichekesho kikubwa sana.
 
Lugha za kuitwa wasaliti sio saws, wanatimiza haki yao ya kikatiba.
Hakuna aliyemwita mtu msaliti, lakini aina ya tweet ya Sumaye ina walakini mkubwa Sana. Yaani anagombea huku akijua atashindwa, halafu amlaumu nani!!?

Hivi katika hali ambayo wahamiaji kutoka CCM wanarudi wakidai ni nyumbani ni mwanachadema yupi atamwamini mhamiaji kumpa nafasi ya juu ya chama Taifa hasa uenyekiti!!?
 
Wafundishe hayo masokwe. Hayajui nini maana ya ushindani. Katika demokrasia ni kitu cha kawaida kabisa kushindwa au kushinda. Lakini wao wana mfanya mpinzani ni adui.

Nawaona hata viongozi wao wa kitaifa nao wako hivyo hivyo. Wakishindwa wanakuwa na kisirani. Wanaanza kutukana ovyo ma kujaribu kutafuta kila mbinu ili kuleta machafuko. Aisee! Hawa watu washukuru kwamba watanzania wana huruma.

Namshangaa kwa mfano mtu kama Tundu Lissu, anathubutu hata kumchukia Boss wake Speaker wa Bunge letu tukufu Mh. Ndugai. Ni mtu ovyo sana. Halafu anategemea Speaker amchekee tu na kumpenda yeye? Kama yeye hataki kuthamini na kutambua nyazifa za wengine, kwanini na wao wasimdharau vile vile?

Sijawahi kuona mbunge aliyekosa uzalendo kwa nchi yake na viongozi wake kama Tundu Lissu. Mbunge na mwana sheria mwenye akili timamu asinge wezaji panda ndege na kusafiri mpaka Washington DC, Amerika ili kuwapakazia uongo Rais wa nchi yake na Kiongozi wa Bunge lake badala ya kurudi mara moja kwao na kukutana na Boss wake ili kumaliza tofauti walizo kuwa nazo.

Mtu kama huyo eti bado ana taka awe kiongozi na jemedari mkuu wa nchi. Itawezekana kweli? Hicho ni kichekesho kikubwa sana.
Yote uliyosema Ni sifuri Kama hao unaowatetea hawatasema Lisu alipigwa risasi na nani!!!? Uwezo huo wanao, waambie watuambie, vinginevyo utakuwa unabwabwaja ujinga kutetea upuuzi wa akina Ndogaye!!!
 
Nimewapongeza sana cdm pale walipopiga kura za ndio na hapana kwa mgombea mmoja. Pale wamefanya demokrasia ya hali ya juu. Na sasa nataka hizo kura za mwenyekiti zihesabiwe hadharani tena wagombea wengine wakiwa sehemu ya kuhesabu kura hizo. Tunahitaji cdm wawe mfano wa kuheshimu box la kura na hata nchi nzima ijue hilo.
Ungesimamia hoja hii, hata mimi ningekuunga mkono bila kusita.

Hiyo ya miaka 15 ni 'dhana' tu na wala sio 'nadharia'.

Sasa tuwasisitizie CHADEMA wahakikishe uchaguzi uwe wa haki, kura zote zihesabiwe kwa utaratibu utakaohakikisha mizengwe haikufanyika.
Atakayeibuka mshindi apewe ushirikiano na visizuke tena visababu vingine pembeni.
 
Haya! Kuna 'Kushindwa kawaida', 'Kushindwa vibaya' na pia kuna 'Kushindwa vizuri'.

Sawa!
 
Watiwe moyo upi. Kwani hawajui katika ushindani Kuna kushinda na kushindwa!!? Kama vipi waishie, Chadema ni imara kama Simba.

..kweli.

..walioshindwa uchaguzi haimaanishi kwamba hawahitajiki tena ndani ya chama.

..Mzee Mkapa aliwahi kushindwa nadhani ujumbe wa nec ccm. Aliokolewa na kura za " kikapu." Baadaye amekuja kuwa Mwenyekiti wa ccm.

..Mzee JK naye alishindwa kura za kupeperusha bendera ya ccm 1995. Miaka 10 baadaye akaja kuwa Mwenyekiti wa ccm.

..Kushindwa uchaguzi maana yake ni kuwa "kura hazikutosha", haimaanishi kwamba mhusika hatakiwi ndani ya chama.
 
Back
Top Bottom