Cecil Mwambe ashindwa vibaya uchaguzi Kanda ya Kusini

Cecil Mwambe ashindwa vibaya uchaguzi Kanda ya Kusini

Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba Mwenyekiti wa Kanda ya Kusini Chadema Cecil Mwambe ameshindwa kutetea nafasi yake baada ya kuangushwa vinaya na mpinzani wake Suleiman Mathew.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imekwenda kwa Salum Baruhan ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Lindi mjini kupitia CUF

Kushindwa kutetea nafasi yake kwa Cecil Mwambe ambaye pia ni mgombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa inaonyesha ni salaam maalum za wanachadema kwake kuelekea uchaguzi mkuu wa chama hicho Desemba 18
Unaweka mno ushabiki. Hata kama hamumtaki sio lazima mseme. Hamkisaidii hiki chama badala yake mnazidisha makundi na kuzidisha uhasama. Kama mna watu wenu mngewateua tu kama wenyeviti wa mtaa wa ccm ijulikane moja
 
..cdm mnatakiwa mvumiliane.

..ushindani ktk uchaguzi isichukuliwe kuwa ni uadui.

..siyo vibaya kushangilia ushindi, lakini pia
mhakikishe wale wanaoshindwa mnawa-embrace na kuwatia moyo.
Naunga mkono hoja , kushindwa ni sehemu ya demokrasia hatuna haja ya kuwakejeli walioshindwa hata kama hatukuwaunga mkono
 
Attachments

  • Screenshot_20191130-170435_Instagram.jpg
    Screenshot_20191130-170435_Instagram.jpg
    150.3 KB · Views: 1
Huyu mwambe in pandikizi LA Magufuli.
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema ukiishaanza kula nyama ya binadamu huwezi kuacha. Kila mtu Chadema mwenye mawazo tofauti ni pansikizi. Ni mamluki. Tabia hiyo ya kuitwa hivyo siku moja itamkuta Lema, itamkuta Msigwa, itamkuta Heche, itamkuta Mnyika, itamkuta Mbowe na itakukuta hata wewe Retired! And that will be the end of Chadema.
 
Kama makapi unamaanisha waliotoka CCM, hata huyo Mathew alitoka huko.
Maskini ya Mungu dogo hajui hilo. Labda umfahamishe kuwa mpaka mwaka 2015, Selemani Mathew alikuwa diwani wa CCM katika moja ya kata za Kigamboni, Dar es Salaam. Kisha akaenda kugombea ubunge Mtama kupitia CCM akashindwa na Mh. Nape. Ndipo akaenda Chadema.
 
Nimeamini kweli kuwa yeyote atakaye jaribu na aliyejaribu kuchukua fomu ya kugombea uwenyekiti taifa kuna figisu lazima afanyiwe.
Na naamini yale maneno ya sumaye kuwa sababu ni kutangaza nia ya kugombea kiti ndio maana kura za hapana zilimiminika kama njugu.
Kwahiyo ndugu zangu yeyote atakayejaribu kusimama na mbowe ni pandikizi si ndio?
Aya bhana uwanja ni wenu pambaneni.
Panapo majaliwa tunasubiri pia kuona hapo mwakani Membe atakapochukua form kugombea nafasi ya kuteuliwa kugombea urais huko kwenu itakuwaje.
We shall see what will happen.
 
Ndo demokrasia huo. kwanini wengine wanahisi kila anatetea nafasi akiangushwa basi ni hujuma. Acheni demokrasia ifanye kazi yake.
Kweli kabisa ndg yangu TsafuRD.

Nashindwa kuelewa watu walitaka wagombea watoke droo au vp, kama ni kugombea uenyekiti Taifa kwani mpaka ushinde ngazi ya kanda? Lo kazi ipo mwaka huu.
 
Kama huyo Mwambe ameshindwa hiyo ni habari nzuri sana, sina imani na mtu yoyote toka ccm kupata nafasi yoyote ndani ya cdm. Bado Nyalandu, hao wanaccm 95%+ ndio waliorudi kuunga mkono juhudi, huu uchaguzi umenifurahisha sana. Ila doa langu kubwa ni kwa Mbowe kuendelea kulazimisha kuwa mwenyekiti wa cdm. Katika hilo simuelewi Mbowe wala siawaelewi kabisa cdm. Ifahamike cdm ni taasisi, iweje mtu mmoja akae madarakani zaidi ya miaka 15?
 
Tafsiri ya wasaliti kulingana na Kamusi ya Chadema;

Msaliti= " Mwanachama yeyote anayetaka kuchukua nafasi ya Mbowe kama mwenyekiti"
 
Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba Mwenyekiti wa Kanda ya Kusini Chadema Cecil Mwambe ameshindwa kutetea nafasi yake baada ya kuangushwa vinaya na mpinzani wake Suleiman Mathew.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imekwenda kwa Salum Baruhan ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Lindi mjini kupitia CUF

Kushindwa kutetea nafasi yake kwa Cecil Mwambe ambaye pia ni mgombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa inaonyesha ni salaam maalum za wanachadema kwake kuelekea uchaguzi mkuu wa chama hicho Desemba 18
Apishe huko mamluki MKUBWA huyo! Naamini ataenda CCM muda wowote!
 
Kwa mazingira ya sasa bado Mbowe anahitajika cdm kuliko wakati wote hebu siumesikia Lisu anakuwa Makamu mwenyekiti ni maandalizi ya Mbowe kuachia uenyekiti Ila kwa sasa nakushauri usijiingize kwenye porojo za lumumba kumbuka chama cha upinzani kilichobaki kwa sasa ni cdm na Mbowe ndio kisiki hebu niambie leo hii kama si Mbowe labda angekuwa Mwenyekiti Zitto...au Slaa..au Arfi nipe muono wako wa chama kingekuwaje! chama kimejemgwa kwa gharama kubwa haitakiwi kiumizwe eti sababu Mbowe Mwenyekiti wa muda mrefu! ujinga huo wauseme ccm wanasababu zao wamekoa bei ya Mbowe lkn Sisi tunaoangalia siasa za sasa zinavyokwenda Mbowe natakiwa abaki kuhakikisha wakina Lisu wanakamati Uongozi watu ambao chama ndio kimekuwa msaada kwao sio hao waliokuja na mafuriko! thank twice brother

Back
Top Bottom