Huo utetezi wa kwamba cdm inamuhitaji sana Mbowe wakati huu hata hauniingii akilini, akifa kesho basi jumanne asubuhi chama kinakufa? Siko na ccm kabisa kuhusu nafasi ya Mbowe, huenda ccm wanataka Mbowe aondoke kwa sababu zao, na mimi nina sababu zangu hata kama wote tumetaka hilo sasa. Mbowe ajilaumu mwenyewe kushindwa kuandaa succesion plan, kwani alipaswa kujua hiyo ni taasisi. Chama kinachomtegemea mtu mmoja kuwaongoza na sio mifumo ya uongozi, hicho sio chama bali kundi la wajanja linalofanya siasa. Naamini kwenye cdm taasisi na sio kwa cdm mtu.