Mwezi April mwishoni nilikua seminar ya wiki pale Serena. Ndio wiki wakina wema,mwijaku,steve Nyerere na wasanii wengine walikua na press conference ya royal tour so wasanii kibao hadi nisiowajua majina ila sura nazifaham. Baada ya siku mbili wakaja watu wengine mashuhuri kwenye uzinduzi wa kitabu cha jaji mkuu mstaafu wa Kenya..so kina prof shivji,membe,fatma karume a.k.a shangazi,nk. Afu jioni kila siku makampuni makubwa kila siku yakawa yanafuturisha so wakina jenista mhagama na mawaziri wengine kibao na ma CEO tukawa tunameet nao dinner. Wakina AY na wasanii wengine kibao hawakukatika ile wiki. Watu wa kutoka mikoani walikua wanashangaa sana kuwaona watu wanaowaonaga tu kwa TV. Ila wengi ni kweli uhalisi wa muonekano wao ni tofauti kabisa hasa wasanii..wanasiasa si sana. Ila shangazi ni kifaa nyie na uzee wake ule mtu bado unamtamani