Chad: Rais Idriss Déby afariki dunia saa chache baada ya kutangazwa mshindi wa Urais kwa muhula wa sita

Chad: Rais Idriss Déby afariki dunia saa chache baada ya kutangazwa mshindi wa Urais kwa muhula wa sita

Breaking news:Rais Idriss Deby wa Chad aliyeshinda uchaguzi mkuu nchini huko ndani ya masaa machache baada ya kutangazwa Amefariki dunia muda mfupi uliopita.,redio nchini huko kupitia jeshi zimetangaza
Duu!
 
Wacha apumzike tu huyo mzee alikuwa rais wa maisha, utake usitake.
 
Breaking news:Rais Idriss Deby wa Chad aliyeshinda uchaguzi mkuu nchini huko ndani ya masaa machache baada ya kutangazwa Amefariki dunia muda mfupi uliopita.,redio nchini huko kupitia jeshi zimetangaza
Hii dose Mungu aliyoileta iendelee hadi kwa akina Museveni, Paul Biya, Ali Bongo na Paul Kagame.

Tumeona Magufuli aliiba kura October 2020 lakini akafa baada ya siku 114. Mungu hachezewi!!
 
Alijifanya kwenda mstari wa mbele kupigana na waasi. Alikuwa anaanza ngwe ya 6 kuongoza. Yaani tangu 1990 yupo tu na alikuwa hataki kumwachia mtu mwingine.
Ukisikia kuchokwa mpaka na roho yako mwenyewe ndio huko sasa. Kizee cha miaka 68 ukajifanye Rambo kama sio kutaka kufa ni nini. Bado kina Museveni nao wanaojiona makomando mpaka uzeeni.
 
Back
Top Bottom