PreGE2025 CHADEMA; baada ya tamko la kutoshiriki Uchaguzi Mkuu, fanyeni haya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kwanza mimi sio chadema na wala sishabikii upumbavu unaoitwa chama cha siasa nilicho andika mimi ni ukweli kua adui wa Tanzania ni ccm na watu wake, kila mwenye akili timamu analijua hilo
 
Sid
sidhani kama kuna mtu atakaa kusoma hilo gazeti lako, inshort chadema wanapambania ni free and fair election na sio hayo ulioyaandika humo. Kama CCM wataweza kuweka usawa kwenye chaguzi wakashinda basi ni haki watawale mpaka watanzania waseme po!
 
Wewe ni chawa hii spinning unavyofanya haiwezi kuwatoa kwenye mtazamo wenye akili,mamilioni ya Watanzania wametuelewa na hatugeuki nyuma, tunakupuuza. Wameshindwa wenye bunduki na mabomu utaweza wewe,don't waste your breath we are not buying your product.
 
Siku mtakayoukubali ukweli kuhusu nyinyi wenyewe, ili mbadililike nyinyi kwanza vyama vya upinzani hususan CHADEMA; ndiyo siku ambayo magumu mnayopitia sasa hamtayaona tena.
Ww huset standards za chama Cha upinzani kiweje..Baki na ideologies zako za KiCCM..sio lazima zifatwe na vyama vyote vya siasa.
 
Kwanza mimi sio chadema na wala sishabikii upumbavu unaoitwa chama cha siasa nilicho andika mimi ni ukweli kua adui wa Tanzania ni ccm na watu wake, kila mwenye akili timamu analijua hilo
Haijalishi adui wa taifa hili awe ni CCM, CHADEMA au chama chochote kile mimi sijui na sitaki kujua kuhusu hilo, wananchi tunasema hivi, tumechoka na hatuzitaki siasa zenu za maneno tunataka siasa za Vitendo tena VITENDO CHANYA nukta.
 
Kikubwa ujumbe ufike kata kwa kufanya skimming and scanning.

Sawa wanapambania free and fair election, swali ni je! Wanapambania wapi? huku mitandaoni na mitaani si mahali sahihi pa kufanya mapambano hayo, heri wangekubali kushiriki uchaguzi wakapambanie hili bungeni ambako ndiko mahali sahihi pa hicho wanachokipambania.
 
Mimi si chawa, sijawahi kuwa chawa na sina mpango wa kuwa chawa. Mimi ni Mtanzania; mwananchi niliyechoshwa na siasa zozote zile zenye maneno mengi, lugha chafu, kashfa, matusi, kuvunjiana heshima na zisizo na tija kwa wananchi. Napenda kuona siasa za kimya kimya zenye VITENDO CHANYA zaidi nchini Tanzania kwa manufaa ya Watanzania.
 
Ww huset standards za chama Cha upinzani kiweje..Baki na ideologies zako za KiCCM..sio lazima zifatwe na vyama vyote vya siasa.
Una uhakika vyama vya upinzani nchini Tanzania viko 100% perfect?
 
Hizi nadharia zako akizikia mtu asiyejua ukweli ataamini. Ni mara moja au 2 cdm wametaka kupeleka huduma kwa jamii na wanakaliwa? Ni mara ngapi cdm walitaka kufanya miradi kwenye halmashauri wanakataliwa na wakurugenzi kwa kuwaambia ilani inayotekelezwa ni ya ccm na sio ya cdm. Mfano halisi, mwaka 2011 cdm walitaka kutoa elimu bure kwa shule za msingi katika manispaa ya moshi, mkurugenzi akakataa kwa kusema haiko kwenye ilani ya ccm?

Baada ya uchaguzi wa 2015, cdm walipata halmashauri nyingi, Magufuli kwa ajili ya wivu wa kisiasa akasema pesa zote zikusanywe na TRA, kisha ziingie hazina na halmashauri ziombe fedha za matumizi huko. Sio mara moja au 2 wakuu wa hospitali ama shule hukwepa kupokea misaada ya wanacdm, na kusema ni maagizo toka juu?
 
Ile lugha ya Makala kuwa cdm wamepanga kuingiza m-pox ama ebola unaichukuliaje, au kwako busara na lugha mbaya zina macho? Hujafanya utafiti wa tabia za ccm, lakini una bandiko refu la mapungufu ya cdm na nini wanatakiwa wafanye. Hili bandiko lako linaonekana ni la mtu aliye nje ya nchi, na uandishi wako umejikita kwenye nadharia na sio uhalisia. Siku ukirudi hapa nchini uje uangalie uhalisia ndio uandike utafiti wako wenye mahaba ya ccm.
 
Hapa naomba nisaidie; huenda wao CHADEMA walitaka wapeleke huduma kwa jamii kama serikali (hili linaweza kuleta changamoto kweli) lakini kuna alternative ya kupeleka huduma kwa jamii kama taasisi binafsi; na hapa ndiyo maana unaona makanisa na misikiti inamiliki shule, vyuo, hospitali, benki na taasisi nyingine za kijamii pasipo kuingiliana wala migogoro na serikali.
 
Unajua unachoongea au nibaki kwenye hilo neno lako huenda? Kama hujafanya utafiti ni bora kukaa kimya, ama andika kama mshabiki wa ccm. Taasisi za dini zina madhara gani kwa madaraka ya ccm. Hebu kaa kimya ndugu maana una nadharia zisizo na uhalisia.
 
Ndugu yangu, mimi nimesema vyama vyote nchini Tanzania tumechoka kusikia vikitukanana, kukashfiana, kusemana vibaya, kunyukana, kuvinjiana heshima, n.k. tunahitaji siasa za VITENDO CHANYA. Kiukweli kabisa hii ni kwa wote; CCM, CHADEMA, ACT na vyama vingine vilivyosalia.
 
Mwandishi yuko sahihi;

Hilo tatizo la uchaguzi ni dogo sana; mfano upinzani unaweza ukasimamisha watu mahiri majimboni ambao wanauzika bila hata kuhitaji msaada wa chama? CCM wamefanikiwa hapo, kwanza wana chama imara lakini wana watu wanaouzika kwenye jamii. Mfano pale Kahama unadhani ni rahisi sana kumshinda Kishimba??? Ni kama ilivyokuwa ile moshi ya Ndesamburo (ukiacha xhama chake lakini Ndesa alikuwa system imara sana na alifanya mambo mengi kwa watu wote CCM na CDM kiasi kwamba kumshinda ilikuwa next to impossible ) Bado safari ni ndefu sana aisee, wanakwenda spidi mno. Mfano baada ya halima kununuliwa pale Kawe kuna mwanachadema yupi mwenye nguvu angalau nusu ya halima? Ukifikiria kwa mapana unaona mwandishi yuko sahihi sana.
 
Bandiko lako lilikuwa kuidunisha cdm na sio ccm ama vyama vingine. Au umezidiwa na hoja sasa unarukia chochote? Ni wapi umetaja vyama vinginge zaidi ya cdm against ccm? Nenda kwenye post yako namba moja kama kuna popote umeonyesha kuikanya ccm ama vyama vingine. Kama huna uelewa wa mambo, usijifanye mcha Mungu huku ukifumbia macho ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…