PreGE2025 CHADEMA; baada ya tamko la kutoshiriki Uchaguzi Mkuu, fanyeni haya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ndio maana tunataka ushindani wa haki, utaona watu ambao hujawahi kuwaona. Wengi hawana ujasiri wa kujitokeza kwenye chaguzi za kihuni. Kutokujua watu waliopo haimaanishi hawapo.
 
Uko sahihi sana Mkuu;

Mfano angalia mkoa wa Geita CDM wanaweza kupata majimbo mangapi tena wakiweka watu sahihi sana? Mkoa wa Singida je? Mkoa wa Tabora je? Mkoa wa Tanga je? mkoa wa Dodoma je? Mkoa wa Simiyu je? Mkoa wa Morogoro je? Mkoa wa Pwani Je? Mkoa wa Katavi Je? lindi?? Shinyanga je? Mtwara? Kigoma ni pro ACT kwa majimbo matatu hivi. Hata kule kwenye ngome zao, mfano Arusha wana majimbi mawili tu (strong red) Kilimanjaro (nako wana majimbo mawili tu strong red) Manyara (wana majimbo mawili tu strong red) Mbeya ni ngome lakini sio full red (wanagawana) halikadhalika Songwe... mara wana majimbo 3 strong red wanakwenda speed bure, kuna kazi kubwa inatakiwa kufanyika kuliko maneno. Ya sasa
 
Ndio maana tunataka ushindani wa haki, utaona watu ambao hujawahi kuwaona. Wengi hawana ujasiri wa kujitokeza kwenye chaguzi za kihuni. Kutokujua watu waliopo haimaanishi hawapo.
Ukiwa na watu kweli hata mzani ukiwaje utashinda tu (too big ti rig) refer kina Ndesa nk shida ni kwamba watanzania tuna hulka za kudeka. Ndicho CDM wanafanya. Kama EL alikuwa very strong lakini aliambulia wabunge 40+ tu katika kipindi ambacho CCM ilikuwa na migawanyiko mikubwa sana sembuse sasa mkuu? Kazi kubwa inatakiwa kufanyika. Kuna wagombea hata hawajulikani, mfano pale Nyamagana pambalu ana nguvu ya kumshinda mgombea strong wa CCM?
 
Unajua unachoongea au nibaki kwenye hilo neno lako huenda? Kama hujafanya utafiti ni bora kukaa kimya, ama andika kama mshabiki wa ccm.
Najua ninachokiongea, na hili swali niliuliza kwenu kuwa ni kipi mmewafanyia watanzania?

Umenijibu sawa, lakini huko walikoenda kwenye halmashauri mimi na wewe hatukuwepo a reason to why nikasema huenda kwa sababu mimi sijafanya utafiti na wewe kwa unavyoongea ni dhahiri kuwa ni maungo aidha ya habari au rumours ambazo na wewe umezisikia tu. Kama ni kweli, tafsiri yake ndicho ninachokipigania mimi; kwamba tumechoka siasa za mivutano, migogoro, kunyukana, kutukanana, n.k. kwani zinarudisha taifa nyuma.

Kingine kwa mfano kufungua 'company ya kuongeza thamani madini' kweli halmashauri nayo inazuia? Haya, ujasiriamali au business entities nayo halmashauri wanazuia? Tuache hayo, na kufungua migahawa ya chakula na ya kitalii nako halmashauri wanazuia? Kuwekeza kwenye utalii na kwenyewe halmashauri wanazuia? Mbona fursa za kijamii ni nyingi sana?
 
Asante nashukuru sana ndugu yangu kwa uchambuzi na kuelewa. High five!
 
Mkuu hakuna mwenye tatizo la kushindwa ama kushinda, tunataka uwanja sawa wa ushindani kisha ulete mrejesho hapa.
 
Hebu ukipata muda fanya utafiti, mimi ninaongea ambacho nina ushahidi nacho. Ww una nadharia za darasani.
 
Hebu ukipata muda fanya utafiti, mimi ninaongea ambacho nina ushahidi nacho. Ww una nadharia za darasani.
Jibu kwanza hili swali ndugu; kufungua bank ya kijamii (community bank) halmashauri nayo inazuia?
 
Nani wafungue community bank, cdm au nani?
Natolea tu mfano wa namna ambavyo huduma za kijamii ni nyingi; na bila shaka CHADEMA wangetaka pia wangeweza kufungua kwani hawasikii malalamiko ya watanzania kuhusu wanavyosumbuka na kuteseka na mikopo ya kausha damu kila siku?
 
Mkuu hakuna mwenye tatizo la kushindwa ama kushinda, tunataka uwanja sawa wa ushindani kisha ulete mrejesho hapa.
It doesn't work like that mkuu;

Upinzani unahitaji agenda setting ambayo haijielekezi kwenye election tu.

Unakumbuka miaka ya 2006 hadi 2012 hivi. Vijana wengi tulivutiwa na CDM kwa sababu ya agenda setting iliyokuwepo; ufisadi nk. Mimi binafsi nimepigwa mabomu mara 3 Arusha mwaja 2009 nadhani; tulioigwa kiwanjani jukwaani akiwepo SG na Chair na baadaye tulitaka tukamchukue mwanachama central. CDM ile ilikuwa na watu wa makundi mengi na wenye kujenga hoja vizuri bila papara; unamkumbuka JJM wa miaka hiyo? ZZK na uchumi wake? Kafulila nk? Leo watu hao wako wapi; kumekuwa na CDM mpya ya waropokaji na watukanaji na washambuliaji...

Imagine kina mdude siku hizi wanapewa mike, kina Sativa wanatukana matusi ya nguoni, kina pambalu wanaishia kupayuka tu hakuna utulivu.... too sad kwa sisi ambao CDM ilituvutia sana; wako wapi wazee wenye busara kama kina baregu, kina Prof Safari nk... kabla ya NRNE CDM inahitaji strategy mpya hii ya sasa ni useless... too sad lakini ndiyo ukweli

Na bahati mbaya vijana wa sasa wa CDM KILA uzi against wao humu majukwaani kazi yao ni kumshambulia mtoa hoja. CDM inazidi kujitenga na watanzania....
 
Mleta mada ishia hapo kabla sijawatuma malaika wangu wakuchalaze viboko,

Ccm ni vibuli, ccm wajiona ni nchi , ccm,ccm naita mara mbili wanaharibu nchi .ccm wanabambikia kesi ya huaini ,ccm haina jema , ccm imekwisha kabisa kabisa alisema dr Remmy( R.IP )

Ccm ,ccm mtavuna ambacho hamkupanda period
 
Natolea tu mfano wa namna ambavyo huduma za kijamii ni nyingi; na bila shaka CHADEMA wangetaka pia wangeweza kufungua kwani hawasikii malalamiko ya watanzania kuhusu wanavyosumbuka na kuteseka na mikopo ya kausha damu kila siku?
Kwanza cdm ni chama cha kisiasa na sio taasisi ya kifedha. Ccm pamoja na ukongwe wao wana bank? Kama kila taasisi itafanya unavyosema, basi team za mpira za yanga na simba zingekuwa na mabenk, mahoteli, viwanja vya mpira nk, ama wao hawaoni hizo fursa? Je team za simba na yanga kukosa hiyo miradi zimepunguza ushawishi wake kwa umma?
 
Unataka kuona cdm ya 2009 na sijui mwaka gani huko, lakini huangalii mazingira ya sasa. Unaongelea mazingira ambayo mpinzani alikuwa anaweza kwenda kwenye chombo cha habari na kufanya mdahalo, wakati sasa hivi ni tofauti. Unaongelea miaka ambayo bunge lilikuwa na spika anayeangalia hoja na sio chama anachotoka. Unaongelea wakati demokrasia ikiwa inaridhisha, unafananisha na sasa.

Sasa hivi polisi anajivunia kuwa mwanaccm hadharani, wakati katiba imetenga kabisa siasa na vyombo vya dola. Naona kama unataka uone vumbi likiwa linatimka juu ya bahari. Tazama uhalisia wa sasa, na sio hizo hadithi za hapo zamani za kale.
 
Aisee! Hii ni zaidi ya comment ndugu yangu. Kongole nyingi kwako
 
Haa! Malaika gani hao? Jeshi la Malaika lililo upande wangu ni kubwa kuliko jeshi lolote lingine. Sina hofu wala mashaka, kwa sababu ninaye BWANA wa majeshi. Kazi inaendelea!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…