Tuangalie wenzetu waliotutangulia katika demokrasia wanasemaje, naangalia demokrasia kwa sababu CHADEMA ni Chama Cha Demokrasia na Maendeleo. Demokrasia ipo katika jina la chama.
Mimi nakaa Marekani kuna demokrasia mpaka inakuwa fujo.
Katika majimbo yote 50 ya Marekani hakuna jimbo linalolazimisha chanjo.Yani wanaweza kukubana ukitaka kufanya kazi hii ni lazima upigwe chanjo, ukitaka kusoma shule hapa ni lazima upigwe chanjo. Hivi vitu vilikuwepo kabla ya Covid.Mimi nilivyosoma chuo hapa ilikuwa huwezi kuanza chuo kabla ya kuonesha ushahidi wa chanjo ya MMR (Measles,Mumps and Rubella). Lakini hakuna sehemu serikali ya Federal au State wanaposema ni lazima watu wote wapigwe chanjo.
Na siku serikali itakapolazimisha chanjo ndipo baadhi ya watu watu watachukua bunduki zao kuingia mtaani kuandamana.
Mimi napenda chanjo, nimechanja chanjo zote mbili za Pfizer, naona watu wanaokataa chanjo kuwa ni tatizo kubwa sana, kwa sababu wao ndio wanaosababisha mlipuko wa ugonjwa uendelee. Sasa hivi Marekani watu wanaolazwa mahospitalini kwa Covid na wanaokufa karibu wote ni wale waliokataa chanjo. 9 Covid deaths out of 10 in the US are for people who are unvaccinated.
See here
Reversing a months-long downward trend, deaths from COVID-19 have begun rising steadily this week. More than 99% of the recent fatalities were among people who had not been vaccinated.
www.npr.org
Lakini sitaki waingiliwe katika haki yao ya kukataa chanjo.
In fact hiyo inaweza kuwa a special case ya Darwinian evolution kuua watu wajinga na kuacha dunia iendelee na watu wenye maarifa.
Sasa mimi siku zote nimekuwa natetea haki binafsi za watu, kama mtu kachoka maisha anataka kufa kifo cha "suicide by Covid" mimi nina haki gani ya kumkatalia?
NPR wameripoti kwamba sasa hivi Marekani vifo vya Covid vinaongezeka, na 90% ya wanaokufa ni watu waliokataa chanjo.
Sasa mtu akitaka kufa mwenyewe mimi ni nani nimkatalie?
Reversing a months-long downward trend, deaths from COVID-19 have begun rising steadily this week. More than 99% of the recent fatalities were among people who had not been vaccinated.
www.npr.org