Ndallo,
Ni kweli hujakosea. Slaa hawezi kucheka wakati ndugu zake miaka 50 baada ya uhuru wanalilia ngozi wakati wachakachuaji wanalalia vono na wanaishi kwenye maghorofa bei mbaya kwa fedha za kiufisadi na uwizi. slaa hawezi kucheka wakati wananchi walio wengi wanaishi hawana uhakika wa mlo wao wa siku. Anayecheka ni yule tu anayesaza bila kugharimia kwa jasho lako au ananufaika kwa migongo ya Mafisadi na mfumo mbovu. Slaa hawezi kucheka wakati kwa dhahiri kabisa wachakachuaji kwa makusudi wanapiga mabomu wananchi wake wanaotaka kuchagua viongozi wao kidemokrasia kama inavyotokea jana na leo kule Buseresere Chato na kwingineko kunakofanyika kesho uchaguzi wa Madiwani, uchaguzi ambao hata sababu za kuahirishwa ni kiinimacho. Anayechekelea hali hiyo ni yule ambaye ni mbumbumbu na shabiki tu wa mambo asiyejua kinachoendelea katika nchi yake au kwa makusudi tu kwa sababu ya kiushabiki au kiulaji hataki kuelewa kuwa mambo siyo sawa. Ningeweza kuendelea zaidi na zaidi. Tucheke panapostahili kucheka, tufurahi palipo na sababu ya kufurahi. Lakini tuwe na "Hasira kali" kwa ajili ya ukombozi wa nchi yetu. Ukombozi kwa dhana yake ni lazima uendane na hasira isipokuwa kwa wale wasiojua maana ya ukombozi au mchakato wa ukombozi. Hao ni wa kusamehewa bure wala msiwatukane kwa sababu tunawajibu wa kuwakomboa na wao pia.
Hapo umenena ,unajua saa ingine inabidi tuwashe moto ili tupate moshi na baadae ndio turine asali, heshima Mkuu ,kitu kimoja ambacho mnakwenda nacho hadi kufikia tarehe ya kupiga kura ni kule kuwa sambamba na katiba mbovu na tume isiyokubalika popote pale penye mfumo wa vyama vingi.
Kosa ambalo linafanywa na vyama vya siasa ni kuingia katika uchaguzi huku vikijua fika kuwa ushindi hautopatikana hata kama mgombea wa CCM hakujipigia kura (Zanzibar Shein hakujipigia kura) na hapa Tanganyika hata kama Kikwete asingelikwenda basi bado angeliibuka mshindi au unasemaje Dr Slaa ??? Unaweza kufafanua ni kwa sababu gani zinazowezesha viongozi wa CCM kushinda bila ya kupiga au kujipigia kura ??
Labda niseme kwa nini tusijipange upya ? Tujipange katika kuandaa mazingira mapya ya kiuchaguzi ,kwani hivi sasa hakuna Mtanzania ambae anauona umuhimu wa kupiga kura kwani wakipiga wasipige bado CCM ataiba matokeo na kuyachezea atakavyo ,utanishawishije niende kupiga kura 2015 ikiwa hali iliyopo au iliyotokea haijapatiwa ufumbuzi ?
Njia ambazo zilitumiwa Zanzibar dhidi ya CUF ndizo hizo zinazotumiwa leo hapa Tanganyika ,kubadilisha matokeo ,moja ambalo halijafika huku Tanganyika ni kutumia mtutu wa bunduki ambako Zanzibar inasemekana hii ni mara ya pili mtutu unatumika ,Je hayo mtakabiliana nayo vipi ?
Kwa kweli wananchi wanataka kuhakikishiwa ni kwa namna gani kura zao zitahifadhiwa na kulindwa hadi yatakapotangazwa bila ya kubadilishwa ? Hili ni jambo muhimu ambalo linahitajika kufanyiwa kazi leo bila ya kuingojea kesho otherwise wapiga kura hawatanyanyua mguu kwenda kwenye vituo na kuwajibika katika upigaji wa kura.
Maoni yangu ni kuwa ushawishi mkubwa unahitajika katika kuibadilisha KATIBA hii na Tume na mfumo uliojiwekea wa kuwa wao wapo juu ya sheria.Hapa hapahitajiki Bunge katika kudai madai ya KATIBA mpya na Tume mpya , Vyama vya siasa ndivyo vinavyohitajika katika kuieleza jamii na kuishawishi kuungana katika kutoa kipaumbele cha madai ya KATIBA mpya na muda ndio huu kabla siku hazijaanza kupungua na kuambiwa kuwa mida haitoshi. La leo lifanywe leo na si vinginevyo.
Kama mlivyoweza kuwashawishi wananchi wawapigie kura kwa wingi na iliwezekana basi ndio hivyo hivyo itakavyowezekana katika kuwashawishi ili washikamane na kuwa kitu kimoja ili kuilazimisha serikali ikubali (Mwanasheria mkuu) kuibadilisha Katiba na likiwezekana hilo basi imani ya uchaguzi wa haki itarudi.